KIWANGO MUAFAKA CHA KUPISHANA UMRI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME WANAO TARAJIA KUOANANa Mchungaji Peter Mitimingi
Mkurugenzi wa huduma ya VHM


KIWANGO MUAFAKA CHA KUPISHANA UMRI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME WANAO TARAJIA KUOANA!

KWA MWANAUME:
Inashauriwa kwamba kwa mwanaume miaka 5 hadi 10 inafaa kupishana na mwanamke anayetarajia kumuoa. Kwamaana ya kwamba mwanaume anaweza kuoa mwanamke ambaye yeye mwanaume anakuwa amemzidi huyo mwanamke miaka miwili, mitano hadi 10. Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu hiyo ni sawa.

KWA MWANAMKE:
1. Inashauriwa pia kwa mwanamke kuzidi miaka 2 hadi miaka 5 kwa mwanaume anayetarajia kuolewa naye. Hii inamaanisha kwamba mwanamke akimzidi mchumba wake au mume wake miaka miwili hadi mitano itakuwa ni sawa hakutakuwa na tofauti kubwa sana wala madhara makubwa.

2. Kuna Athari kwa wanandoa wakipishaza zaidi ya miaka 10.
Wanandoa wanapokuwa wamepishana kwa zaidi ya miaka 10 kunakuwa na utafauti mkubwa katika kuhusiana kwao kama jinsi tulivyokwisha elezea. BONYEZA HAPA KUSOMA

3. USHAURI KWA WACHUMBA WALIOPISHANA UMRI MKUBWA
Wachumba ambao wana tofauti kubwa ya umri wao, wanashauriwa kutafuta ushauri kwa washauri wazuri (good counselors) kabla ya kuoana. Hata hivyo bado Mungu ni wa neema na miujiza anaweza akatenda hata kwa mwanamke au mwanaume mwenye umri mkubwa kuliko mwenzake hata kama ameshapitisha muda wa kuzaa au na mambo mengine Bwana bado hashindwi.
Luka 1:37
Kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Wafilipi 4:13
Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.