SOMO: MGONGANO WA FALME MBILI KATIKA NCHI MOJA - ASKOFU GWAJIMA


SOMO: MGONGANO WA FALME MBILI KATIKA NCHI MOJA
ASKOFU MKUU UFUFUO NA UZIMA - DKT JOSEPHAT GWAJIMA


Biblia Takatifu sio kitabu kinachohusu dini au historia bali ni kitabu cha agano la Mungu wa mbinguni, kitabu cha makubaliano au mkataba wa Ufalme wa mbinguni.

DINI BIBLIA INAHUSU MAMBO YAFUATAYO.
Biblia ni kuhusu Ufalme.
Biblia inahusu familia ya Ufalme.
Biblia ni habari ya serikali ya Mungu.
Biblia inahusu ukoloni wa mbinguni kuja hapa duniani
Biblia inahusu sheria na katiba ya nchi ya mbinguni.
Biblia inahusu haki za wananchi wa Ufalme.

Yesu alifundisha kuhusu Ufalme wa mbinguni kuliko vitu vingine vyo vyote.

“Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. MATHAYO 4:17~19

“Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu. Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya. Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng'ambo ya Yordani. MATHAYO 4:23~25

Yesu alizungukazunguka kaitika miji yote Kazi ya pili ya Yesu ilikuwa kufundisha katika masinagogi, kazi ya tatu aliyoifanya Yesu ilikuwa ni kuhubiri injili ya ufalme na habari safi zisizotisha yaani habari njema na kuponya udhaifu katika maisha ya watu.

“Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. MATHAYO 9:25

Tumeona Kusudi la Yesu kuja duniani lilikuwa ni kuhubiri habari njema lakini kuna watu wanawaza alikuja kusulubiwa na kuonewa ndio maana alipigwa na kutemewa mate lakini lengo halikuwa hilo bali alikuja duniani kuuleta Ufalme wa Mungu na njia ya kuuleta Ufalme ilikuwa ni kusulubiwa msalabani na ndiomaana wakati akihubiri alikuwa akifundisha kuhudu ufalme wa Mungu.

“Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. 10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.” MATHAYO 5:3

Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. MATHAYO 9:19

“Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.” MATHAYO 6:33~34

“Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa.” LUKA 4:43~44

“Mwanafunzi hampiti mwalimu wake, wala mtumwa hampiti bwana wake. Yamtosha mwanafunzi kuwa kama mwalimu wake, na mtumwa kuwa kama bwana wake. Ikiwa wamemwita mwenye nyumba Beelzebuli, je! Si zaidi wale walio wa nyumbani mwake? Basi, msiwaogope, kwa maana hakuna neno lililositirika, ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa, ambalo halitajulikana. Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba. Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika jehanum.” MATHAYO 10:24~30

“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.” WAFILIPI 3:20~21

Ufalme wa mbinguni ni nchi ya mbinguni., ukimpata raia wa mahali fulani fahamu kuna nchi ya alipotoka, ukimpata raia wa Tanzania maana yake kuna nchi ya Tanzania. Wazo la awali mwanadamu kuwekwa na Mungu hapa duniani lilikuwa ni kuujenga Ufalme wa mbinguni.

“Yesu aliposikia hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli. Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni; bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. MATHAYO 8:10~15

“Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia. Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia? Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Kama mngalinijua mimi, mngalimjua na Baba; tangu sasa mnamjua, tena mmemwona. YOHANA 14:3~10

Mbinguni ni nchi inayojitegemea na ni halisi na ina mfalme anayeitwa Yesu Kristo

“Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;” MATHAYO 5:38

Ufalme huu wa mbinguni ulikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo.
Mungu alipata wazo awe na koloni lake hapa duniani. Mungu alitengeneza dunia ili baadaye aje aweke koloni lake ambalo ili lifanye mambo yafanyike kama mbinguni, akatengeneza watoto ili waje watawale ambao ni sisi, tulikuwepo tunaishi mbinguni kabla hatujazaliwa hapa duniani kwa miili hii tuliyo nayo lakini hatukumbuki kama tulikuwepo awali. Mbinguni kuna nchi yenye jeshi na barabara na hapa duniani tunatakiwa tujenge koloni la mbinguni.

“Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?” MATHAYO 26:53

Mbinguni kuna nchi ya Ufalme iliyo na majeshi yake.

“Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. UFUNUO WA YOHANA 21:10~13

Mpango wa Mungu wa kwanza ulikuwa ni kutengeneza watoto ambao ni sisi ili tutawale hapa duniani kwa jinsi ya mwilini kwa nguvu ya Ufalme wake wa mbinguni.

Watu wengi wanapenda maisha mazuri kwasababu kwa uhalisia walikuwa wanaishi maisha mazuri yasiyo na shida hapo kabla hawajaja duniani na tunafahamu mbinguni kulikuwa na kila kitu na ndiyo asili yetu kuishi vizuri lakini hatukumbuki ilikuwa lini.

