CHAGUO LA GK NI KUTOKA KWA MOJA YA KWAYA KONGWE TANZANIA


Leo katika chaguo la GK tupo na kwaya kongwe nchini ambayo hata hivyo haifahamiki sana kama ilivyo kwa kwaya pacha kutoka kanisa moja na usharika mmoja. Nazungumzia kwaya ya Upendo kutoka kanisa la Anglikana la Mtakatifu James Kaloleni jijini Arusha kanisa ambalo pia ndipo inapotea kwaya maarufu ya Tumaini Shangilieni.

Upendo waliweza kujitambulisha vyema kwa wapenzi wa muziki wa injili miaka ya 2000 walipotoa video yao ya kwanza ifahamikayo 'Furaha Gani' kisha wakapitisha ukimya wa muda mrefu sana na kufanikiwa kutoa video ya pili mwaka 2011 kupitia video hiyo nimekuchagulia wimbo uitwao 'Ndugu zangu'. Natumaini utabarikiwa utazamapo na kusikiliza ujumbe uliopo kwenye wimbo huu.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.