MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUJUTISHA SIKU ZIJAZOFaraja Mndeme,
GK Contributor.


MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUJUTISHA SIKU ZIJAZO.


1. KUISHI MAISHA YA KUWAPENDEZA WENGINE. 
Mara kadhaa tumepoteza nafasi za kuishi katika kile kiwango chetu ambacho tunakifurahia na kutuma amani ya moyo huku tukitumia muda huo kuwafurahisha na kuwapendezesha wengine bila kujali athari zake katika siku zijazo.Kumbuka unapotumia muda mwingi kuwafurahisha na kuwapendezesha wengine unapoteza rasilimali zako muhimu sana .Moja ya rasilimali hiyo ni wakati,Wakati ni jambo ambalo likiondoka hairudi tena ,jambo jingine ni gharama mbali mbali ikiwemo matumizi makubwa ya fedha.Ni muhimu kuhakikisha unatumia nguvu kubwa kuwekeza kwa ajili yako mwenyewe maana siku zijazo unaowapendezesha wanaweza wasiwe tena sehemu ya maisha yako.Watu huja na watu huondoka ni muhimu kujenga msingi wa kujiwekezea na kujijenga katika vitu vya muhimu kwa ajili ya maisha yako yajayo kuepuka majuto. 

2. KUWAACHA WATU WENGINE WAKUAMULIE NDOTO YAKO. 
Kila mtu namna alivyoumbwa kuna kusudi limewekwa ndani mwake,namna Mungu alivyokubuni kuna vitu alijua na alitambua kwamba unaweza kuvifanya ndio maana akakuleta kwenye hii sayari.Hakuna mtu ambaye hana kusudi kwenye hii dunia.Tunapowaacha wengine watuamulie juu ya kile kilichopo ndani mwetu maana yake tunawaacha waamue lile kusudi lililomo ndani mwetu.Hakuna mtu aliyeishi nje ya kusudi akaishi kwa furaha.Kuishi nje ya ndoto ulizo nazo maana yake ni kukubali kuishi maisha yasiyo yako na matokeo yake utaishi kwa majuto na maamumivu makubwa.Ndoto zako ni muhimu sana kwa ajili ya furaha yako ya ndani,Ndoto yako ni muhimu sana kuliko maoni ya watu wengine.Maoni yao yakusaidie kukusaidia kukupa kasi zaidi kuzifika ndoto zako.Kila mtu ana ndoto yake na wewe hakikisha yako yatimia maana siku zijazo inaweza ika maneno yafwatayo “Laiti ningelijua” 

3. KUENDELEA KUISHI NA WATU WENYE MTAZAMO HASI SASA. 
Kila mtu ana chaguo la nani awe sehemu ya maisha yake na nani asiwe sehemu ya maisha yake.Aina ya watu unaokutana nao kwenye maisha mara nyingi huacha alama fulani ya tabia kwenye maisha yako.Iwapo uliishi nao kwa muda mrefu ndivyo alama hizo zitakapokuwa na athari kubwa zaidi kwenye maisha yako.Kuendelea kuishi na watu wenye mtazamo hasi ni kuendelea kujilisha sufu kwenye tabia yako ambayo kwa sasa unaweza usione ina athari lakini kwa siku zijazo athari zake zitakuwa kubwa maana akili yako haitaweza kuzalisha kilicho bora.Haiwezekani shamba upande kabichi halafu siku ya kuvuna utarajie utavuna mapera.Maisha yako ya siku zijazo yanaamukiwa na sasa yako.Watu unaoishi nao kwa sasa wana sehemu kubwa kuchangia maisha yako ya siku zijazo.Hakikisha unajitenga na watu ambao kila mara wanafikiri kushindwa kwenye kila jambo maana itakusaidi kwenye siku zijazo.Usitarajie akili inayowaza kushindwa kila mara siku moja inaweza kuzalisha ushindi.Epuka kujichimbia kaburi lako mwenyewe sasa. 

4. KUISHI MAISHA YA UCHOYO NA UMIMI. 
Hakuna mtu anayeweza kuishi bila kumtegemea mwingine.Unapojenga kuishi maisha ya umimi na uchoyo maana yake unasema kwamba ushemejitosheleza na hauhitaji msaada wa mtu mwingine.Wakati wa sasa unaweza usione umuhimu wa wengine sababu una nguvu na uweza wa kufanya majukumu mbali mbali .Umri unaposogea utagundua hawezi kufanya kila jambo wewe mwenyewe na ndipo utakapohitaji watu.Iwapo uliishi maisha ya uchoyo na umimi ndipo pale utakowahitaji watu lakini hawahusika kwenye mambo yako maana haukusuki kwa ukaribu kwenye mambo yao muhimu kwenye maisha.Ni muhimu kuhakikisha hauishi maisha ya uchoyo na umimi.Hakikisha unachiriki kwenye mambo ya watu wengine ikiwa ni akiba yako ya maisha yajao.Itakusaidia kuepuka majuto yasiyokuwa na ulazima kwa siku hizo zikifika. 

5. KUISHI KWA KUOGOPA NA KUEPUKA MABADILIKO. 
Maisha ya mwanadamu ni maisha ya mabadiliko kutoka hatua moja kwenda nyingine.Mabadiliko ni swala lisiloepukika,Kuna wakati usipo kubali kubadilika wewe mwenyewe mabadiliko yatakulazimisha ubadilike bila wewe kupenda.Wakati mabadiliko yatakapokulazimisha yenyewe ndipo athari zake zitakuwa kubwa maana mabadiliko hayo yatakuamulia mahitaji yake kinyume na wewe vile ulivyokuwa unapenda.Hakikisha wewe ndio unakuwa kiongozi wa kuongoza mabadiiko unayoyahitaji na sio yenyewe ya kuongoze maana hayafanya vile unavyopenda.Mabadiliko ni dalili ya kwamba unapiga hatua moja kwenda nyingine ,kukataa mabadiliko ni kukataa maendeleo na kukataa hatua mpya kwenye maisha yako.Ni muhimu kuhakikisha unajenga mazingira mazuri hata mabadiliko yatakapokuja yawe na tija kwenye maisha yako badala ya kuleta maamuvi yasikokuwa nataji kwenye maisha yako.Watu wengi wanaokataa mabadiliko kwenye hatua fulani ya maisha yao mara nyingi mwisho wa safari hujuta maana mabadiliko hwalazimisha kwa nguvu bila mapenzi wao wenyewe.

Hakikisha hauwi mtumwa wa mabadiliko bali kiongozi wa mabadiliko yanapotokea. 

Email : naki1419@gmail.com 
+255788454585 
God Bless You All

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.