BWANA YESU AMFUFUA BINTI WA JUMBE

Picha ya maiti ikiwa imehifadhiwa chumba cha maiti, haina uhusiano na habari hii ©independentUK

Kutoka kwa Mchungaji Gasper Madumla.

Bwana Yesu asifiwe…

Ipo miujiza mingi aliyoifanya Bwana Yesu ambayo laiti kama ingeliandikwa miujiza yote katika biblia basi ni dhahili kabisa biblia isingebebeka maana ingekuwa kubwa mno (Yoh 21:25 ). Muujiza mmoja kati ya mingi iliyotendeka,ni huu wa kufufuka kwa binti jumbe. Yapo mambo mengi ya kujifunza katika muujiza huu. Biblia inasema;

” Alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi.

Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. 25 Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama.Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote. ” Mathayo 9:18-19 & 23-26

Biblia inasema kwamba Yesu alipokuwa angali akinena ndipo jumbe mmoja alimjia. Sasa katika muujiza huu tunajifunza mambo kama manne hivi. Jambo la kwanza ni;

▪Kumwendea Yesu,Bwana wa utukufu.

Jumbe anatufundisha kanuni ya kupokea uponyaji na muujiza wa kufufuliwa mambo yako yaliyokuwa yamekufa. Hivyo jambo la kwanza kabisa pale upatapo msiba ni kumwendea Yesu pekee ambaye kwake kilichokuwa kimekufa kinauhishwa tena,kinafufuliwa maana Yeye hashindwi na kitu.

Kufufuliwa kwa binti jumbe kulimuhitaji jumbe aende kwa Yesu,maana laiti jumbe huyu asingelienda kwa Yesu basi ni dhahili wale waombolezaji wangemzika binti yake. Jumbe,ni kama vile alikataa taharifa ya msiba akaona binti yake ataishi tena,na ndivyo tunavyojifunza kukataa taharifa zote mbaya hata kama zinaonekana ni za ukweli,lakini waweza kuzipindua taharifa hizo za mauti kwa kutamka uzima ukilitumia jana la Yesu Kristo Yeye kiboko ya mauti.

Sikia,hata kama umeambiwa na daktari kwamba unaumwa UKIMWI wewe kataa UKIMWI katika roho,kisha tamka uzima kwa jina la Yesu Kristo mwenye kuhuisha tena.

Kama jumbe asingemuendea Yesu,basi yule binti angezikwa.Sasawaweza kujiuliza kwamba ni mara ngapi umeyazika mambo yako uliyoyaona kwamba yamekufa,kwa sababu umeshindwa kumuendea Yesu,Yeye afufuaye?

Maana laiti ungelimfuata Yesu,mambo yako yaliyokufa yasingelizikwa. Mfano mdogo ni huu,; rafiki yangu mmoja aliyekuwa anafuga paka nyumbani kwao. Sasa siku moja paka wake mmoja alikula sumu akaishiwa nguvu,hata paka huyo akajinyoosha chaliii.

Paka yule kwisha habari yake..!! Baadae alionekana kafa kabisa!sasa watu wa nyumbani walianza kufikilia ni wapi watachimba ili wamfukie sababu amekufa. Lakini huyu ndugu alipofika nyumbani naye akitaraji amzike paka wake,lakini gafula Roho akamwambia hajafa huyo paka wako,muombee tu.

Hivi,unajua ni vigumu kumuombea paka,maana utajiuliza sasa ya nini maombi kwa paka?,tena paka mwenyewe unajua hata haemi kabisaa,yaani kamekufa. Ndugu akaomba pale,akamuekea mkono mara kale ka paka kakazinduka kutoka umautini,kakaanza kuhema kwa mbaaali,kisha uzima ukaonekana kwa paka.Kilichomfufua huyu paka ni Bwana Yesu,kama binti wa jumbe alivyopewa uzima baada ya kufa.

~ Wote waliomkimbilia Yesu,walitendewa jambo la ajabu. Jumbe akaona ni vyema aende kwa Yesu kumpelekea msiba wake. Wewe pia yawezekana una msiba ndani yako,mpelekee Yesu naye akuponye na msiba huo. Tazama hatua ya pili ya jumbe aliyoichukua kwa mujibu wa Mathayo 9:18,andiko lililopo hapo juu alichukua hatua ya kusujudu mbele za Bwana kabla hajamueleza Yesu chochote kile.

▪Kumsujudia Bwana.

Kabla hata ya kuomba kwako yakupasa ushuke mbele za Bwana,maana Yeye anastahili kuinuliwa. Jumbe alipogundua hilo akamsujudia Bwana pasipo kuanza na chochote kile. Kusujudi ni kuabudu,kusujudu ni kumuinulia Bwana utukufu,Yeye mwenye uweza na uwezo wote. Sasa wapo watu wenye misiba mioyoni mwao ambapo wanaiangalia misiba hiyo sana kiasi kwamba wanashindwa kumuabudu Mungu wa kweli.

Msimba wako usikufanye ushindwe kusujudu/kumuabudu Mungu katika roho na kweli. Kuabudu ni moja ya njia ya kutendewa muujiza wako; Jumbe akachukua hatua ya tatu ambapo alitamka hoja moja yenye nguvu kwa Yesu kuhusu msimba wake.

