CHAGUO LA GK: NAJISIKIA SALAMA YAKE BOMBY JOHNSON

Bomby na Angel
Habari ya Jumapili hii mdau wa GK, leo ikiwa ni Jumapili ya kwanza ya mwezi Agosti, tunakuchagulia wimbo wake Bomby alioimba sanjari na Angel Benard, ndani ya ukumbi wa Sundown Carnival, Kisongo jijini Arusha, wakati wa tamasha la kuwatambulisha Men of Standards.

Jukwaani Bomby alianza kuimba na kisha baadae kumuita Angel aimbe naye (asolo naye), Angel bila kutegemea wasaa huo, aliungana naye na kisha sifa na utukufu zikarejea kwake BWANA Yesu, na kila mtu akajisikia salama.


Ni maombi yetu kwamba kuanzia mwezi huu wa nane na kuendelea, ujisikie salama ndani yake Yesu, na akapate kukujibu maombi yako. Uwe na Jumapili njema yenye baraka tele.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.