MSAMA PROMOTIONS YAWAKUMBUKA WATOTO YATIMA

Kampuni inayosifika kwa kuandaa matamasha ya kimataifa ya Pasaka na Krismasi nchini, Msama Promotions, imekabidhi msaaada wa vitu mbalimbali kwa vituo 10 vya kulea watoto yatima jijini Dar es salaam ikiwa ni mwendelezo wa kusaidia makundi maalumu katika jamii.


Akikabidhi misaada hiyo katika ofisi zake zilizopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, Bwana Alex Msama ambaye ni mkurugenzi wa kampuni hiyo amesema kuwa lengo la misaada hiyo ni kuwawezesha watoto yatima kusherehekea kwa furaha sikukuu ya Idd el Fitr.


 Bwa. Msama amesema misaada hiyo inathamani ya shilingi Milioni Tisa na Nusu ikiwa ni sehemu ya fedha  za Tamasha la Pasaka lililofanyika mwezi wa nne mwaka huu.


Baadhi ya vituo ambavyo vimepata misaada hiyo ni pamoja na Sifa Group Foundation kilichopo Bunju, Honorata kilichopo Temeke, Chakuwama kutoka Mwenge Umra cha Magomeni, na Mujahidina kutoka Mwananyamala.

Misaada hiyo ni pamoja na mchele, unga, sabuni, mafuta, biskuti, juisi pamoja na soda.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.