KONGAMANO LA PENUEL 2015 LILIVYOFANA KAWE

Mwenyeji wa PENUEL 2015 Apostle Onesmo Ndegi na Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre Kawe
PENUEL Maana yake mahala pa Kukutana na Mungu uso kwa uso. (Udhihirisho wa Utukufu wa Mungu) Mwanzo 32:22-30. PENUEL 2015 ni kusanyiko la mafundisho ya Neno la Mungu likiwa limelenga ukutane na Mungu kupitia haja ya moyo wako katika kila kona ya maisha yako. PENUEL 2015 likijumuisha watumishi wa Mungu waliotoka katika nchi mbalimbali za Afrika kwa mwaka huu watumishi walitoka Afrika Kusini, DRC, Kenya na Tanzania.

Apostle Onesmo Ndegi na Kiongozi wa huduma ya Living Water Centre ndiye mwandaaji wa kusanyiko hilo ambapo hapo mwanzo miaka ya nyuma lilikuwa likifanyika ila likijulikana kwa majina tofauti tofauti, lakini kwa mwaka huu 2015 na kundelea mbele litajulikana kama PENUEL kisha mwaka husika wa kusanyiko hilo, yaani PENUEL 2015.

Watumishi waliohudumu katika PENUEL 2015 ni Rev. Dr. Muteba Peter kutoka Johannesburg, Afrika Kusini ambaye ni Kiongozi wa Breakthrough Ministry Conference (BMC), pia Mchungaji Kiongozi wa Yahweh Shammah Assembly huko Johannesburg Afrika Kusini, Apostle Aaron Timothee Tshimanga kutoka Lubumbashi, DRC. Prof. Dr. Zacharie Mayamba Kabengele kutoka Lubumbashi, DRC. Bishop Olam Mustapha kutoka Gloryland International Church Arusha, Tanzania. Bishop Tengu Yoka kutoka Nairobi, Kenya na Pastor Moses Ilunga pia kutoka Nairobi.

Kusanyiko hilo la PENUEL 2015 limefanyika kwa muda wa wiki moja kwa mafunindisho ya Neno la Mungu kuanzia asubuhi mpaka jioni, ambapo watu walipata kujifunza na kujua ahadi za Mungu katika Maisha yao. Pia maombezi kwa wenye shida na matatizo mbalimbali yalifanyika siku ya mwisho wa Kongamano hilo.

Zifuatazo ni picha za matukio, kama ambavyo GK imezipata kutoka idara ya habari kanisani hapo.

Rev. Dr. Muteba Peter ambaye ni kiongozi wa Breakthrough Ministry Conference (BMC) na Mchungaji Kiongozi wa Yahweh Shammah Assembly huko Johannesburg South Africa mmoja katika wanenaji wa PENUEL 2015 
Bishop Olam Mustapha kutoka Gloryland International Church  Arusha Tanzania
Bishop Tengu Yoka kutoka huduma ya Resurrection Temple Nairobi Kenya 
Apostle Aaron Timothee Tshimanga kutoka Lubumbashi DRC
Pastor Moses Ilunga kutoka Resurrection Temple Nairobi Kenya 
Prof. Dr. Zacharie Mayamba Kabengele from Lubumbashi DRC 
 Apostle Onesmo Ndegi akizungumza katika Mwenyeji wa PENUEL 2015Joshua Mlelwa alikuwepo kuhudumu katika PENUEL 2015 
Watumishi wa Mungu kutoka nchi mbalimbali waliohudumu katika PENUEL 2015 wakiwa na wake zao katika picha ya pamoja
Watumishi wa Mungu kutoka nchi mbalimbali waliohudumu katika PENUEL 2015 
Wake wa Watumishi wa Mungu kutoka nchi mbalimbali waliohudumu katika PENUEL 2015 

Living Waters wenyeji wakiongoza sifa katika PENUEL 2015
Living Waters wenyeji wakiongoza sifa katika PENUEL 2015

Waumini wakicheza na Kuimba mbele za Bwana
John Mmbaga katika Drums
Barikeyz Mmbaga katika Piano

Watoto wakionesha ujuzi wao katika kupiga guitar
Pendo Mwamlenga wa Living Waters akiongoza sifa
Rodney wa Living Waters akiongoza sifa
Living Waters akiongoza sifa na kuabudu
wakicheza mbele za Bwana
wakicheza mbele za Bwana
wakicheza mbele za Bwana


Watumishi wakifuatilia mahubiri kwa makini
Watumishi wakifuatilia mahubiri kwa makini
Watumishi wakifuatilia mahubiri kwa makini
Washirika wa Prof. Dr. Zacharie Mayamba Kabengele kutoka Lubumbashi walioambatana nae kuja katika PENUEL 2015
 Washirika wa Kanisa la Yahweh Shammah Assembly huko Johannesburg South Africa walioongozana na Mchungaji wao  Rev. Dr. Muteba Peter katika PENUEL 2015
Baadhi ya wageni kutoka Lubumbashi waliokuja kuhudhulia PENUEL 2015

GUG Dancers
Paul Clement alikuwepo kuhudumu katika PENUEL 2015

The Doxas kutoka Word Alive walikuwepo kuhudumu katika PENUEL 2015
The Doxas kutoka Word Alive walikuwepo kuhudumu katika PENUEL 2015
The Doxas kutoka Word Alive walikuwepo kuhudumu katika PENUEL 2015

Mombezi kwa wenye matatizo mbalimbali

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.