SOMO: UFALME NA MFALME ALIYEZUILIWASOMO: UFALME NA MFALME ALIYEZUILIWA
MCHUNGAJI MWANDAMIZI RP ADRIANO MAKAZI -Ufufuo na Uzima.

Mungu ameweka agano lake kwenye Biblia, ni vuzuri kujua kwamba Mungu tangu mwanzo agano lake lilikuwa ni kuujenga Ufalme hapa duniani.

“Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu” Mathayo25:34

Kabla mwanadamu hajaumbwa tayari Mungu alikuwa amejenga ufalme wake hapa duniani.

“Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza. Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?” Warumi 8:29

Maisha yako hayajaanza tangu ulipozaliwa bali Mungu alikuchagua tangu asili kwaajili ya jambo aliloliweka ndani yako tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

“Neno la Bwana lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.” Yeremia 1:4

Mungu alimwambia Yeremia kwamba alimjua kabla ahajamuumba tangu tumboni mwa mamayake, na kabla yajatoka tumboni alimtakasa. Mazingira aliyonayo mtu yanaweza kumwongoza jinsi ya kuamua cha kufanya lakini hayo yote yaijalishi ni mazingira yapi yanayokufanya ulivyo fahamu kwamba ulikuwepo hata kabla haujakuwepo hapa duniani na uliumbwa kabla haujaingia tumboni mwa mamayako.

Inawezekana Kuna mahali umezuiliwa huwezi kutoka na inatakiwa nguvu fulani ikukute pale ulipo ikupeleke uende mahali ulipokusudiwa kufika. Mungu aliliona hilo na akaamua kumuumba mtu kwaajili ya kuuruthi ufalme aliouweka tangu asili ili ufanyike kama nguvu kwa kuwawezesha watu wake kufikia makusudi aliyoyaweka ndani yao.

“Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” Mwanzo 1:26

Mungu alisema na tumfanye mtu kwa mfano wetu na kwa sura yetu (Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho mtakaifu) ili akatawale duniani awe mfalme. Unaweza ukajiuliza kama sote tukiwa watawala ni nani atakayetawaliwa, hilo haliwezi kuondoa lile kusudi la Mungu kwasababu yeye ndiye anayetupa namna ya kila mtu atawale eneo lake sababu ametuumba kwa mfano wake na yeye anatawala.

“Mbingu ni mbingu za Bwana, Bali nchi amewapa wanadamu.” Zaburi 115:16 “Ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.” Ufunuo 5:10
Nchi hii tumepewa tuitawale na viumbe vyake vya baharini, angani na nchi kavu.

Yesu alichinjwa kabla ya kuwepo misingi ya ulimwengu maana yake alishaandaliwa tayari kuja kutimiza hapa duniani kabla ya kuumbwa misingi ya ulimwengu, Yesu alitununua na kutufanya kuwa makuhani na wafalme juu ya nchi.

Yale matatizo unayoyapitia yasikukatishe tamaa kwasababu ulishaandaliwa tangu asili ili uje ufanye kazi ikupasayo kuifanya hapa duniani. Ulipofika utimilifu wa wakati Yesu alizaliwa na kutimiza kusudi alilokuja nalo hapa duniani. Yesu alikuwa na ndugu na watu waokuwa wanamzuia asiifanye kazi yake lakini hakuangalia hilo bali alisisimama na kulitimiza kusudi lililomleta, na wewe leo unatakiwa ulitimize kusudi ulilokuja kulitimiza tangia kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu na ukisimama utalifanya kwa jina la Yesu.

Akili yako isikuzuie kwa kile inachoisikia, mawazo yako na watu wasikuzuie kwenda unapotakiwa kufika, wewe ni mwana wa Mungu, umeumbwa kwa mfano wa Mungu, wewe ni mwali wa Moto, wewe ni raia wa mbinguni uliumbwa tangu asili, tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

Unaweza kusema watu wote wako kinyume na wewe, fahamu kwamba wewe ni mtawala na wapo watu watakaokufuata tokea mbali kama mama jusi walivyomfuata Yesu ili waje wakutengenzee njia ya kutawala.

