MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUJUTISHA SIKU ZIJAZO (2)

Faraja Mndeme,
GK Contributor.MAMBO MACHACHE YANAYOWEZA KUKUJUTISHA SIKU ZIJAZO. (SEHEMU II.)

1. KUKATAA TAMAA MAMBO YANAPOKUWA MAGUMU.

Hakuna jambo lillilo rahisi kwenye maisha ,unapoamua kufanya jambo lolote tambua ugumu hauwezi kukwepeka.Ugumu wa jambo ni sehemu ya mafanikio ya jambo ambalo unalifanya.Hakuna mtu aliyefanikiwa katika jambo lolote kwa kuogopa ugumu au kukimbia ugumu.Changamoto ngumu unazokutana nazo kwenye maisha ya kila siku zinakupa hatua mpya na wakati wa kuweza kujifunza jambo jipya.Ugumu hukufundisha kufungua macho na kuongeza ufahamu kutoka pande kadha wa kadha kwenye maisha yako.Kukimbia ugumu wa changamoto ni kuamua kukimbia mafanikio yako.Kuna wakati unaweza ukakimbia ugumu kumbe ndio umekimbia kupiga hatua mpya kwenye taaluma,uchumi na mambo mebine.Ugumu wa jambo haukimbiwi bali unatafutiwa ufupumbuzi.Pindi ufumbuzi utakapopatikana basi tambua na ndio hatua mpya ya kufanikiwa kwako. 

2. KUKUZA VITU VIDOGO KUWA VIKUBWA. 

Akili ya binadamu inafanya kazi kwa namna ya ajabu sana,unapolioa tatizo au changamoto ni ndogo basi ndivyo utafanikiwa kuitatua kwa haraka zaidi na unapoona changamoto ni kubwa basin a yenyewe inakupa mzunguko mkubwa wa kutatua changamoto hiyo.Mara nyingi kwenye maisha ya mwanadamu tumekutana na vitu vya kawaida ambavyo muda mwingine vilikuwa havina sababu ya kuvifanya vionekane ni vikubwa kwa kiasi hicho.Unapojenga tabia ya kukuza mambo na vitu vidogo vidogo kuonekana na vikubwa na vigumu tambua unajiharibu mwenyewe maana itafika kipindi hata vitu vya kawaida kwako kuvitatua itakuwa ni taabu maana tayari umeshajijengea hulka hiyo ulioyo nayo leo.Ni muhimu kujenga msingi mzuri ili kesho yako isijawe na majuto yasiyo na ulazima. 

3. KUFANYA KAZI CHINI YA KIWANGO. 

Kila mtu amepewa uwezo wake wa kufanya mambo mbali mbali kwenye maisha kuna watu wana kasi kubwa kuliko wengine na wengine wana kasi ndogo kuliko wengine.Tatizo linakuja pale mtu mwenye kasi kubwa zaidi ya wengine ataka kuishi kama wale wenye kasi ndogo.Kila mtu ana ndoto zake kwenye maisha hakuna mtu anayeshindana na mwingine iwapo wewe unaona hatua na kasi yako ni ndogo na haipaswi kuwe vivyo ilivyo usisite kuiongeza.Maana haumumizi mtu mwingine bali unajiuumiza mwenyewe maana kuna wakati utahitajika kwenda kwa kasi hautaweza maana unafanya kazi chini ya kiwango.Ishi kulingana na kasi yako kwenye maisha yako ya kila siku fanya jambo kulingana na kasi ulio nayo na sio kulingana na kasi ya jirani yako.Epuka kufanya mambo mengi chini ya kiwango maana unajilewesha wewe mwenyewe binafsi.Kuna wakati usipokuwa makini unaweza kusema laiti ningelijua. 

4. KUISHI KWA MATARAJIO BILA VITENDO. 

Kinachotofautisha kati ya mtu mwingine na mwingine ni hatua moja zaidi ambayo ameamua kuichuku kwenye maisha yetu.Hakuna mtu asikuwa na taraja fulani kwenye maisha kila mtu ana taraja lake ,lakini tarajio haliwezi kutimilika kwa mataneno na mawazo tu.Tarajio linaweza kubaki kuwa wazo mfu tu iwapo halifanyia kazi kwa vitendo.Iwapo unataka kupiga hatua kwenye mambo kadha wa kadha epuka kuishi kwa matarajio tu bali hakikisha unakuwa mtendaji wa vitu kuepuka kuja kujilaumu siku moja kwamba sikufanya hiki na kile maana vote vilikuwa china ya uwezo wako wa kufanya.Epuka sana kuiharibu kesho yako kwa maamuzi yasiyo na tija leo.Wekeza muda wako vyema na hakikisha unakuwa mtendaji kwenye kila tarajio ambalo unatarajia litokee kwenye maisha yako kwenye siku zijazo za maisha yako.Kuna watu wengi makaburini waekufa nao waliishi kwa matarajio tu na wala hawakufaidi matunda ya matarajio yao kwa maana hawakua na muda wa kuwekeza matarajio yao katika vitendo. 

Email : naki1419@gmail.com 
+255788454585 
God Bless You All
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.