KWA TAARIFA YAKO: NAMNA WAISLAMU WALIVYOWAJENGEA WAKRISTO MAKANISA MAREKANI

Haya msomaji wetu wa Gospel Kitaa karibu katika kipengele chetu maalumu ''KWA TAARIFA YAKO'' ambacho kinakujia kila siku za alhamisi ndani ya GK kikiwa na lengo la kukupatia habari ambayo iliwahi kutukia lakini yawezekana huijui pia yawezekana ilitukia ukawa unaijua lakini GK ikawa imesahau mahali au kuna sehemu haina usahihi utapata fursa ya kusahihisha kwa kuweka comment yako chini kabisa kwenye habari husika. Karibu

Faatimah Knight ©WBUR
Katika mambo ambayo ni nadra kutoka ulimwengu huu ni ushurika wa kufikia misikiti kujenga makanisa ama makanisa kujenga misikiti. Kwa hali kama hii ni dhahiri kwamba kama ilisemwa mwaka 1500 kwamba Yesu yu karibu kurudi. Basi sasa yu karibu zaidi. KWA TAARIFA YAKO GK imewahi kuripoti kuhusu ujenzi wa jengo la ibada la pamoja, yaani kwa Sinagogi, Msikiti na Kanisa kwa wakati mmoja. Bofya hapa kusoma.

Leo hii KWA TAARIFA YAKO tunaangazia namna ambavyo Waislamu wanajichangisha kujenga makanisa nchini Marekani.


Hivi karibuni kumekuwa na mashambulii yanayohusu ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Na jambo hilo limepelekea vifo kadhaa na hata marejuhi wengi. Mnamo tarehe 17 mwezi Juni 2015, shambulizi lilifanyika kwenye kanisa la Emanuel Methodist Episcopal lililopo Carolina Kusini na watu 9 kufariki dunia kwa kupigwa risasi. Na Matukio ya kuchoma makanisa yaliambatana na tukio hilo pia. KWA TAARIFA YAKO kufuatia hilo, binti wa Kiislamu mwenye umri wa miaka 23, Faatimah Knight alianzisha kampeni maalumu ya kukusanya fedha kwa ajili ya ujezi wa makanisa yaliyoathirika na uchomaji huo.

Jambo hilo ambalo ni la kipekee, lilianza pale ambapo Bi Knight na wenzake walikuwa na lengo la kuchangisha kiasi cha dola 500 ili kununua maua ya kwa ajili ya kuwafariji wafiwa wote, lakini mwisho wa siku ikapatikana dola 900.KWA TAARIFA YAKO tukio hilo ambalo liliendana sanjari na msimu wa sikukuu ya Ramadhani, lilivuta hisia za wengi, hasa pale ambapo mashirika kadha wa kadha yalianza kupokea mtazamo huo kwa uhai na kuamua kushirikiana naye. Baadhi ya mashirika yaliyounganisha nguvu kwenye kampeni ya Respond with Love ni Muslim Anti-Racism Collaborative, Arab-American Association of New York na Ummah Wid, huku pia watu wa imani nyingine wakiunga mkono juhudi hizo.

Japo siki za uchangiaji zilikuwa ni wiki mbili na nusu kuanzia tarehe 2 hadi 18 Julai, kilipatikana kiasi cha dola laki moja na mia nne sabini. (100,470) ambazo ni takribani zaidi ya Shilingi za Kitanzania milioni mia mbili (200,000,000). Na KWA TAARIFA YAKO michango yote hii iliambatana na hamasa ya misemo kama vile, "mahala pa ibada ni patakatifu"

©AlJazeera
Katika hatua nyingine jukumu la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakomboa Wakristo limetokana na asili yao, ambapo ni Wamarekani Weusi, kama ambavyo Faatimah Knight alivyo. Ambapo KWA TAARIFA YAKO mfululizo wa makanisa yote yaliyochomomwa yalikuwa ya watu weusi, jambo lililoonyesha kwamba linatokana na ubaguzi wa rangi, na si wa dini.Mlolongo wa matukio ya mashambulizi kwa makanisa

Juni 17: Wamarekani wenye asili ya Afrika 9 walifariki dunia kwa kufyatuliwa risasi, huku wa kumi akinusurika. Mtuhumiwa alikamatwa kwenye shambulizi hilo lililofanyila kanisa la Charleston.

Juni 22: Kanisa la Sabato la College Hill lililopo Knoxville Tennessee lilichomwa moto

Juni 23: Kanisa la Kristo la Nguvu ya Mungu (God's Power Church of Christ) lilichomwa moto Georgia.

Juni 24: Kanisa la Sabato la Briar Greek lililo Charlotte, Carolina Kaskazini lilichomwa moto

Juni 26: Kanisa la Sabato la Glover Grove lililo Warrenville, Carolina Kusini lilichomwa moto

Juni 26: Kanisa la Greater Miracle Apostolic Holiness lililopo Tallahassee, Florida pia liliungua (ikielezwa kwamba ni hitilafu ya umeme)

June 24: Kushambuliwa kwa Kanisa la Fruitland Presbyterian lililopo Gibson, Tennesse (uchunguzi ungali unaendelea)

Julai 1: Kushambuliwa kwa Kanisa a Mount Zion AME, ambalo kundi la KKK liliwahi kuliteketeza kwa moto miaka 20 iliyopita. Liliteketezwa tena kwa moto (uchunguzi bado unaendelea.)

KWA TAARIFA YAKO ijapokuwa kiasi cha pesa kilichokusanywa hakikutosha kwa makanisa yote kulinganisha na athari zilizotokea, mgawanyo wake uliendana na kadri ya uhitaji wa kanisa husika. Lakini jambo lililogusa kila mmoja duniani ni namna ambavyo Taasisi za Kiislamu zilifanya amchakato huu chini ya uongozi wa binti mwenye umri wa miaka 23 tu. Mungu atabaki kuwa Mungu.

Hiyo ndo KWA TAARIFA YAKO, vinginevyo tukutane wiki ijayo...

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.