KUSUDI LA MAJIRA YAKO CHAINGIA MTAANI KWA NJIA YA SIMULIZI


Kama umekua mfuatiliaji mzuri wa tasnia ya injili, bila shaka Fred Msungu halitakua jina geni kwako.

Na kama hujawahi kabisa kumsikia, basi Fred ni kijana ambae ni muanzilishi wa huduma ya PURE MISSION ambayo lengo lake kubwa ni kufanya mapinduzi ya fikra kwa kuleta maarifa mapya kwa watu kwa kutumia Neno, ambayo inawafikia watu kwa njia mbali mbali kama vile

-Semina/maongezi hamasishi na mahubiri
-Mafundisho ya vitabu, makala, CD, DVD
-Vipindi vya Radio & Television nk.

Pia amekua akionekana kwenye majukwaa mbalimbali kama MC wa matukio mbalimbali, mwanamuziki na mpigaji wa vyombo vya muziki.

Kwa mujibu wake, Fred anaeleza kuingia kwenye historia kwa mara ya kwanza Tanzania kuwa mtu wa kwanza aliyefanya AUDIO BOOK (Kitabu sauti) Jina la kitabu ni KUSUDI LA MAJIRA YAKO.

Alipoulizwa kwanini ameamua kuja na wazo hili, kwa maneno yake anasema,

"Nimepata wazo hili la kufanya audio book baada ya kutambua kua watu wengi hawajajenga utamaduni wa kusoma vitabu lakini watu hawa pia kuna maaarifa /taarifa muhimu zilizoko vitabuni ambazo wanazihitaji pia. Hivyo nadhani audio book ni njia rahisi sana na ya mbadala ya watu kuweza kupata ujumbe kwa haraka, lakini ni njia ya kisasa pia... mtu unaweza kuweka katika simu yako ukasikiliza au gari lako na hata nyumbani pia, kwa hiyo kama wewe ulikua hausomi kwasababu unaona uvivu wa kurasa nyingi basi sasa hauna sababu tena kwasababu kitabu kipo kwa mfumo wa sauti kazi kwako wewe tu kusikiliza"

Sikiliza utangulizi wa kitabu hicho;

Kwa wewe ambae ungependa kupata nakala yako ya kitabu hiki tafadhali wasiliana nae kwa njia zifuatazo;


Simu: 0653 318117
Barua pepe:fredymsungu@gmail.com
Facebook: Fred Msungu
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.