ANGALIA PICHA ZA UBATIZO WA MJUKUU MPYA WA MALKIA ELIZABETH WA UINGEREZA

Malkia Elizabeth akiwa amekaa na Prince William, Prince George mtoto wa kwanza wa Prince William pamoja na mkewe Kate bila kumsahau mwenye tukio Princess Charlotte akiwa amebebwa na mama yake. Nyuma ni ukoo wa Kate mkono wa kushoto huku upande wa kulia ukoo wa malkia ukiongozwa na mumewe Prince Philip.

Siku ya jumapili iliyopita kulifanyika ibada ya ubatizo kwa familia ya malkia wa Uingereza Elizabeth wa pili pale ambapo mjukuu wake Prince William na mkewe Princess Kate Middleton walimbatiza mtoto wao wa pili aitwaye Princess Charlotte Diana Elizabeth aliyezaliwa hivi karibuni jijini London katika kanisa la Kianglikana la Mtakatifu Mary Magdalena lililopo Sandringham nchini Uingereza.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na watu walipoewa mwaliko wapatao 21, wakiwemo wazazi wa Kate pamoja na malkia na mumewe Prince Philip, babu wa mbatizwaji Prince Charles na mkewe Camilla pamoja na wengine kutoka ukoo wa kifalme. Huku mamia yakiwa yamefurika nje ya kanisa hilo kumpongeza binti huyo ambaye amepewa jina la mama mzazi wa Prince William marehemu Princess Diana pamoja na jina la malkia. Mpiga picha aliyepewa kazi ya kunasa matukio hayo anafahamika kwa jina la Mario Testino anayedaiwa kutofanya kazi siku za jumapili lakini kwa mwaliko kutoka katika familia ya malkia hakuweza kukataa kutokana na nafasi hizo kutopatikana kirahisi.

Picha ikimuonyesha Prince William alipokuwa mdogo akiwa amebebwa na mama yake marehemu Princess Diana, huku picha ya kati aakiwa amembeba mwanae wa kwanza Prince George na kushoto Princess Kate akiwa amembeba Princess Charlotte.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.