NJOO UJIFUNZE KUONGEA NA HADHIRA NDANI YA VICTORIA JUMAPILI HII

Umekuwa na siku zenye baraka kwenye kusifu na kuabudu pamoja na GWT. Jumapili hii pia baraka ziko mlangoni kwako, amua mwenyewe kufungua ama kutofungua mlango. Awamu hii, kuna mafunzo ya kuongea mbele ya umma. Tunaita Public Speaking.

Mwalimu James Mwang'amba na Eric Shigongo watakuwepo kukamilisha jukumu hilo. Waswahili husema sherehe ni watu, bila watu haiwezi kunoga, ndio maana hata wavamizi pia wanapendezesha. Sasa kabla ya kuanza kufikiria kiingilio, tukio hili la kipekee ni bure. Kwa wale ambao ndani yao wamekuwa wanajisikia kuzungumza na hadhira ya aina yoyote ile, iwe ni kwenye mawasilisho ya kazi shuleni, kazini na hata kanisani usimamapo kuzungumza na vijana ama hata na watu wote kwa ujumla. Neno moja kwa ajili yako, tafadhali usikose Jumapili hii ndani ya ukumbi wa Victoria Service Station jijini Dar es Salaam.

Anza mwezi Agosti kipekee, tukutane kuanzia saa tisa mchana.

Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.