SOMO: KIFO CHA KUTENGENEZA - ASKOFU DKT JOSEPHAT GWAJIMA

Askofu mkuu wa makanisa ya Ufufuo na Uzima Dkt Josephat Gwajima
SOMO: KIFO CHA KUTENGENEZA

Kifo ni utengano kati ya roho na mwili. “Niutengano” Kuna aina za vifo ambazo zimo ndani ya Biblia.

i. Kifo kwasababu ya makosa ya mtu.
Maana yake mtu anapokuwa dhambini anaishi lakini anakuwa ameshakufa anakuwa ana jina la kuwa hai lakini ameskwisha kufariki. Kifo sio tukio bali kifo kina masikio, kina ona na kinaweza kutumwa kwenda mahali fulani kikaenda na kurudi.

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” Yohana 3:16

Kabla hujaokoka ulikuwa umefariki na siku ulipompokea Bwana Yesu kwenye maisha yako ulikuwa hai. Mungu alimtuma mwanaye wa pekee ili sisi tukombolewe kupitia yeye.

“kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia. Luka 15:24

Mtu anapokuwa mbali na Mungu na hajamwamini Bwana Yesu mtu huyo mbele za Mungu anaitwa amekufa.

“Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. “Luka 15:32

ii. Aina ya Pili ya kifo ni kulala mauti.
Roho ya mtu na mwili wa mtu vikitengana mtu huyo anaitwa amelala mauti, maana nyingine ya kulala mauti ni “kulala katika Bwana”. Sisi tuliookolewa kile kitendo cha kwenda mbinguni hatusemi amekufa kwasababu tulishakufa kabla hatujaokoka tukafufuliwa pale tulipompokea Bwana Yesu kwahiyo tunasema amekwenda rahani pake.

“Naam, na sisi tumeonekana kuwa mashahidi wa uongo wa Mungu; kwa maana tulimshuhudia Mungu ya kuwa alimfufua Kristo, ambaye hakumfufua, ikiwa wafu hawafufuliwi. Maana kama wafu hawafufuliwi, Kristo naye hakufufuka. Na kama Kristo hakufufuka, imani yenu ni bure; mngalimo katika dhambi zenu. Na hapo wao nao waliolala katika Kristo wamepotea. Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote. Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu.” 1 Wakorintho 15:15~21

Kuna wakati unafika ambao miili hii tulionayo tutaondoka ndani yake na kubaki na miili ya mbinguni. Miili hii haitaurithi ufalme wa Mbinguni. Imeandikwa

“Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.” Wafilipi 1:21

MAUTI YA PILI
Kwa watu waliokoka hawana mauti ya pili. Siku mtu ambaye hajokoka anapokufa kimwili atapata kitu kinaitwa uchungu wa mauti ambao ni maumivu machungu kuliko vitu vyote duniani. Ndiomaana mtu ambaye hajaokoka anapokufa huangaika sana maana roho yake na mwili wake vinatengana lakini mtu aliyeokoka anapokufa hutulia na kuchukuliwa na malaika hadi mbinguni juu.

“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili. Ufunuo wa yohana 2:11

Waliookolewa na kudumu kwenye wokovu mpaka mwisho kwa kupigana vita na kuilinda imani hawata iona mauti ya pili.

“Mauti na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani, hilo ziwa la moto. Ufunuo wa Yohana 20:14

Inaitwa mauti ya pili kwasababu mtu anapokufa hapa duniani anajiungamanisha kwenye kifo ambacho ni hatari kuliko vitu vyote ambacho ni Jehanam ya moto. Yesu alikuja kuwaunganisha waliotengana na Mungu kwa msalaba. Mti wa msalaba ni kama alama ya kujumlisha na maana yake ni kwamba mti wa kuchoto na kulia unasema kwamba wanadamu waungane pamoja na mti wa juu na wa chini unamaanisha walioko chini waende juu mbinguni.

“Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” Ufunuo wa Yohana 21:8

Watu wa kwanza watakao ingia kwenye jehanam ya moto ni watu waoga wala sio wale wachawi wala waganga lakini wale waoga wamaisha, waoga wa hali, waoga wa kuzungumza, waoga wa kujitetea, waoga wa kuokoka, waoga wa kujaribu watu waoga ndio watakaoingia jehanam ya moto kwasababu Mungu hakutupa roho za uoga bali ametupa roho ya ujasiri na moyo wa kiasi.

“Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake. Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala; nao wakiisha kutoka makaburini mwao, baada ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.” Mathayo 27:50~55

Kumbe roho inaweza kutolewa na mwenye roho ndiye anayeweza kuitoa roho yake.

Kama mtu ni akili akili ni nini kwahiyo mtu sio akili, kama mtu ni elimu na elimu yake imetokana na nini kwahiyo mtu sio elimu, kama mtu ni moyo moyo unaweza kufaniywa upasuaji kwahiyo mtu sio moyo bali MTU NI ROHO YENYE NAFSI INAYOKAA NDANI YA NYUMBA NA NYUMBA INAITWA MWILI. Roho inaweza kukaa ndani ya mwili na mtu akawa ndani ya mwili, roho ya mtu inaweza kukaa nje ya mwili na mtu akawa nje ya Mwili pia

“(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;” 2 Wakorintho 10:4~8

Paulo anasema haelewi kama mtu huyu alikuwa nje ya mwili au ndani ya mwili, kwa maneno mengine mtu ni roho na ndio maana akiwa nje ya mwili ni yuleyule ni mtu na akiwa ndani ya mwili ni yeye yuleyule.

“Useme, Bwana MUNGU asema hivi; Ole wao wanawake wale, washonao hirizi katika viungo vyote vya mikono, wawekao leso juu ya vichwa vya kila kimo, ili wawinde roho za watu; je! Mtaziwinda roho za watu wangu, na kuzihifadhi hai roho zenu wenyewe? Nanyi mmeninajisi kati ya watu wangu, kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, ili kuziua roho za watu ambao haiwapasi kufa, na kuzihifadhi hai roho za watu ambao haikuwapasa kuwa hai, kwa kuwaambia uongo watu wangu wasikilizao uongo. Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.” Ezekiel 13:18~20

Roho ya mtu inaweza kutolewa na joka au jini ambalo linakuja kuingia ndani ya mtu kuitoa roho ya mtu. kwasababu roho ndiyo imtiayo mwili uzima kwahiyo roho ya mtu ikitolewa nje ya mwili, mtu huyo unaacha kufanya kazi. Mtu huyo anaitwa amekufa

“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Yohana 6:63

Kuna majini au majoka ambayo yanaingia ndani ya mwili wa mtu na kuitoa roho yake. Hospitali wanaweza kupima macho, punzi, na mzunguko wa damu kama vinafanya kazi na kama havifanyi wanasema amekufa. Sisi tumepewa uwezo wa kuwaita waliotoka ndani ya miili yao na wakarudi.
Roho ya mtu inaweza kuwindwa na kukamatwa.

“Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula.” 2 Wafalme 4:40

Kama mauti ipo ndani ya sufuria kwanini isiwepo ndani ya gari?!, kama kifo kimeingia sufuriani pia kinaweza kutumwa kwenye biashara ya mtu biashara ikafa, kumbuka kifo ni utengano na kinaweza kumtenga mtuna familia yake, kinaweza kutenganisha ndoa, kinaweza kumtenga mtu na kazi yake. kifo cha kutengeneza kinaweza kumfuata mtu kikamuingia na kumtenganisha na mwili wake au kumtenganisha na jambo lolote alilo nalo.
“Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Mauti, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa hayawani wa nchi. Ufunuo wa Yohana 6:8~10

Kifo kina uhusikika na ni kama yalivyo mapepo, majoka, mizimu, majini na miungu. Kifo kina akili kinaweza kujua kule kilikotumwa kuna hatari sana na kisiende (mtu aliyeokoka). Kifo kinaweza kumchukua mtu kikakaa naye ndiomaana siku ya mwoshi kifo kita amriwa kiwatoe wote kilichowamezwa. Kifo kinaweza kuwekwa kwenye gari. Zamani watu walikuwa wanatumia farasi kama usafiri lakini leo hii kuna magari na kifo kinaweza kuwekwa ndani yake kikawachukua watu.

“Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.” Ufunuo wa Yohana 20:13

Kifo kitanyanyuliwa na tupwa kwenye ziwa la motoni.
“Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo. Walikuwako wana saba wa mtu mmoja Skewa, Myahudi, kuhani mkuu, waliofanya hivyo. Yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?” Matendo ya mitume 19:13~15

Hawa wayahudi walikuwa ni watu wa kupandisha mapepo na kuyatuma ambapo walijaribu kutumia jina la Yesu kutoa pepo mchafu lakini walishindwa kwasababu ni wachawi. Kuna mashetani yanayoweza kuitwa na wachawi, kuna mashetani ya wanawake ambayo kazi zao ni maringo, ukahaba, kuharibu mimba, kuvunja ndoa, kusababisha utasa na mambo mengine. Kuna majini/mapepo ya uchizi, kuna mashetani maalum yanayotenda kazi kulingana na ngazi zao.

“Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12

“Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na wafalme wa Uajemi.” Daniel 10:13

Kuna majini ya aina fulani ambayo yanatumwa kwenda kumwingia mtu na kukaa ndani yake kusubiri tarehe iliyopangwa ili kutenda kazi iliyokusudiwa. Kifo kilikuwa ndani ya sufuria kinasubiri watu wale lakini kikateguliwa hii inadhihirisha kuwa watu wengi wanatembea na kifo ndani yao bila ya wao kujua. Unaweza kuona kwamba mtu anaona hatari iko mbele yake lakini anaenda bila kuiona kwasababu kifo kiko ndani yake kimempofusha asiione na kinasubiri nafasi ili kimuingie kimtenganishe na mwili wake.

Kila unayemwona hapa duniani anatumikia utawala wa juu au wa chini kwa kujua au bila ya yeye kujua.

Inawezekana rafiki yako wa kazini anakuonea wivu jinsi unavyofanikiwa akakuendea kwa mganga wa kienyeji ili ufe umuachie nafasi uliyo nayo. Akifika anapewa masharti na Yule mganga anatuma kifo kuja kwako. Kifo kinaweza kutumwa kwa mtu kulingana na mazingira aliyo nayo. Shetani akimuuwa mtu hupenda kumuuwa bila kujulikana hutengeneza mazingira ambayo watu wakiangalia watasema marehemu alifariki kwa ajali, kwa kuugua, kwa presha na watu wakiangalia wanakubaliana na hali hiyo kumbe ni kifo kimemchukua mtu huyo.

Ukiri:
“Kwa mamlaka ya jina la Yesu kila roho ya mwanadamu, mashetani, kifo, na mapepo yote na miungu yote iliyotumwa kuja kuingia ndani yangu, kwenye biashara yangu, kwenye kazi yangu ili nife au kazi yangu ife ninakinyofoa kwa jina la Yesu, ninazifunga na kuzivunja roho zote zilizotumwa kwangu kwa mamlaka ya jina la Yesu. Amen”

“Kwa Yesu ni kupigana mpaka uzeeni na kwenda mbinguni. Mtu akiokoka anakuwa mtu wa vita mpaka uzeeni mwake na kwenda mbinguni lazima uwe mtu wa vita siku zote haijalishi umeokoka shetani haogopi mtu aliye okoka bali anaogopa mtu mwenye maarifa na anayejua kuyatumia maarifa yake.”

