CHAGUO LA GK NI KUCHAGUA MOJA NA AIC DAR ES SALAAM CHOIRKatika chaguo la GK jumapili ya leo tupo na waimbaji wakongwe waliotokea kubariki wengi miaka iliyopita kwa uimbaji wao, upangiliaji wa sare bila kusahau namna ya uchezaji wao. Hawa si wengine bali ni AIC Dar es salaam Choir, kutoka kanisa la AIC Magomeni mapipa jijini Dar es salaam. 

Kupitia album yao ya 'Watu wangu wanaangamizwa' tumekuchagulia wimbo uitwao 'Huwezi' ulioimbishwa na mwanadada mahiri katika ushambuliaji wa jukwaa awapo hudumani Mercy Nyagwaswa Mwakilasa ambaye pia amekuwa mmoja wa walimu wa kwaya hiyo kwa kipindi kirefu bila kusahau akihusika pia katika kufundisha namna ya uchezaji.

Nimatumaini yetu wimbo huu utakupatia ujumbe mahususi endapo umekuwa mtu wa kutangatanga katika njia mbili. Sikiliza na tazama ili upate burudiko ndani ya Roho bila kusahau kupata baraka kupitia waimbaji hawa ambao bado wapo ngangali katika kumtokomeza shetani na mawakala zake kupitia uimbaji wa kumsifu Mungu kwa viwango. Uwe na jumapili njema.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.