BAADHI YA CHANGAMOTO ZA KUOA MWANAMKE ALIYEKUZIDI MIAKA MINGI KULIKO KIWANGO MUAFAKA!

Mchungaji Peter Mitimingi, mkurugenzi wa huduma ya VHM

BAADHI YA CHANGAMOTO ZA KUOA MWANAMKE ALIYEKUZIDI MIAKA MINGI KULIKO KIWANGO MUAFAKA!
i. Maneno maneno ya kuvunja moyo kutoka kwa jamii
Inapotokea mwanamke akawa na miaka mingi sana kuliko mumewe jamii huweza kuongea maneno ambayo wakati mwingine huwakosesha raha na amani.

ii. Kukosa Uhuru wa kuwa na Mwenzi wako Hadharani.
Kutokana na maneno ya watu mitaani, kanisani, kazini na kwingineko mnaweza kukosa uhuru wa kuongazana pamoja au kumtambulisha kwa marafiki au inapotokea mmealikwa kwenye sherehe au hafla fulani unapata utata wa kuongozana kutokana na kuhofia kunyooshewa vidole na watu kwa kuwasema vibaya.


iii. Kupishana kwa mapendeleo na maslahi “Hobbies & Interests" Baina ya Wanandoa Hao
Moja ya changamoto inayowakabiri wanandoa ambao wamepishana umri wa miaka mingi ni kwamba mmoja atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa kiujana na mwingine atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa Kiutuuzima au ulimwengu wa uzee. Tatizo litakalotokea hapa kila mmoja anajaribu kumvuta mwenzake kwenye ulimwengu wake.

iv. Changamoto ya Kutoendana na Kuangalia Nje ya "Fance"
Kadri miaka itakavyozidi kwenda ile "gap" ya umri itakuwa ikijitokeza kwa ukubwa zaidi. Kijana ataanza kuona huyu mzee hatuendani namimi yupo nyuma ya wakati na kuanza kuvutiwa zaidi na mtu mwingine wa rika lake. Mfano kama kijana ameoa mwanamke ambaye wamepishana sana umri, kijana anaweza kutamani mkewe awe anavaa yale mavazi ya ujana ambayo huvaliwa na wasichana mitindo na mishono ya kiujana ili atakapokutana na marafiki zake waone kuwa ana mwanamke ambaye anakwenda na wakati. Kwa upande wake huyo mwanamke kulinganana umri wake hawezi kuthubutu kuvaa mavazi ya kiujana kama hayo na hapo mgogoro huweza kutokea na wote wawili kuona kuwa hawaendani kabisa.

v. Imani ya kwamba Ndoa ni Kwajili ya Kupata Watoto
Katika tamaduni na mazingira yetu ya Kiafrika, umri wa mwanamke anapoolewa ni wa msingi sana hasa linapokuja swala la kuzaa watoto. Kwa tamaduni za kiafrika swala la kuzaa watoto katika ndoa ni jambo la msingi sana kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo mwanaume anapooa anakuwa na mategemeo kwa sehemu kubwa kwamba atapata watoto kupitia mke ambaye anamuoa.

vi. Jamii Huamini kwamba Mwanamke Mwenye Umri Mkubwa Atashindwa Kuzaa.
Jamii nyingi huamini kwamba kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza kushindwa kumzalia watoto mumewe. Kulingaana na watafiti wanasema kwamba kadri mwanamke anavyoziku kuongezeka umri ndivyo ambavyo viungo vyake vya uzazi hupoteza uwezo wake wa kushika mimba na kuzaa watoto.

Pamoja na hayo yote bado tunaamini kwamba hata katika mazingira magumu yasiyo na njia Bwana bado anaweza kufanya njia mahali pasipo na njia na anaweza kukutokezea hata katika dakika ya mwisho.
NIKIRUDI NITAKULETEA SASA MIAKA FUAFAKA YA WACHUMBA KUPISHANA!
STAY TUNED!
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.