HABARI PICHA: MWILI WA MCHUNGAJI SICHINGA WAAGWA NA KUZIKWA JIJINI DAR

Mojawapo ya t-shirt zilizochapwa
Katika kuuaga mwili wa aliyekuwa mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Tabata Bima Mountains Movers na pia ni katibu wa umoja wa makanisa ya kipentekoste (CPCT) jijini Dar es salaam mchungaji Geoffrey Sichinga ulihudhuriwa na viongozi wa dini na madhehebu mbalimbali na kuuaga mwili huo.
Mwili ukiwa umeshawasilishwaNeno la Mungu limehubiriwa na askofu wa Jimbo la Mashariki Kusini ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Amani Christian Center, Askofu Dkt Lawrence Kameta ambapo alisema kuwa kuna hukumu za wanadamu na hukumu ya Mungu na katika hukumu hizo za wanadamu kuna upendeleo na kuhangana ila ya Mungu ni ya haki na kweli.

Alisema kuwa kwa hali ya kawaida wanadamu wengi wanaonewa na kukosa haki zao za msingi kutokana na hukumu ambazo wanadamu wanazitoa mara nyingi ni za kupindisha. 
Makamu Askofu mkuu wa TAG Askofu Magnus Muhiche akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya ofisi kuu ya TAG.
Askofu Muhiche na mke wake
Mwinjilisti Emanuel Nicodemus akiwa katika msiba wa mchungaji Sichinga.
Askofu Geofrey Masawe kutoka kushoto akiwa na mwangalisi Ibrahim Ashambwa.
Baadhi ya wachungaji na maaskofu ambao wamehudhuria katika msiba.

Kutoka kushoto ni Askofu wa jimbo la mshariki kaskazini DKT Lawrence Kameta akitetajambo na mmoja wa wachungaji katika ni askofu wa jimbo la mashariki kaskazini na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Mabibo Sahara Spiritual Center Askofu Geofrey Masawe na kulia ni mwangalizi Ibrahimu Ashambwa.Katibu mkuu wa umoja wa makanisa ya kipentekoste Tanzania CPCT na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la Naioth Gospel Assembly, Askofu Dkt David Mwasota akiwasili katika eneo la msiba.
Mke wa mchungaji Sabinus Mbogo katikati akiwa na waombolezaji
Mke wa mchungaji sichinga kulia akiwa na majozi kwa kuondokewa na mume wake.Baadhi ya waumini ambao walihudhuria katika mazishi ya mchungaji Sichinga.


Mhubiri kutoka Uganda mmoja wa mapacha wa Uganda KATO ambao wamekuwa wakifanya huduma mara nyingi katika makanisa mbalimbali hapa nchini.

WAumini wakifuatilia kwa makini ratiba inayotangazwa na mtu ambaye hayupo pichani.Askofu wa jimbo la mashariki kaskazini na pia ni mchungaji kiongozi wa kanisa la TAG Sahara Spiritual Center Mabibo Askofu Geofrey Masawe.akitoa salamu za rambirambi.Wakati mwili ukiwasili maeneo ya Ilala alipokuwa akiishi.Ndugu wa karibu na marehemu mchungaji Sichinga wakiwa na watoto wake na mke wake.Waumini wa kaisa la Wadventisti Ilala wakiwa na mchungaji wao ambao walishiriki katika msiba na kuimba wimbo wa faraja pia walitoa salamu za rambirambi.

Mchungaji wa kanisa la EAGT kwa Asis Aly akitoa heshima za mwisho.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa kuuaga mwili kwa kutoa heshima za mwisho.
Godfrey Sichinga amezaliwa tarehe 15 Septemba 1973, na kufariki 15 Julai 2015 na kuzikwa kwenye makaburi ya Segerea Jijini Dar es Salaam.

Habari na picha kutoka Amani na Furaha blog
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.