NI ZAMU YA MTAKATIFU YA DERICK NDONGE JIJINI MWANZA JUMAPILI HII

Uwanja wa mpira wa CCM Kirumba umepokea waimbaji wengi, wenyeji wa jiji la Mwanza, nje ya mkoa huo, na hata nje ya taifa la Tanzania. waimbaji wengi wa kimataifa wamepitia hapo, na sasa ni zamu ya mcheza kwao kutunzwa, hapa tunamzungumzia Derick Ndonge.


Kama uko Mwanza, basi shamrashamra umeshaanza kuzisikia, na kama uko nje ya jiji hilo, basi waweza ukawa umeshaanza kupata taarifa kupitia vyombo vya habari. GK tumenza kukuletea, na hadi ifike siku ya tukio tutakuwa tukiachia wimbo mmoja mmoja. Kwa leo tuanze na jina linalobeba album, Mtakatifu.Wimbo huu umeimbwa kwa kumshirikisha Dr Eddo wa Zoo Records, ambaye ndiye ameutengeneza huu wimbo pia. Tayari waimbaji kadhaa wameshathibisha kushiriki tukio hilo la muimbaji kutoka One Voice Family International.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.