TUMAINI SHANGILIENI WAKUMBUKWA KILELENI MWA MLIMA KILIMANJARONi watu wachache ambao hukumbuka kuonyesha upendo kwa ndugu zao, marafiki au jamaa wa karibu hasa wanapofanya jambo ambalo kwa akili zao hudhani ni lakawaida bila kujua kwamba linaweza kuleta maana kubwa sana kwa watu waliowazunguka hasa kwa watu aliowatendea jambo hilo.
Namzungumzia mmoja kati ya waimbaji nyota waliobarikiwa sauti nzuri za kumtukuza Mungu katika kwaya kongwe ya Tumaini Shangilieni ya St James Arusha, aitwaye Samuel Kusamba ambaye pia anamiliki kampuni ya utalii jijini Arusha ijulikanayo kama 'Best Northern Tours and Safari'. Bwana Kusamba ambaye ameanzisha nyimbo mbalimbali na katika kwaya hiyo, hufanya safari nyingi za kuwapandisha watalii na wazawa katika mlima Kilimanjaro.

Na katika moja ya safari zake mlimani hivi karibuni, akiwa kileleni mwa mlima Kilimanjaro aliamua kuikumbuka kwaya yake ya Tumaini kwa kuandika "For My Lovely Choir Tumaini Shangilieni'. Akimaanisha safari hiyo ameitoa maalumu kwa kwaya yake aipendayo ya Tumaini. Je wewe unaonyesha Upendo kwa watu wako wa karibu?? Hongera sana mdau wetu wa Gospel Kitaa bwana Samuel Kusamba.

Mwangalie Samuel Kusamba akiwaongoza waimbaji wa Tumaini katika album yao ya 'Unishike'


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.