▪Kueleza hoja yako yenye nguvu mbele za Bwana.

Hivi unajua kwamba Jumbe ingawa alikuwa ana msiba wa binti yake;lakini alikuwa ana hoja nyingi ambazo angeliweza kumueleza Yesu kwa wakati ule ili asaidiwe saa ile alipomuendea.

Maana labda mmoja leo angekutana na Yesu katika msiba wake angeliweza kumueleza hoja zaidi ya msiba wake,mfano ” Baba uniponye na msiba huu,pia nahitaji pesa,alafu nipatie mume/mke,Baba ninashida ya kujenga….” Lakini sivyo alivyofanya Jumbe,yeye aliweza kumueleza Yesu hoja moja yenye nguvu pasipo kupindisha pindisha ( Mathayo 9:18 )

Yawezekana shida hii ya kushindwa kupeleka hoja ya msingi mbele za Yesu,ukawa nayo na wewe. Maana wapo watu ambao huomba mambo mengi yasiyopangiliwa kwa wakati mmoja wawapo mbele za Bwana. Kuwa na maombi mengi sio shida,shida ni kukosa hoja kamili yenye nguvu iliyopangiliwa sawa sawa na neno la Mungu lisemavyo katika Isaya 41:21. Jifunze kwa Jumbe huyu,tazama jumbe aombavyo ”... binti yangu amekufa,njoo uweke mkono wako juu yake,naye ataishi.” Ni ivo tuu,.

Kwa mfano wa Jumbe tunajifunza kuwa maombi pasipo imani kwa kile ukiombacho hayana matunda,bali maombi yakisimama katika imani huzaa matunda. Jumbe alikuwa na imani,kisha akaomba na majibu akayapokea ( Mathayo 21:21 )

▪ Usione shaka,bali amini na yatatendeka.

Jumbe hakuwa na shaka,ndio maana anasema ”… muwekee mkono wako kisha ataishi…”

Biblia inazidi kutueleza kuwa Yesu alipofika nyumbani kwa yule Jumbe aliwaondosha wale waombolezaji na wapiga filimbi kwa sababu waombolezaji walimuona kijana amekufa,lakini sivyo alivyomuona Yesu,bali Bwana alimuona kijana amelala.

Nilipokuwa nikisoma andiko hili ( Mathayo 9:23-24 ) nikajiuliza kwamba kwa nini Yesu aliwaondoa wale waombolezaji,ili atende muujiza wa kumfufua binti Jumbe? Au kwa nini asingetenda jambo hili wakiwepo waombolezaji ?

Ndiposa nikagundua kwamba aliwaondosha waombolezaji ikiwa ni moja wa mfano ambao anatufundisha sisi maana si kana kwamba hakuweza kutenda muujiza mbele za macho ya watu wote bali kulikuwa na fundisho kubwa alilokuwa akifundisha kwa mfano.

Hapo ni kama vile anasema kwamba ukitenda jambo jema usipende kujikweza/kujionesha kusudi upate sifa fulani hivi na ndio maana mara nyingi Yesu Kristo alipotenda miujiza aliwaagiza wasimuambie mtu yeyote. Lakini pia tunajifunza kwamba wakiwemo wenye kuamini huku wakiwa wamechanganyika na wasioamini basi ni afadhali sana kujitenga na wasioamini ili wale wenye kuamini ushughulike nao papo hapo maana wenye kuamini wasije wakarudishwa nyuma mioyo yao na wasioamini katika msiba wao.

Wapo watu wenye kuisonga imani yako,watu hawa ni wataabishaji. Wenyewe hucheka sana juu ya kile unachokiamini. Ikiwa utawatazama hawa hakika muujiza wako hautafanikiwa,sababu wenyewe wapo kinyume na wewe kiimani. Bwana Yesu alipowatazama na kuwaona awaamini kabisa,ilimbidi awaondoshe.

Lakini pia Yesu alitizama msiba wa jumbe katika roho,na kuona hajafa binti bali wale wengine waombolezaji walitazama msiba katika macho ya damu na nyama wakaona mauti kwa binti,ndiposa nasi tunahitaji kuyaangalia mambo yetu kwa macho ya rohoni.

Ndipo tunaweza sema biashara hajafa,fulani hajafa, au waweza sema uchumi wangu hajakufa hata kama watu mfano wa waombolezaji wakitangaza umauti bali wewe ukiwa wa rohoni utagundua na kurejesha uzima kwa kutamka uzima katika uweza wa jina la YESU KRISTO,na kila kitu kitakuwa kizima.

Mungu akusaidie ili awaondoshe watu wa namna hiyo katika maisha yako ya imani. Ninajua kwamba upo msiba maishani mwako,lakini sijui ni msiba wa aina gani,lakini Mungu aliye sirini akujua vyema. Leo ujumbe huu ni wa kwako maana Yesu Kristo mnazareti yupo hapa apate kuponya kama alivyotenda kwa binti jumbe.

Waweza kunipigia kwa namba yangu ili kwa pamoja tukaombe,piga sasa 0655111149.

Mchungaji Gasper Madumla.

S.L.P 55051,Dar.

Beroya bible fellowship church.( Kimara baruti,Dar-Tanzania ).

UBARIKIWE.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.