“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba. Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi. Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo. Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita. MWANZO 1:26~31

Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu roho mtakatifu walisema na tumfanye mtu kwa sura yetu na mfano wetu. Maana yake tumuumbe mtu aonekane kama Mungu anavyoonekana, atembee kama Mungu anavyo tembea, akatawale kama Mungu anavyotawala.

Wanadamu tumekuja hapa duniani kwaajili ya kufanya misheni maalumu ya Mungu aliyotuwekea ndani yetu pamoja na kuujenga ufalme wake kama mabalozi wa mbinguni. Lengo kuu la Mungu ni kutiisha, kumiliki na kutawala hapa duniani.

Mimi sina roho bali mimi ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili. Wanadamu Kila mtu ataishi milele tatizo ni wapi atakapoishi
“jehanum au mbinguni”. Ndani ya nyumba hii ya udongo unaweza kuishi kwa muda mchache tu na ukaenda sehemu unayostahili kufika.
Mungu alituleta hapa duniani ili kutuonjesha ladha ya kutawala hapa duniani hilo ndilo lililokuwa lengo la Mungu kutuleta hapa duniani na kuujenga ufalme wake. Utawala wa kwanza unaonyesha sisi tunatakiwa tutawale baharini na samaki wake, angani na nchi yote na kila kilichomo na kinachotoka ndani ya nchi lazima tukitawale na Kila chenye kutambaa juu ya nchi.

Lile neno zaeni muongezeke halimaanishi kuzaa kimwili peke yake bali kiroho pia kwa mfano tukihubiri mahali watu wakaokoka na kuijaza nchi maana yake kila mahali watu watakapotusikia na wanatakiwa waogope na kupisha njia. Mungu akawabariki na baada ya Baraka unazaa na unaongezeka na nchi inakutii.

Ukoloni ni kiu ya njia kupanua mipaka yako mpaka nchi ya mbali. Mungu alimleta Binadamu hapa duniani wa kwanza kama koloni lake na mkoloni akija mahali anafundisha mila zake ili zitumike sehemu hiyo. Mkoloni hawezi kushika mila yako bali yeye analeta ya kwake ili umfuate yeye na mila zake, lugha yake, na tabia zake. Mtu ambaye ukoloni umemkolea lazima atafanya mambo ya kikoloni hata kwa wakati usioruhusu. Mungu kwenye ufalme wa Mbinguni aliamua aanze ukoloni wake duniani ili aiambukize dunia tabia ya mbinguni kupitia sisi. Adam alikuwa mfalme lakini aliupoteza hapa duniani lakini aliupoteza.

Hakuna raha ya kuteseka na hatujaumbwa ili kuteseka bali kuna kitu kipo mahali kimesababisha hayo. Watu wengi hawaokoki kwasababu wanaowahubiria hawana fedha wana hali ngumu,lakini mtu mwenye fedha akimwambia mtu aokoke anaokoka mara moja. Uwamsho ukitokea lazima uguse serikali na maendeleo yawepo kwenye nchi yote uamsho hauanzii kanisani bali unaanzia serikalini ndipo na kanisani unastawi na kusonga mbele.

Yesu alipokuja alifahamu sisi tumeupoteza Ufalme ndiomaana alikuja duniani ili kufanya ukoloni hapa duniani sio kuomba bali kueneza ukoloni wa mbinguni.

“Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa, ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi. UFUNUO WA YOHANA 5:9~10

Kumbe yesu alipokuja hapa duniani alichinjwa akamnunulia Mungu Baba watu wa kila kabila na lugha na kutufanya kuwa Ufalme ili tumiliki juu ya nchi.

Ukiri:
“ Mimi ni Ufalme wa mbinguni,sisi ni taifa la Mungu ndani ya taifa la Tanzania. “

Yesu alipowafundisha wanafunzi wake kyomba aliwaambia mkiomba mseme Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe ufalme wako uje duniani kama ulivyo mbinguni, maana yake tunatakiwa tujue kwamba Baba yetu anakaa Mbinguni na Ufalme wake unatakiwa uje hapa duniani kama ulivyo mbinguni maana yake watu wote hapa duniani wajae tabia za mbinguni na mila ya mbinguni kama ulivyo mbinguni.

Shetani naye ni mfalme ana ufalme wake hapa duniani ambao unapigana na Ufalme wa Mungu wa mbinguni.

“Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu.” YUDA 1:6

“Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni. Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye. Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.” UFUNUO WA YOHANA 12:7~10

Kuna mashetani yalitupwa kutokea mbinguni yanaishi kuzimu na shetani ni mfalme wao kutokea kwenye shimo hilo la kuzimu.

