SOMO: UMEBEBA MIMBA AU UMEBEBA MATAIFA?

Mkurugenzi wa huduma ya sauti ya matumaini VHM, Mchungaji Peter Mitimingi
UMEBEBA MIMBA AU UMEBEBA MATAIFA?
Mambo Yaliyomtofautisha Yesu Na Wengine
1. Wanadamu wanakuona umebeba mimba, Mungu anakuona umebeba Mataifa.
Mwanzo 25:21 - 23
21 Isaka akamwomba Bwana kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye Bwana akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.
22 Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza Bwana.
23 Bwana akamwambia, Mataifa mawili yamo tumboni mwako, Na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili, Na mkubwa atamtumikia mdogo.
i. Rebeka aliona watoto wakishindana, Bwana aliona mataifa yakishindana.
ii. Wewe unaona umebeba nini? Umebeba mimba au Umebeba Mataifa?
iii. Rebeka aliona amebeba watoto, Mungu anaona umebeba Makabila.
iv. Mungu anataka uone kama anavyoona yeye.

UNAONA SAMAKI WANGAPI
Mambo Yaliyomtofautisha Yesu Na Wengine
YESU ALIONA MAELFU YA SAMAKI NA MIKATE, WENGINE WALIONA MIKATE MITANO NA SAMAKI WAWILI.

Mathayo 14:15 - 21
1. Wanadamu waliona nyika iliyojaa ukame, Yesu aliona nyika iliyojaa neema, vyakula, uponyaji wa mwili na roho.
2. Yesu alikuwa anaona mikate na samaki za kula maelfu ya watu, wanafunzi walikuwa wanaona mikate na samaki za kula mtu mmoja.
3. Yesu anataka uone kile anachokiona yeye kila akiyaangalia maisha yako.
4. Kile anachokiona Yesu juu ya maisha yako ni kikubwa sana kuliko kile unachokiona wewe katika uhalisia wake.
5. Yesu anauona muujiza wako kabla haujatungwa mimba.

YESU ALIONA MAMBO AMBAYO WENGINE HAWAKUWEZA KUONA


3. Yesu aliiona nia ya ndani ya Zakayo, wengine waliyaona maovu ya Zakayo.
Luka 19:5 - 7
5 Na Yesu, alipofika mahali pale, alitazama juu, akamwambia, Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako. 6 Akafanya haraka, akashuka, akamkaribisha kwa furaha. 7 Hata watu walipoona, walinung'unika wote, wakisema, Ameingia kukaa kwa mtu mwenye dhambi.

• Yesu huangalia huyu ni nani kesho, wanadamu huangalia huyu alikuwa nani jana.
• Macho ya Yesu huangalia kuona maisha ya kesho, bali macho ya wanadamu hunagalia kuona maisha yale ya jana.
• Macho ya Bwana yanatafuta jema ndani ya mtu, macho ya wanadamu yanatafuta maovu ndani ya mtu.

• Macho ya Yesu yalimuona Paulo wa kesho, wakati macho ya wanadamu yalimuona Sauli wa jana.

Yesu Alimuona Paulo wa kesho:
Matendo ya Mitume 9:11
Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba;
Wanadamu walimuona Sauli wa Jana
Matendo ya Mitume 9:26
Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.