KWA TAARIFA YAKO: MTAYARISHAJI NA MUIMBAJI ANAYEJIANDAA KUMALIZA 2015 KWA KISHINDO

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Watayarishaji wa muziki, Goodluck Gozbert na Gaston.
Jina Goodluck Gozbert linabeba taswirwa nyingi kwenye tasnia ya muziki wa injili. Kwa upande mmoja ni mtayarishaji wa muziki, kwa upande mwingine ni mwandishi na mtunzi wa nyimbo. Achilia mbali uimbaji.

Goodluck Gozbert ameanza huduma ya uimbaji mwaka 2004 akiwa mwanakwaya katika Kanisa la KKKT Usharika wa Imani Mwanza. KWA TAARIFA YAKO mwaka 2008 aliingia studio kwa mara ya kwanza na kufanya album ambayo aliipa jina la, "Nimelipiwa Deni".


Safari haikuishia hapo kwani mwaka 2012 mara baada ya kuwa amemaliza masomo yake ya kidato cha sita aliingia studio na kurekodi album aliyoipa jina la Nimeuona. Na KW TAARIFA YAKO mwaka huu 2015 mnamo mwezi wa kwanza aliachia single inayokwenda kwa jina la Acha Waambiane, kwa mfumo wa sauti na picha za sauti (audio na video), ambapo wimbo huo ulipata kibali na nafasi ya kuchezwa katika vituo vyote vya Redio na Runinga ndani na nje ya nchi.


Kwa sasa Goodluck ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Ipo Siku, ambayo imebeba jina la albam yake mpya, anayotarajia kuiachia mwezi huu, Agosti 2015.

Kwa upande wa kuwa mtayarishaji, halikuwa jambo jipya sana kwake, kwani alikuwa akifanya tokea akiwa shuleni, na hivyo alipomaliza kidato cha sita aliingia rasmi. KWA TAARIFA YAKO sababu mojawapo pia ni kutokana na vikwazo ambavyo amekuwa akikutana nazo kila alipokuwa akienda studio. Hatimaye akaamua kuanzisha Mini Sound, jina la studio yake.

©Examiner UK

Kama ambavyo watu kadha wa kadha wamekuwa na majina mbalimbali, Goodluck yeye hujita Lollipop Man, yaani kwa lugha rahisi, ni mtu anayesaidia kuvusha watu barabarani, mathalani wanafunzi na hata wale wasiojiweza (hasa kwa nchi zilizoendelea). hivyo KWA TAARIFA YAKO lengo lake hasa ni kuvusha watu kutoka hatua moja kwenda nyingine, hasa waimbaji.

Katika hatua nyingine, Goodluck, ambaye anaeleza kwamba yeye kurekodi na kuimba si tatizo kwake, na kwamba namna pekee ya kuepukana na changamoto za ujana ni kumuweka Mungu kwanza, maana kupitia yeye tunayaweza yote.

Sikiliza Ipo Siku, huku ukiimba sanjari na mashairi yake.


Mashairi ya Goodluck Gozbert, Ipo Siku

Ubeti wa 1

Ni Mbali Nimetoka tena Ni ajabu kuwa Hai Maana Ningeshakufaga
Ni mengi Nimeona tena Ya Kuvunja Moyo Labda Ningeshamwacha Mungu

Kibwagizo
Kama Ni Misongo ya Mawazo, Magonjwa Mama, Nimepitia, Ninajipa Moyo

Kiitikio
Ipo siku Yangu Tu Ipo Siku Ipo siku Yangu Tu, Nami Nibarikiwe Nami Nibarikiwe (Nibarikiwe) Aah Nibarikiwe (Nibarikiwe) Nami Nibarikiwe (Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiwe

Ubeti wa 2
Ingawa kwa sasa Wananisema vibaya Nami sishangai Najua ni ya Wanadamu Hayo Ingawa sipati Na ni Kwa Muda Mrefu Siachi Kuomba, Mungu Si Kiziwi Binadamu Wema, Ukiwa nacho, Kwa Sasa Wani epuka Sina Rafiki wa dhati Bridge

Kiitikio

Ipo siku Yangu Tu Ipo Siku Ipo siku Yangu Tu, Nami Nibarikiwe Nami Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Aah Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Nami Nibarikiwe ( Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiwe

Ubeti wa 3
Miaka Imepita Unaombaga Mtoto Hupati, Vuta Subira Maana Yeye Hachelewi, Ona Biashara Imeandamwa Mikosi Hupati, Usimwache Mungu Waganga Watakuponza,

Mpo Kwa Ndoa Ila nyumbani Amani Hakuna

Msimwache Mungu Michepuko sio Jibu

Umeugua Tumaini La Kupona Hakuna, Usimtazame Mwanadamu Siku Yako Imekaribia,

Kibwagizo cha 2
Najua Ayaya x ( Ipo Oo aaaah) Najua Ayaya x ( Ipoo Oo aaah)

Ubeti wa 4
Misuko Suko Ya Ndoa Mtoto Anakusumbua Giza Likiingia Unawaza Wapi Utalala Masimango Mashemeji Ati Huzai Mtoto Masimango Mama Wa Kambo Umemchosha Nyumbani Usiwaze Usiumie Najua yote Yatapita Nawe Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Aah Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Nawe Ubarikiwe ( Nibarikiwe) Niba, Niba, Nibarikiweee

Hiyo ni KWA TAARIFA YAKO kwa wiki hii tukiwa na Goodluck Gozbert, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.