SOMO: KUJIAMINI KUPITA KIASI NI SUMU YA MADILIKO YA KUDUMU - MCHUNGAJI MITIMINGI

Mchungaji Peter Mitimingi,mkurugenzi wa huduma ya sauti ya matumaini (VHM)

KUJIAMINI KUPITA KIASI NI SUMU YA MADILIKO YA KUDUMU.
(COUNSELING TRAINING!)

Mara nyingi watu wengi hupenda mambo mengi yabadilike na huweza kufanya lolote ilimradi tu wafikie malengo hayo. Kisha wanajisahau. Huwa wanafikiri kuwa wameshafika na kusahau kutambua kuwa wanaweza kurudi tena hatua ya nyuma walikokuwa kwa urahisi kabisa .
Ni sawa na mgonjwa wa mareria aliyepewa dozi ya dawa akaambiwa kunywa vidonge 3 sasa na baada ya wiki moja unakunywa vingine. Baada ya kunywa vile vidonge 3 na kujihisi kama amepona anasahau na kuamua kutoendelea na vile vidonge vingine 3 baada ya wiki moja mareria inarudi tena kali sana kuliko ile ya mwanzo.
Kwa wao kujiamini kupita kiasi ni adui wa mabadiliko ya kudumu.

UTAYARI NA KUJITOA (COMMITMENT).
MBINU ZA KULETA MABADILIKO YA KUDUMU


1. Mabadiliko ya kudumu yanahitaji utayari wa mtu binafsi.
2. Utayari ndicho “kiungo muhimu katika kuharakisha mabadiliko yanayodumu.
3. Utayari na kujitoa inahusu ni kwa kiasi gani mtu anataka mabadiliko.
4. Utayari huonyesha ni kwa kiasi gani mtu yupo tayari kudumisha hayo mabadiliko pale yatakapo tokea.

MALENGO YANAYOFIKIKA. (ATTAINABLE GOALS).
MBINU ZA KULETA MABADILIKO YA KUDUMU


1. Mabadiliko yakudumu yanahitaji kuweka malengo yanayoweza kutekelezeka.
2. Hakuna kinacho haribu juhudi za kutaka mabadiliko ya kudumu kama kuweka malengo yale ambayo hayawezi kufikika.
3. Mabadiliko yanahitaji malengo yenye "MASHIKO"
4. Malengo ambayo yanaweza kufikika huwa yako bayana na mahsusi kiliko ya jumla. (Attainable goals are specific rather than vague).
5. Malengo ya kudumu yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya mhusika. (part of his life)
6. Malengo huwa yanadumu muda mrefu kama mhusika anapata taarifa sahihi kuhusu maendeleo yake. Kwa mfano kufanya vipimo vya uzito katika kituo cha kupunguza uzito kila wiki, inaweza kukupa taarifa mahususi kuhusu jinsi gani uzito unapungua.

KUZUIA KURUDI NYUMA. (RELAPSE PREVENTION).
MBINU ZA KULETA MABADILIKO YA KUDUMU


1. Hili ni jambo la uhakika kabisa. Lakini kuna njia ya kupunguza jambo hili mpaka katika hali ndogo sana kumsaidia mtu kupata nafuu na kuendelea wakati anapotokea kushindwa.
2. Yule anaye shauriwa anaweza kusaidiwa kuchambua kushindwa kuliko pita na anaweza kujua ni kitu gani kilichokuwa kimekosewa mpaka kumfanya kurudi nyuma tena.
3. Na kuweza kujua ni kwa jinsi gani makosa ya namna hii yanaweza kuepukwa hapo baadae ili mshauriwa asirudi nyuma tena mara kwa mara.
4. Mshauriwa anapaswa kufahamu kuwa kurudi nyuma sio jambo geni au baya ili kuwafanya wasikate tamaa pale wanaposhindwa kufikia malengo.
5. Hakikisha pia kuwa wanafahamu vile vile kuwa njia nzuri ya kukufungua (recover) na kuendelea kurudia rudia kufanyia kazi tabia njema ambayo unaitaka haraka iwezekanavyo.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.