KWA TAARIFA YAKO: ISIS WANAVYOITOLEA MACHO ISRAEL KWA TAMAA

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.

Kuchinjwa ni tukio la kawaida kwa kundi la IS, pichani wananchi wakishuhudia tukio hilo. ©Mirror
Ni taarifa za kawaida kwenye vyombo vya habari kusikia kuna ugomvi, kujitoa mhanga na kujilipua, kuvamia makazi ya watu, kurusha makombora, na hata kupita chini kwa chini kwenye mahandaki ili kufanya mashambulizi kwenye taifa la Israel. Haya hufanywa na kundi lijiitalo Hamas, kundi ambalo limekuwa likifanya mashambulizi ya mara kwa mara licha ya kwamba kumekuwa na makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano. Hilo Hamas hawaliangalii.

Hamas, kundi la kiislamu nchini Palestina ambalo limeanzishwa mwaka 1987 kwa nia ya kisiasa na kundi la mapigano, limekuwa likifanya mashambulizi ya aina mbalimbali, lengo ikiwa ni kuifuta Israel katika historia ya dunia na badala yake kuiweka Palestina. KWA TAARIFA YAKO licha ya kwamba wengi wanalifahamu kundi hili kwa jina la Hamas, mashambulizi hufanywa na idara yake iitwayo Izz ad-Din al-Qassam

Watoto wakiwa wamejihifadhi kwenye mahandaki kwa ajili ya usalama wao wakati wa shambulizi la mabomu ya masafa marefu (rockets) nchini Israel.
Wakati Hamas wakiendelea na maisha yao ya mashambulizi kwa taifa la Israel, kundi la kiislamu lenye itikadi kali la Islamic States (ISIS), lenyewe KWA TAARIFA YAKO limerusha lawama kwa Hamas, na kutishia kulishambulia, kwa kuwa linaonekana kutofanya kazi yake ipasavyo (mashambulizi) ili kuikomboa Palestina.

Katika taarifa ambayo wameitoa hivi karibuni, ISIS wameeleza kwamba Hamas wameshindwa kazi yao, na kwamba kinachoendelea hivi sasa nchini Syria KWA TAARIFA YAKO ndicho kinachotakiwa kutokea Ukanda wa Gaza, ambapo Hamas wanaonekana kulegalega.

Kwa mantiki hiyo, Israel watakuwa wanatazamia adui mpya ambaye dhahiri ameonekana kuteka akili ya baadhi ya vijana wa Kiislamu kwenye nchi za bara la Ulaya, ambapo KWA TAARIFA YAKO wamekuwa wakitoroka kwenda kujiunga nao kwa hadaa ya ahadi mbalimbali, ambazo huzijutia baadae.
Jeshi la watoto wa ISIS ©Blessings Buzz
Swali ni je, huu ni mwanzo wa mwisho wao? Kwa habari ya kuanza kufarakana miongoni mwao, na kama ni kuongezeka kwa mabavu yao, je taifa la Israel litakuwa katika hali gani?

Hiyo ndo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.