KIKOSI KAMILI CHA SACRIFICE OF PRAISE 2 ARUSHA TOUR


Jiji la Arusha ndio Jiji ambalo Sacrifice of Praise ilizaliwa. Na maono haya yakaanza kuenezwa maeneo mbalimbali. Msimu huu wa pili (2015) baada ya kuanzia Tanga, ziara ya matamasha haya itafanyika Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.

Jumapili hii Arusha the City of Praise kunawaka moto wa sifa na utukufu. Baadhi ya wahudumu watakaokuwepo ni kama vile;
Wimbo wake wa sitakufa moyo unafanya jambo kila mara unaposikika mahali. ni wimbo uliojaa utukufu ukitukumbusha ya kwamba hakika BWANA anatuona na anatuwazia mema. Hilo halina ubishi. Moja kwa moja kutoka Nairobi, Kenya. Joy atakuwepo Jumapili hii Jijini Arusha kukuhudumia.


Huyu kijana ni mdogokwa umbo tu, lakini kwa habari ya kushusha uwepo wa Roho Mtakatifu, hapo wala hakuna cha kuhoji. Moja kwa moja kutoka Dar es Salaam, yeye na Glorious Worship Team ni kitu kimoja. Ila awamu hii yupo na timu ya wana Arusha. (bofya hapa kumfahamu zaidi Paul)
kama jina lao linavyoeleza, hawa ni Men of Standards. Viwango kwao hakuna shaka vipo. Chief Pianist Jimmy Kimutuo na Holy Bass James Honore. Kazi yao sio ndogo hata kidogo. Mungu ana vifaa vyake. Watazame kkwenye video japa chini hasa kuanzia dakika ya 7 sekunde 13.Efraa Musica
Hakuna maelezo yanayoweza kuwafaa hawa vijana. Ila ukitaka kuona nguvu zinavyotumika kwa Mungu. Njoo siku hiyo. Hawa pia ni wenyeji wetu pale Elerai E.A.G.T.

Nelly Music

Nelson ni Music Director, upangiliaji wake wa kila kitu panapo jukwaani hauelezeki. Huweza kupiga gitaa, drums, na pia mic ikishikwa uwezo upo wa kutosha tu.

Abednego & The Worshipperz

Abednego ni Kijana wa makamo ambaye mawazo yake bado yako on fire. Kwa pamoja na The Worshipperz, watakuwepo kukamilisha duru zima ya kuabudu.

 

Shangwe Voices

Hakuna asiyejua Shangwe Voices (Voice of Triumph Foundation) hapa Jijini Arusha. Umoja wao ulisheheni vipaji vya Mungu chini ya Rais Elder Tolla'g Michael. Njoo tu uhudumu pampja nao. Tafadhali sana njoo.Hellen Kijazi

Wakati Mungu anagawa majukumu kwa watoto wake.  Kati ya idara ambazo Hellen alikuwepo ni hii ya uimbaji. Sauti yake ni 'crafted' kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Jumapili hii tuko naye pia. Karibu akuvuvie upako huu.

Kelvin Weiber
Huyu bwana kama umebahatika kuiona SOPA Mass Choir, basi Kelvin ni mwalimu wa sauti. Nadhani ukiita kwa kiingereza ina ladha fulani hivi, we muite Vocal Coach wa Africa Gospel Zone. Ameshahudumu maeneo mbalimbali ikiwemo Mombasa na Nairobi. Una swali kuhusu uimbaji? Njoo umuulize siku hiyo na atakujibu.

Desry

Huyu ni mbeba maono wa tukio zima, kuna maneno machache yanaweza kuongelea hapa kwa sasa. Ila fika siku hiyo umuone na umsikie. Endelea kufuatilia GK kumfahamu zaidi.


Kwa leo tuishie hapa, waimbaji ni wengi na hatuwezi kuwamaliza kwa siku moja, ila Jumapili njoo ukutane nao tuabudu kwa pamoja na kisha turudi makwetu tukiwa tumeguswa kwa upya.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.