MWALIMU MWAKASEGE AWAFUNDISHA SOMO LA VITI VYA ENZI WAKAZI WA UINGEREZA

Wakazi wa Afrika mashariki hususani Kenya na Tanzania wakaao nchini Uingereza, walipata wasaa mzuri wa kujumuika pamoja katika kusikiliza mafundisho ya neno la Mungu wakati wa kambi ya siku mbili Summer conference  iliyofanyika katika ukumbi wa Woughton Leisure centre uliopo Milton Keynes nchini Uingereza ikifundishwa na mwalimu Christopher Mwakasege.

Wakazi waliopata nafasi waliweza kubarikiwa na somo la Viti vya enzi alilofundisha mwalimu Mwakasege na kisha kufanya maombi pamoja nao mara baada ya kuhitimisha kwa kambi hiyo hapo jana. Aidha katika kambi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka kwasasa, iliongozwa na kundi la kusifu na kuabudu chini ya Bubele Kihayile na Paul Mhando ambao waliweza kuwaongoza wahudhuriaji katika kusifu na kumuabudu Mungu. Kwa mujibu wa viongozi waliowezesha mkutano huo, wakiongozwa na mchungaji Emmanuel Chatawe wamepanga summer conference ya mwakani kufanyikia nchini Scotland

Ukitaka kusoma somo zima kama lilivyofundishwa na Mwalimu Mwakasege katika semina aliyoifanya Dar es salaam BONYEZA HAPA


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.