UMUHIMU WA KUWA NA MSHAURI MAISHANI

Faraja Mndeme,
GK Contributor.
©Peter Casey
1. MSHAURI HUKUSAIDIA KUTORUDIA MAKOSA.
Muda mwingi tumepoteza sana kwenye maisha yetu ya kila siku kwa kuweza kurudiarudia makosa yasiokuwa na ulazima kwa sababu tu ni vile tumekosa mtu muhimu wa kutushauri. Mshauri ni mtu ambaye ana ujuzi kwenye swala husika kwa muda mrefu. Unapokaa chini yake na akakushauri na kukuelekeza  anafahamu aina ya matokeo ambayo unaweza kuyapata. Mshauri atakusaidia zaidi pia kutokurudia makosa waliyoyafanya wengine maana amekuwa na ujuzi mkubwa kwenye maisha ya kila siku. Ameona wengine wakifanikiwa na wengine wakiangamia kutokana na makosa waliyoyafanya kwenye maisha yao. Ni muhimu kujenga utamaduni kuwa na mshauri kwenye maisha yako kuokoa kurudia rudia makosa ambayo hayana ulazima, iwe kwenye biashara, kazi, ujasiriamali  na mengineyo.

2. MSHAURI  HUKUSAIDIA KUOKOA MUDA.
Namna jamii yetu ilivyolelewa mara nyingi huwa hatufundishwi namna ya kuokoa muda na kuishi kulingana na muda. Muda ni moja ya rasilimali ambazo thamani yake ni kubwa zaidi na pindi inapopotea haiwezi kurudia tena. Unapopoteza muda maana yake umekubali kuishi kwa hasara. Unapokuwa na mtu wa kukushauri atakusaidia kukuokolea muda wako  kwa kukuelekeza namna na kutokurudia makosa ambayo wengine wamefanya au wewe mwenyewe ungeyafanya na yangekuchukua muda mrefu kuyarekebisha na kuyaweka sawa. Kumbuka wakati unafanya marekebisho ya makosa hayo muda haukungoji lakini mshauri atakuambia usifanye hili na usifanye lile maana itakugharimu muda kuweza kutoka kwenye jambo husika.

3.  MSHAURI  HUKUSAIDIA KUOKOA RASILIMALI.
Muda mwigine tumetumia rasilimali zetu kwenye mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye maisha yetu kwa sababu tu hakukuwa na ulazima, na mwisho wa siku tumepata hasara ya kudumu. Unapokuwa na mtu wa kukushauri aliye makini kwenye mambo mbali mbali  anaweza kukusaidia kukuelekeza namna ya kuwekeza rasilimali zako kwa umakini. Ili kuepuka kupata hasara na kupoteza rasilimali zako.Mshauri ni mtu muhimu sana .Hakikisha Unapokuwa na mshauri kwenye swala husika ,mshauri huyo amebobea kwenye hilo eneo  unalohitaji kushauriwa.Usiende kuomba ushauri kwa muuza vitungu wakati wewe aina ya ushauri uonataka ni namna ya kuwa  Nahodha wa Meli.NI muhimu pia kuangalia aina ya ushauri unaopewa si kila mtu ana ruhusa kukushauri bali mshauri awe mjuzi husika katika eneo unalohitaji kushauriwa ili kuweza kuokoa rasilimali zako .

4. MSHAURI ATAKUSAIDIA KUOKOA NGUVU NYINGI .
Unaweza ukawekeza kwenye jambo fulani kwenye maisha yako kwa kutumia nguvu nyingi kumbe swala unalopania kuwekeza ni  batili na unaweza ukapoteza nguvu zako pasipo kuwa na ulazima.Hakuna mtu ambaye hapendi kuwekeza kwenye maisha kwa usahihi  kila mtu anapenda kufanya vivyo lakini wengine wamewekeza nguvu zao kwenye sehemu sahihi na wamefurahia faida ya nguvu na jasho lao lakini wengine wameangua kilio kisicho na ukomo sababu  ni vile wameshindwa kupata ushauri sahihi wa namna ya kuwekeza nguvu zao kwenye maisha yao.Mshauri atakusaidia kukuambia hapa uwekeze nguvu kiasi fulani au hapa usiwekeze kabisa na hapa ufanye kitu fulani na pale usifanye hivi.Hii itakuvusha kwa haraka na itakusaidia kuwekeza nguvu zako kwa tija na faida kwenye maisha yako.

5.  MSHAURI ATAKUSAIDIA KUKUONGEZEA  MAARIFA YA ZAIDA.
Tofauti kati  ya mtu mmoja na mwingine ni namna wanavyotumia kiwango cha maarifa,ufahamu na ujuzi walio nao kwenye jambo husika.Unapokuwa na mtu wa kukushauri kwenye eneo husika la maisha anakuwa amekupa faidia nyingine ya kukuongeza maarifa maana kuna vitu vipya ambavyo unaweza kujifunza kutoka kwa mtu anayekushauri,Ni muhimu kujijengea utamaduni wa kuwa na washauri kwenye maisha yetu kama watanzania .Watanzania wengi hatujajengewa na hatupendi kujiweka chini ya washauri maana tunaamini muda mwingine tuna ujuzi mkuu lakini tambua hakuna aliyeishi kwenye haya maisha kwenye hii sayari akafahamu kila jambo na kila kitu kwa urahisi.

Email : naki1419@gmail.com
+255788454585
God Bless You All
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.