Shetani anaweza kushindana na mtu akiwa nje yake, kupitia watu wanaomzunguka na kupitia mazingira yake. Inawezekana kazini, kwenye biashara au nyumbani. 2Wathesalonike2:10 paulo alizuiwa na shetani kwenye mazingira yake. Unapokuwa unaomba ombea na wale wanaokuzunguka, vitu vinavyo kuzunguka na mahali unapokwenda unawatiisha kwa damu ya mwanakondoo, kwa jina la Yesu.
Inawezekana hapo ulipo umekuwa kwenye tatizo la siku nyingi, umasiknii uliopita kipimo, magonjwa, matatizo na wewe unawaza ni matatizo kumbe ni roho imetumwa na mtu kukuletea matatizo. Wachawi wapo na kila familia ina watu wanaojishughulisha na ushirikina anaweza kuwa baba au mama au kaka, dada, shangazi, mjomba, binamu au mtu yeyote. mchawi wa ndani ya familia ni hatari sana kuliko mchawi wa njie ya familia kwasababu mchawi wa ndani ya familia anaijua vizuri familia kuliko wa nje, mashetani wanaomkandamiza mtu ni mizimu ya familia sababu inaijua familia kwa muda mrefu mfano:- mtoto anaweza kupewa majina ya mtu aliyefariki kwenye dhambi na akawa na ile roho yake au mzimu wake unamfuatilia na kumkandamiza asifanikiwe awe na mikosi na matatizo kwenye maisha yake.

Kuna majini yenye asili ya kiarabu yenye uwezo wa kuvaa miili ya binadamu. mashetani haya yanatawala kwenye maeneo ya mwambao wa baharini na mashetani haya hayamjui Mungu aliye hai kwasababu yametengenezwa yanatumika kwa kutumwa kuharibu ndoa, msomo, kazi, biashara na mambo mengine.

Aina nyingine ni majoka ni mashetani yaliyotoka mbinguni na ukishindana nayo unatakiwa ulifahamu neno la Mungu sababu walishawahi kuwepo mbinguni hivyo wanaijua Biblia vizuri, yanaweza kujigeuza kuwa mizimu au kitu chochote ili kushindana na watu.

Kuna miungu ambayo inaabudiwa hapa duniani nayo ni mashetani imetengenezewa kama sanamu na watu wanaiabudu kama mungu halisi lakini ni mashetani. Watu wengine wameiweka kwenye majengo na wengine wameiweka manyumbani wanaiabudu ili iwatajirishe na kuwalinda kumbe ni mapepo na mawakala wa shetani.

Mashetani mengine ni roho za binadamu ambazo ni wachawi. Japan kuna watu wanaofanya mambo ya yoga ambayo watu wanaweza kutoka nje ya miili yao na kutembea kwenda kuingia kwa watu na kuwaongoza. Roho hizo huenda kuchunguza kinachoendelea kwa wengine na kujua siri zao huku wanao chunguzwa hawajui kinachoendelea.

Unapokuwa unaomba unatakiwa unafunga kila roho inayokuja nyumbani kwako kwasababu wakati mwingine sio shetani anayekutesa ni roho kama hizi ndizo zinazo kutesa na kukusumbua, unatakiwa uzifunge na kuzifyeka kwa jina la Yesu kristo.

Ukiri:
“Kwa jina la Yesu ninaamuru leo kila mpango mbaya wa kifo uliopangwa kuja kwangu ushindwe kwa jina la Yesu”
Dawa ya mapepo na miungu hii ni jina la Yesu, unapokuwa ofisini au sehemu yako ya kazi au sehemu yeyote ile na unaona kuna hali isiyo ya kawaida unaliitia jina la Yesu, jina la Yesu haliangalii dhehebu, au dini bali mtu yeyote anaweza kuliitia jina la Yesu na akawa salama. Unatakiwa utumie mamlaka ya Jina la Yesu kuishinda roho ya kifo na mawakala wa kishetani.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.