KWA TAARIFA YAKO: MFAHAMU MWIMBAJI NYOTA WA JOYOUS ALIYEAMUA KUBADILI JINA LAKE

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu.
KWA TAARIFA YAKO hii leo tupo kukujuza kuhusu mmoja kati ya waimbaji ambao wameweza kuendelea kushikilia chati za juu katika kumsifu Mungu hata baada ya kumaliza mkataba na kundi maarufu la Joyous Celebration. Kikubwa kuhusu taarifa kutoka kwa mwimbaji huyu ni kwamba aliweza kujikusanyia mashabiki na jina lake kufahamika vyema miongoni mwa mashabiki wa kundi hilo. Lakini wakati mashabiki wakiwa wamemzoea kwa jina hilo yeye akaamua kubadili jina kabisa na kuamsha maswali kutoka kwa mashabiki na watu waliokuwa wakifuatilia huduma yake.

KWA TAARIFA YAKO namzungumzia mwanadada Tebello Sukwene mke wa mmoja wa wapigaji ngoma (drum) maarufu huko Afrika ya kusini bwana Bafana Sukwene ambaye pia ndiye aliyerekodi na Joyous toleo la 19 baada ya Sabu kupata ajali mbaya ya gari iliyopoteza maisha ya mwimbaji mwingine wa kundi hilo. KWA TAARIFA YAKO Tebello alikuwa akijulikana kwa jina la Priscilla Moeketsi ambapo alijikusanyia mashabiki kupitia wimbo kama Ngena kwenye Joyous 13 na nyimbo O Jesu Themba katika Joyous 15. Huku Joyous 16 ikiwa ndio toleo lake la mwisho kuwa na Joyous.

KWA TAARIFA YAKO baada ya maswali ya muda mrefu kutoka kwa mashabiki wakitaka kujua kisa cha mwimbaji huyo anayetamba na album yake binafsi ya He's Alive ambayo ilifikia hata kutajwa kuwania tuzo za SAMA mwaka huu nchini Afrika ya kusini lakini hata hivyo hakuweza kuchukua, ingawa kazi yake imetambulika vyema ikiwa pamoja na kufanya vizuri kwenye chati za iTune za nchini humo mara baada ya kuanza kuuzwa. Amesema jina la Tebello sio jipya ingawa alikuwa halitumii, jina hilo alipewa na bibi yake toka enzi hio ingawa hakujua kwamba alikuwa na jina hilo kutoka kabila la Tshwane la nchini humo na kwamba alipogundua ana jina hilo akaamua kulitumia na kuachana na Priscilla.


Tebello na mumewe bwana Bafana Sukwene


KWA TAARIFA YAKO mwimbaji huyo amesema mara alipoanza kutumia jina hilo alianza kujiona mpya, mwanzo mpya na kufanyika mtu mpya tena. Amesema Tebello maana yake ni mtu anayesubiri mambo makubwa kutokea. Na kwamba jina hilo linamfanya ajisikie kama mtoto aliyesubiriwa kwa hamu kuleta furaha na mafanikio katika familia yake. na kwamba analitumia jina hilo kwa kujivunia na kujiamini kwakuwa kuna watu walikuwa wakisubiri kuzaliwa kwake duniani kwa hamu. KWA TAARIFA YAKO licha ya Tebello kutoa sababu hizo lakini GK pia katika uchunguzi wake (yawezekana sio kweli lakini pia ikawa kweli) ni kwamba mwimbaji huyu aliamua kubadili jina kwasababu ya kibiashara. Kwanza kuna waimbaji mbalimbali wanatumia jina la Priscilla akiwemo mwimbaji wa kwaya ya IPCC ya Afrika ya kusini ambao nao walikuwa maarufu. Kutokana na wengi kutumia jina hilo labda alishauriwa kuachana nalo hasa ukizingatia alishaanza kujitengenezea jina nchini humo.


Unaweza kumtazama Tebello kwenye wimbo wa pili katika video hii chini Joyous 15 moja ya kazi nzuri aliyowahi kuifanya na Joyous Celebration.


KWA TAARIFA YAKO suala la kubadili majina ni la kawaida kwa waimbaji, hasa ukizingatia kwamba kuna mwimbaji mwingine mwenye jina kama lako mnaimba aina moja ya muziki, kuna uwezekano mkubwa mkawachanganya mashabiki kwahiyo njia bora ni kubadili jina. Mfano mwimbaji Sphumelele Mbambo wa Joyous jina lake halisi ni Ntokozo lakini alipojiunga Joyous alimkuta Ntokozo Mbambo wa Nqubeko akiwa ameshatengeneza jina lake kundini na kwa mashabiki, kilichofanyika akaamua kutumia Sphumelele Mbambo ili kuondoa watu kuwachanganya.

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa leo, vinginevyo tukutane wiki ijayo...


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.