HABARI PICHA: SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA KUMI BCIC MBEZI BEACH

Maelfu ya watu walijitokeza siku ya jumamosi ya june 4 katika ukumbi wa kituo cha maombezi na ushauri wa kibiblia BCIC Mbezi beach katika sherehe ya shukrani kwa Mungu kwa miaka kumi ya BCIC  makao makuu mbezi beach  na sherehe hizo zikiongozwa na mwangalizi mkuu wa Wapo Mission International askofu Sylvester Gamanywa.

Mbali ya maelfu ya watu kujitokeza pia waimbaji mbalimbali walikuwepo wakiwa pamoja na Kinondoni Revival, KKKT Kigogo Uinjilisti Kwaya, John Lisu na Kwaya ya watoto BCIC pamoja na waimbaji wengine. Ambapo pia watu walipata wakati wa kula na kunywa katika sherehe hiyo.

Akizunguza katika sherehe hiyo Askofu Sylvester Gamanywa amemshukuru Mungu kwa kuwezesha huduma hiyo kuwahudumia watu wengi kw kipindi cha miaka kumi. Pia ameongeza kuwa mkakati ni kuendelea kutangaza injili na kuwafikia wengi zaidi. Na kwa kufanikisha hilo kituo hicho kimepanda kuelekea mikoani ambayo ni Arusha , Mwanza na Mbeya.

Askofu Gamanywa ameongeza kwa kusema kuwa kwa sasa wanahitaji kupanua usikivu wa matangazo ya kituo cha Wapo radio fm kusikika mikoani mkakati ambao umeshaanza kufanyiwa kazi.

Zifuatazo ni baadhi ya picha za matukio katika sherehe hiyo


ASKOFU GAMANYWA AKIELEZEA MAFANIKIO 

Mwangalizi wa makao makuu BCIC Mbezi Beach Askofu John Rwezaura akizungumza.


JOHN LISU AKIWA NA TIMU YAKE
 

KINONDONI REVIVAL NA WATU MBALIMBALI WAKIFUATILIA
Dr Makenzi kiongozi wa kwaya ya Kinondoni Revival
Philemon Rupia maarufu kwa jina la Father Rupia (mwenye camera) nae alikuwepo kupata matukio
Askofu Sylvester Gamanywa akiwa na mke wake
Add caption
Watoto wa Askofu Gamanywa wakiwa na ndugu zao
Ai Laizer mtangazaji wa Wapo Radio nae alikuwepo

KWAYA YA WATOTO BCIC

ASKOFU MICHAEL PETER AKAFANYA CHANGIZO LA ZIARA YA MIKOANI 


KIGOGO UINJILISTI KWAYA

MAOMBEEZI PIA YALIFANYIKAZAWADI ZIKATOLEWA
Mhariri wa gazeti la Msema Kweli na Wapo Radio Elibariki Minja (katikati) akiwawakilisha wafanyakazi wa vyombo hivyo vya habari kutoa zawadi ya ua la upendo kwa Askofu Gamanywa na mke wake allhappiness 
Mkurugenzi wa Huduma za jamii wa wapo Mission International Bwana Respicius Mwesiga akizungumza baada ya kukabidhi zawadi ya kalenda ya computer


WATU WAKAPATA CHAKULA CHA PAMOJA

WAIMBAJI WAKIBADILISHANA MAWAZO NA KUAGANA


TUPATE NA SISI YA KUMBUKUMBUHizo ni baadhi ya picha za matukio ya sherehe ya kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka kumi kituo cha Maombezi na Ushauri wa Kibiblia  BCIC Mbezi Beach makao makuu jijini Dar es salaam.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.