Wazo la Mungu tangia mwanzo ni kuzaa watawala, Yesu alikuja kutuachia uwezo wa kutawala hapa duniani. Adamu alipokuja hapa duniani alipewa utawala na Mungu ili atawale, Shetani alipoona hayo yote akaamua amfuate nyoka ili aingie ndani ya mwili wake amfuate Adamu na kumdanganya auchukue ufalme wake. Shetani ni mwerevu anatumia maneno kuwadanganya watu ili awachukue waingie kwenye ufalme wake. Adamu alisahau kwamba yeye ni mfano na sura ya Mungu ambaye ni mtawala akautoa Ufalme wake kwa shetani.

Adamu alipoutoa utawala wake kwa shetani alimfanya shetani aujenge utawala wake juu ya nchi na mwanadamu akawa mtumwa kwenye nchi yake, shetani aliijenga dunia akiwa yeye kama mtawala.

Mungu alipoona hali hiyo imejitokeza akaamua kutumia njia nyingine ya kumtuma mwanaye Yesu Kristo ili aje kuutwaa ule Ufalme na kuujenga upya hapa duniani kwa kuimwaga damu yake ili imtakase mwanadamu arudi kwenye kusudi lake la awali la kutawala hapa juu ya nchi.

Mungu alimfukuza Adamu nje ya bustani ya Edeni sababu alitenda kinyume na sheria yake, tunaona kwamba ukitenda kinyume cha sheria ya Mungu Mungu anakufukuza nje ya utukufu wake.

Imeandikwa “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3: 16

Imeandikwa “Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mathayo 4:17

Imeandikwa “Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.” Mathayo3:2

Mungu aliwarudisha wanadamu kwa kuwaambia watubu kwamaana Ufalme wa Mbinguni umekaribia/umefika. Yesu alifundisha kwa habari ya ufalme na akawafundisha wanafunzi wake jinsi ya kusali wakiwa ndani ya ufalme wa Mungu.
Imeandikwa “Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.” Mathayo6:9

Tangu asili agenda ya Mungu ni kujenga Ufalme wake hapa duniani na aliwanunua watu kwa damu yake msalabani kwaajili ya kumiliki juu ya nchi kwasababu ufalme wake umeshaandaliwa tayari. Unaweza ukajiuliza mbona huoni uhalisia wa hayo yote yaliyozungumziwa, hapo ndipo mahali ndipo ulipozuiliwa na shetani usielewe maneno haya.(kufungwa ufahamu)
Imeandikwa “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.” Mwanzo 2:7

Mungu alimuumba mtu na kumpulizia pumzi ya uhai na mtu akawa nafsi hai, mwili umetoka kwenye mavumbi, udongo na roho asili yake ni mbiguni. Mungu ni roho. Mwanadamu ni roho iliyo ndani ya nyumba inaitwa mwili.

“Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.” Yohana 4:24

Mungu ni roho alitengeneza roho ili ije itawale hapa duniani ikiwa ndani ya nyumba inayoitwa mwili. Chenye maana ni roho kuliko mwili na ndiomaana imeandikwa “mpenzi naomba ufanikiwe kama vile roho yako ifanikiwavyo” maana yake mafanikio yanaanzia rohoni halafu baadaye yanakuja mwilini.

Imeandikwa “Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.” 1Wakorintho 15:45

Huyu mtu aliyetoka katika nchi(udongo) ni wa muda mfupi anaidadi ya miaka ya kuishi na baadaye atarudi kwenye udongo lakini huyu mtu wa pili ni wa milele ametoka mbinguni na anaweza kurudi mbinguni lakini kuna mambo ambayo sio ya ufalme wa mbinguni huyu mtu anaweza kuyafanya na asiingie mbinguni akajikuta anaingia kuzimu kwa shetani. Roho ni mwanadamu halisi na huyu ndiye amekwisha kuandaliwa ili awe mtawala hapa duniani, huyu ndiye aliyetakaswa kabla ya kuzaliwa, kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

Waamuzi 13:2-25

Samsoni aliungamanishwa mtu wake wa ndani na wa nje ili atimize kusudi la Mungu lilowekwa ndani yake hapa duniani, hakuvunja agano lililowekwa ndani yake ili atoe ile alisi yake ya tangu mwanzo.