“Baada ya hayo nikasikia sauti kama sauti ya makutano mengi, sauti kubwa mbinguni, ikisema, Haleluya; a Wokovu na utukufu na nguvu zina Bwana Mungu wetu; kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na za haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.” UFUNUO WA YOHANA 19:1~3

Shetani ni mfalme naye ni malaika wa kuzimu. Shimo la kuzimu ni dhahiri lipo kabisa. Shetani na yeye ana watu wake duniani, ana mapendekezo yake duniani.

1 YOHANA 3:10
Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.

Shetani anaishi yupo kwenye makazi yake lakini anawatu wake duniani, watu wa Mungu ni koloni la Mungu duniani na shetani naye ana watu wake duniani ambao ni koloni lake. Mbingu inataka dunia iwe koloni la mbinguni na kuzimu nayo inataka duniani pawe koloni la kuzimu. Huwezi kuwa katikati lazima uwakilishe ufalme wa mbinguni au kuzimu, kila linalotendeka na kunenwa hapa duniani linawakilisha ufalme wa juu mbinguni au chini kuzimu.

“Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.” YOHANA 4:44~45

Hakuna njia mbili au tatu hapa duniani njia pekee ya kwenda mbinguni ni Yesu kristo maana Yesu mwenyewe alisema mimi ndiye njia ya kweli na uzima. Hakuna mtu anayeweza kusema yupo katikati hachagui ufalme wowote ule mtu huyo lazima atakuwa ni koloni la kuzimu bila ya yeye kujua. Siku hizi kuna nguvu ambayo ni ya kuzimu na inasimamia maneno yanayotamkwa, umaarufu wa wanasiasa, kupendwa na watu, ushawishi kwa watu.

Hapa duniani kuna nchi mbili zinazowakilisha ufalme wa giza au nuru, watu wake wanao ongea wanaongea mambo ya nuru au ya giza na sisi kama wakoloni wa mbinguni sisi ni halali wa kuishi hapa duniani na tunawaondoa wale mabalozi wa giza waondoke kwenye eneo letu kwa jina la Yesu.

Biblia ni kitabu cha wayahudi na “Tanzania lazima ubalozi wa wayahudi urudi kasababu kutokuwepo kwa ubalozi ni laana tosha inayoifanya nchi isifanikiwe”. Utawala wa waisraeli hauji Tanzania kwasababu kuna mataifa mawili yanapigana ndani ya Taifa ambayo ni taifa la Ufalme wa mbinguni na taifa la ufalme wa kuzimu yote haya yanataka kueneza ukoloni wa kutoka kwenye ufalme wao. Ufalme wa nuru na giza unapigana ndani ya taifa na ufalme utakaoshinda ndio utaeneza Ufalme wake na sisi wa Ufalme wa nuruni tutashinda na kuwameza wote wa Ufalme wa Giza kwa jina la Yesu.

Wale wawakilishi wa kuzimu wanaijaza dunia na mitindo yao ya kuongea kwa mfano wanaitana mambo vipi mchizi wangu, na mtu anakubali kuitwa mchizi bila kuona ajabu kuitwa hivyo maana yake ni mila ya kuzimu imekuja duniani kutengeneza duniania kuwa utawala wa kuzimu. Utawala huu wa ufalme wa kuzimu ndio umeharibu mitazamo ya watu kiakili, fikra na kiroho kwa kuingizia maneno ya ajabu, tabia za ajabu na kuwapofusha fikra zao wasijielewe wao ni watu gani na wanafanya nini hapa duniani, ufalme huu muda wake umefika na nisasa unashushwa ulipotoka na kufungiwa huko ili Ufalme wa mbinguni na koloni lake lienee kwa kasi ya ajabu duniani kote mpaka kila goti na ulimi vimkiri Mfalme wa mbinguni Yesu Kristo kuwa ni Bwana na anatiisha, miliki na kutawala tawala za wanadamu. Kwenye baadhi ya nchi Utawala wa mbinguni umelegalega lakini hii ni saa ya kuusimamisha imara kama ufalme wa mbinguni na Ufalme wa Mungu kwa jina la Yesu kristo.

Maombi ni kumruhusu Mungu aingilie shughuli za kibinadamu. Tunapoomba tunatumia mamlaka kama mabalozi wa Ufalme wa mbinguni kuwaangusha watawala wenye malengu ya ufalme wa kuzimu wasiichukue nchi kwa mamlaka ya jina la Yesu, tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na n’ge na kila nguvu ya Yule adui na hakuna kitakachu tudhuru.

Tumia mamlaka uliyonayo kama balozi wa Ufalme wa mbinguni kuangusha, kubomoa, kufyeka, kuharibu kila kinachojihusisha na ufalme wa kuzimu kwa kina la Yesu na ujenge na kupanda Raisi wa Tanzania ajaye ambaye anamaagizo ya Ufalme wa mbinguni na mabalozi wake hapa duniani.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.