TAARIFA YA AWALI: MSIBA WA MCHUNGAJI SALVATORY LEONARD

Marehemu Mchungaji Salvatory akiwa na mkewe siku ya ufunguzi wa Naioth tawi la Pugu Kinyamwezi. ©NGA
Simanzi kuu bado imetawala kanisa la Naioth kwa kile kilichojiri siku ya Jumapili, ambapo Mchungaji wa tawi la Pugu Kinyawezi, Salvatory Leonard, amefariki dunia majira ya saa moja jioni.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka makao makuu ya kanisa hilo, Mabibo External, lilipo Makuburi, Mchungaji Salvatory aliugua ghafla siku ya Jumamosi, akitapika damu na pia kutokwa na damu. NA kufikia mchana siku ya Jumapili bado alikuwa na hali mbaya akiwa amelazwa Hospitali  ya Taifa ya Muhimbili. Ilipofika majira ya saa moja jioni, historia ikabadilika, kwamba Mchungaji Salvatory hakuwapo tena duniani, ametangulia mbele ya haki.

Mazishi yatafanyika siku ya Jumanne Makuburi, kwenye kanisa la Naioth Gospel Assembly, kwa Askofu David Mwasota.

Hadi mauti inamkuta, Mchungaji Salvatory amekuwa mhasibu Naioth Gospel Assembly, na amehamia Pugu kwa kazi ya BWANA mnamo mwaka 2013, huu ukiwa ni mwaka wa tatu akiendelea kulitunza kanisa Pugu. Halikadhalika, marehemu alikuwa mtumishi wa umma, akifanya kazi taasisi ya kudhibiti na kupambana na rushwa, PCCB.

Hakika mawazo ya Mungu si kama ya wanadamu. BWANA ametoa na BWANA ametwaa, Jina lake na lihimidiwe.

Miaka ya tishini, Salvatory (mwenye tai kwenye benchi) akiwa bado kijana mdogo ndani ya Naioth Gospel Assembly
GK itaendelea kukufahamisha taarifa mpya kwa kadri ambayo itakuwa ikizipata.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.