Ule muunganiko uliowekwa ndani yetu kuruhusu asili zetu ziliowekwa ndani yetu ambazo zinazuia nguvu za Mungu zisidhihirike nje yetu unaitwa nafsi.

Mwadanamu ana nafsi ambayo ni kiunganishi kati ya mwili na roho, nafsi ni daraja ambalo limeshika roho na mwili linaruhusu nguvu zilizoko kwenye roho ziingie mwilini kupitia nafsini, mtu anapokufa nafsi yake inapotea na vile vyote anavyovifahamu anaviacha hapa duniani. Nafsi ya mtu inaweza kufundishika ikambadilisha mtu na kuzimu inauwezo wa kuikamata nafsi ya mtu na kuiwekea elimu ya kuzimu ili mtu ajenge ufalme wa kuzimu hapa duniani.

Imeandikwa “Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.” Zaburi 142: 7
Mtu akiwa kifungoni anapewa mavazi ya kuvaa, anapangiwa muda wa kulala, anapangiwa chakula cha kula na kuna kazi za kufanya anapangiwa azifanye, anakuwa chini ya Bwanajela ambaye ndiye mwenye mamlaka juu yake na anapangiwa chakula cha kula hatakama hakipendi.
Imeandikwa “Aliyeufanya ulimwengu ukiwa, akaipindua miji yake; Asiyewafungua wafungwa wake waende kwao?” Isaya 14:17

Ukiri:-

“Ninaomba leo bwana kwa neema yako kila kilichokaa kama mlima mrefu ndani yangu ninaomba kinitoke kwa jina la Yesu”
Imeandikwa “Yeye huizuia nafsi yake isiende shimoni, Na uhai wake usiangamie kwa upanga. Yeye ameikomboa nafsi yangu isiende shimoni, Na uhai wangu utautazama mwanga.” Ayubu 33:18,28

Mungu anaweza kuizuia nafsi isiende shimoni, nafsi inaweza kwenda shimoni ikatumika kwaajili ya kuimarisha na kujenga utawala wa shetani. Nafsi ni daraja lililo katika muunganiko wa roho na mwilini, ndani ya nafsi kuna tabia na mazoea ambayo mwanadamu ameyaruhusu yakakaa ndani na zinaweza kuwa mbaya au nzuri na kuna vitu vipo ndani ya nafsi ambavyo haviruhusu nguvu za Mungu zitoke nje ya mwili na kudhihirika. Ndani ya nafsi kuna nia, moyo, na hisia ambazo zote zinasababisha uwezo wa Mungu udhihirike nje ya mwili.

Ndani ya nia kuna fikra, kuna mawazo, kuna elimu. Ndani ya nafsi kuna utashi. Ndani ya nia kuna kuhitaji kutenda kupata fedha, kutaka kufanya maamuzi fulani. Shetani anaweza kukamata nia ya mtu na utashi na kumfanya mtu awe anafanya maamuzi ambayo hayapendi lakini anayafanya, unakuta mtu amepanga kwenda kanisani au kufunga au kufanya jambo la maana lakini anashindwa kulifanya sababu ya mawazo yanayotoka ndani yake yametokana na hisia alizoziweka kwenye nafsi yake,

Mungu ametupa zawadi ya Damu yake ambayo kwa hiyo tunavifuta vitu vyote vilivyo kinyume na Ufalme wa Mungu, itumie damu ya Yesu kufuta sumu zote ambazo zinazuia nguvu za Mungu zisitoke ndani ya Roho na kudhihirika mwilini, vile vipawa na utashi wa kufanya kusudi la Mungu utaonekana pale utakaposafisha nafsi yako kwa damu ya Yesu, kila picha mbaya uliyoiona, kumbukumbu mbaya uliyoiweka, sauti, miziki, harufu, hisia, maneno, na nia zote ulizoziweka ndani ya nafsi zifute kwa damu ya Yesu kristo wa Nazareth AMEN.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.