ASKOFU GWAJIMA AONGOZA FAMILIA NA WAUMINI WAKE KUJIANDIKISHA KUPIGA KURA

Kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Askofu Dkt Josephat Gwajima na familia yake wameongoza msururu wa baadhi ya waumini wa kanisa hilo pamoja na majirani kwenda kujiandikisha ili kupata vitambulisho vya kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwezi Octoba mwaka huu.

Katika picha mbili ambazo GK imezipata kutoka katika kundi la Ufufuo linaonyesha Askofu Gwajima, mkewe pamoja na binti yao na waumini wa kanisa lake wakiwa wenye furaha katika foleni hiyo, mapema asubuhi ya leo huko Salasala jijini Dar es salaam.

Askofu Gwajima amekuwa akipamba vyombo vya habari kwa misimamo yake kwenye masuala ya ki Mungu na kisiasa ambayo imeonekana viongozi wengi wa kisiasa hupenda kuwa karibu na Askofu huyo kutokana na ushawishi wake kwa waumini wake zaidi ya 70,000 ambao huudhuria ibada kwa wiki kanisani hapo.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.