CHAGUO LA GK: SITAKUFA MOYO KUTOKA KWA JOY AMBALE


Ikiwa ni wiki moja imesalia kuelekea tukio tamasha la Sacrifice of Praise Jijini Arusha, Chaguo la GK linakuletea mwanamama kutoka Nchini Kenya ambaye nae atakuwa miongoni mwa watakaokuwa wanabubujika kwa kumtolea BWANA Yesu dhabihu za sifa ndani ya EAGT Elerai. Waimbaji wengine watakaohudumu ni pamoja na Kelvin Weiber, Paul Clement, Shangwe Voices na Hellen Kijazi na wengineo wengi.

Joy na gitaa lake ©@JoyAmbale
Kutoka Jiji la Nairobi, Bi Ambale ni mtunzi wa nyimbo, na pia muimbaji. Na hufahamika zaidi kwa nyimbo za taratibu. Leo GK inakupatia Sitakufa Moyo, kazi iliyoongozwa na J Blessings. Ni maombi yetu Mungu akuwezeshe kuvuka kila kikwazo bila kukata tamaa ya maisha.


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.