KWETU PAZURI WAREKODI DVD MPYA YA 12 JUMAPILI ILIYOPITA

Ambassadors of Christ wakiwa jukwaani.

Kundi maarufu la kwaya ya Kisabato kutoka nchini Rwanda la Ambassadors of Christ siku ya jumapili lilirekodi DVD yake mpya ya 12 katika tukio lililofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Kisabato tawi la Gishushu nchini humo. Kwamujibu wa blog ya Mtangazaji maduhu inasema lengo la kurekodi toleo hilo lenye nyimbo za Kinyarwanda ni la 12 toka waimbaji hao waanze kuimba mwaka 1995, kwa lengo la kutangaza injili na kuwaunganisha wanyarwanda baada ya mauaji ya kimbali ya mwaka 1994.

Katika rekodi hiyo pia waimbaji waliowahi kuvuma na kwaya hiyo kama solo wao mwanadada Mbabazi Milly Kamugisha alikuwa mmoja wa waimbaji waliorekodi na kwaya yake hiyo baada ya kutubu kisha kurejeshwa kundini miezi kadhaa iliyopita. Bila kumsahau shemeji na wifi wa Watanzania mwanadada mwenye sauti nzuri ya kwanza aliyeolewa na Mtanzania aitwaye Claire Warren na ambaye makazi yake kwasasa yapo nchini lakini pia alijumuika na wenzake katika tukio hilo. Zifuatazo ni baadhi ya picha za tukio hilo
Mamia ya wakazi wa Rwanda wakiangalia tukio la rekodi hiyo ya wana wa 'KWETU PAZURI' ©Warren & Mutabazi

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.