SOMO: FIMBO NI INJILI YA MTOTO (2)

Kelvin Kitaso,
GK Contributor.

picha ya mtandao
Wiki iliyopita tulitazama dhana nzima ya fimbo kwa ufupi, unaweza kubofya hapa kusoma kisha uendelee na sehemu hii ya pili.

Kwa nini adhabu ya viboko ni muhimu kwa mtoto.    
ü  Ni ishara ya upendo wa mzazi kwa mtoto wake kwa kuonyesha hutaki apotee, afanye makosa na kuharibikiwa. “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi, basi uwe na bidii ukatubu (Yohana 3:19).” Na Mithali 13:24 “Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanae bali yeye ampendae humrudi mapema”

  • Huleta faida kwa mtoto ya kuwa makini sana kwa vile atendavyo na umfanya kufanya vitu makini. Mithali 19:18 “Mrudi mwanao, kwa maana lipo tumaini, wala usikaze nafsi yako kwa kuangamia kwake.” 

  • Huondoa ujinga ambao umefungwa ndani ya mtoto, Mithali 22:15 “Ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto; Lakini fimbo ya adhabu itaufukuzia mbali”

  • Humpa kuijua njia ya kuiendea ambayo hataiacha hata akiwa mkubwa.

  • Humfanya kukuheshimu na kuheshimu jamii ya watu wakubwa, Mithali 29:15 “Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye”.

  • Watoto wengi wamekuwa na nidhamu ya uoga ila si heshima. Wanavyofanya mbele za watu ni kama wana heshima ila wamejaa nidhamu ya uoga.

  • Humfanya kuwa mtoto wa tabia njema ambaye uweza changia kubadilisha watoto wenzake wakawa na tabia njema pia.

  • Humfanya mtoto kuwa na hofu ya kurudia kosa kwa kuwa anajua akirudia ni lazima atapigwa tena. Ni kwa kupitia viboko mtoto aweza jua ipi ni sahihi na ipi si sahihi.

  • Huongeza umakini kwa mtoto hata kwenye hatua ya Kufanya mambo kwa umakini mkubwa (smart).

  • Humfanya mtoto akuletee sifa njema katika jamii inayokuzunguka, Mithali 29:17 “Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam atakufurahisha nafsi yako.”

  • Humuongezea kibari yeye na wewe mbele za Mungu kwa kule kurekebishika kwa tabia.

Adhabu katika wakati wa kutolewa kwake huwa ni kitu kibaya sana ila uleta matokeo mazuri kwake yeye aipokeaye. Fimbo ni jambo la umuhimu sana katika malezi bora, suala la vyombo vikubwa vya kimataifa kukataza adhabu ya viboko kwa mtoto ni kupingana na Mungu na hii ni mbinu ya shetani ya kuchafua kizazi kilichopo sasa. 
“kumbuka kuwa samaki hukunjwa akiwa mbichi na akikauka hakunjiki tena na hata kama ukimkunja wajisumbua bure tu kwa kuwa ameshakauka na kumsababishia maumivu ambayo hayawezi kumkunja na ukilazimisha waweza mvunja”


Namna ya kutoa adhabu ya viboko kwa mtoto.
Wengi wamekuwa wakikili kuwa adhabu ya viboko haifai kwa vile walivyowahi kuitumia na ikasababisha watu wakawa sugu au kwa vile walivyoona wengine wakiitumia na ikasababisha bado kuharibikiwa kwa watoto kwa kuwa watoto wengine uwa sugu pasipo kujali adhabu hiyo itolewapo kwao.
Si kila kiboko kinaweza kuleta matokeo mema niliyoyataja hapo juu, ila ni kiboko kitolewacho kwa njia sahihi, kwa wakati sahihi na juu ya jambo sahihi. Namna njema ya kutoa adhabu kwa mtoto ni kwa mzazi kurejea kwenye zile nafasi za yeye kama mzazi kwa kuangalia anapaswa kufanya nini kama kiongzi, mwalimu na rafiki, nakadharika.
Kama kiongozi, mzazi hutoa adhabu na huku akimsaidia mtoto kuijua njia na kutembea katika njia, na kama mkufunzi anapaswa kumchapa mtoto huku hakimfanya kujua ni kwa sababu gani anamchapa na kumfundisha ili kwa siku nyingine asijerudia tena, na kama rafiki huweza kuifanya kazi yake kwa kuwa karibu naye ili aweze kufahamu mengi, ila ni vyema kuzingatia kuwa hii nafasi ya urafiki haifanyi kazi sana katika wakati huu wa adhabu.

Ukali, adhabu ya viboko na makelele  havitoshi kumfunza mtoto katika njia impasayo
Ni ukweli kabisa kuwa wapo wazazi wengi sana ambao wametumia muda wao mwingi kupiga makelele kwa watoto wao kuhusu tabia mbaya na wengine wamekuwa wakali sana na huogopwa kila wakati wafikapo mbele za watoto wao, na utumia fimbo kila wakoseapo watoto wao, ila kwa jitihada zote hizo bado juhudi zao zinagonga mwamba kwa kutokuwa na matunda mazuri ya kuwakuza watoto hao, hii ni kwa sababu ukali, fimbo na makelele mengi havitoshi kumfanya mtoto abadilike, ila kutumia fimbo pamoja na kumfunza neno la Mungu na likakaa vizuri ndani umfanya mtoto kuwa na hofu ya Mungu ambayo itamzuia kujishughulisha katika uovu ajishughulishao.
Ni neno la Mungu ndilo lina nguvu ya kumkuza mtoto likiambatanishwa na fimbo pale makosa yanapotokea ila likikaa vizuri ndani litamfanya mtoto kujua ni yapi yaliyo makusudi ya Mungu. 

Katika mfululizo wa somo la namna ya kumlea mtoto katika njia ipasayo (soma hapa) wiki ijayo tutatazamia malezi ya Yesu na malezi ya Samweli.
_____
Mwalimu Kelvin Kitaso anapatikana kupitia 0767190019 / 0713804078 na pia kupitia barua pepe; kitasokelvin@gmail.com


Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.