WEMA NI AKIBA YA JENNIFER MGENDI KUANZIA SAA NANE MCHANA

Ukitaja waimbaji wanaoheshimika sana ni nchini, basi jina la Jennifer Mgendi ni miongoni mwa watakaotajwa. Lakini si tu kuheshimika, bali pia kupendwa, na kutokuwa na kashfa. Ni mwanamama asiye na makuu. Kiufupi, anamuwakilisha Mungu vema.

Ni takriban miaka 20 sasa yuko kwenye huduma tokea arekodi albamu yake ya kwanza mwaka 1995 iliyoenda kwa jina la "Nini", na Mungu anaendelea kumuonekania kwa namna tofauti tofauti. Na leo hii ndani ya TAG DCT lililopo Tabata, anazindua DVD yake ya Wema ni Akiba. Huna haja ya kuuliza kiingilio, maana ni bure, cha muhimu ni kutafuta nauli yako ili uweze kuungana na mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuweza kumsifu na kumuabudu Mungu.


Jennifer Mgendi ©Jennifer Mgendi

Cosmas Chidumule, Mchungaji Ency Mwalukasa, Christina Matai, Rev Charles Jangalason, Lilian Kimola, Bahati Bukuku na Wito William ni sehemu tu ya waimbaji watakaomsindikiza Bi Mgendi, ambapo tukio hilo litashuhudiwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God, Dr Barnabas Mtokambali.

Tukutane kuanzia saa nane mchana DCT, Tabata Shule. lakini hatukuachi hivihivi, sikiliza wimbo unaobeba jina la DVD inayozinduliwa leo hii, Wema ni Akiba. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea tovuti yake, www.jennifermgendi.comShare on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.