SOMO: KUJENGA KATIKATI YA UPINZANI - ASKOFU GWAJIMA

Askofu Mkuu, Dr Josephat Gwajima
“katika mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Danielii, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la Bwana lilimjia Yeremia nabii, ya kuutimiza ukiwa wa Yerusalemu, yaani, miaka sabini.” Danie 9:2 - 27

Waana wa Israeli walipotoka katika nchi ya Misri Mungu aliwapa Sheria ambazo kwa hizo wakizishika watafaninikiwa na wasipozishika ataruhusu mfalme wa Babeli nebkadneza kuwachukua na kuwapeleka babeli kwa muda wa miaka sabuni wale chakula cha taabu kwa muda wa maka sabini na kulala kwa shida kwa muda wa miaka sabini, Danieli aligundua kwa kusoma vitabu miaka imetimia.

“Basi adui za Yuda na Benyamini, waliposikia ya kuwa wana wa uhamisho wanamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, hekalu, wakamkaribia Zerubabeli, na wakuu wa mbari za mababa, wakawaambia, Na tujenge sisi nasi pamoja nanyi; kwa maana tunamtafuta Mungu wenu kama ninyi, nasi twamtolea dhabihu tangu zamani za Esar-hadoni, mfalme wa Ashuru, aliyetupandisha mpaka hapa. Lakini Zerubabeli, na Yoshua, na wakuu wengine wa mbari za mababa katika Israeli, wakawaambia, Ninyi haiwahusu kushirikiana nasi katika kumjengea Mungu wetu nyumba; bali sisi wenyewe peke yetu tutamjengea Bwana, Mungu wa Israeli, nyumba, kama mfalme Koreshi, mfalme wa Uajemi, alivyotuamuru. Ndipo watu wa nchi wakaidhoofisha mikono ya watu wa Yuda, wakawasumbua, walipokuwa wakijenga. Wakawaajiri washauri juu yao, ili kuwapinga kusudi lao, siku zote za Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata wakati wa kutawala kwake Dario, mfalme wa Uajemi. Tena, wakati wa kutawala kwake Ahasuero, mwanzo wa kutawala kwake, watu wakaandika mashitaka juu ya wenyeji wa Yuda na Yerusalemu.” Ezra 4:1-24

Utawala wa uajemi ulikuwa na nguvu mwaka wa mia sita na sita kabla ya kuzaliwa kristo, ulikuwa na nguvu kama Marekani ilivyo leo. Mfalme mpaka koreshi akafariki na akatokea mwingine tena akafa na alipotokea mfalme wa tatu akasema roho yake imeamua iwaache waende nyumbani kwao wakamjengee Bwana wao nyumba, tunajifunza kumbe yule wa kukuumiza muda wake ukifika ule uwezo wake wa kukushikilia unakwisha na kuamua akuruhusu uende zako.

Mfalme koreshi aliamua kuandika barua kwamba wana wa Israeli waende nyumbani kwao, na walipofika maadui wakaamua wajichanganye nao ndani ili wajenge pamoja, adui anatabia ya kujipenyeza ili naye aonekane anajenga pamoja na wewe kumbe anabomoa, Joshua alipoona hayo aliwajibu haiwahusu na wakaamua wajenge wenyewe.

Mfalme Koresh alipowaruhusu wana wa Israeli warudi wakamjengee Mungu wao hawakwenda muda ule ule bali ilipita miaka mpaka mingi mpaka Mfalme aliyewaruhusu akafariki na akaja mwingine, sio kwavile Mungu amekwisha kusema jambo fulani inakuwa muda huo huo bali hupita muda fulani ndipo jambo lile litokee kwa kumtumia mtu, Mungu alipotaka kumwangusha haman alimtumia Esta, Mungu alipotaka kugawa bahari ya shamu alimtumia Musa, Mungu alipotaka kuwakomboa watu alimtumia Yesu, Mungu anatafuta mtu wa kurusha makombora mahali panapotakiwa kurushwa, kwenye kila kizazi Mungu hutumia watu kuwavusha watu waende kwenye ahadi zao. Kwenye kizazi hiki Mungu anakutumia wewe uipeleke nchi ya Tanzania ivuke mpaka mahali inapotakiwai kufika. Ukinyamaza hakuna kitakachofanyika lazima uamke uipeleke nchi mahali inapotakiwa kufika kama balozi wa Ufalme wa mbinguni duniani.

Mungu huinua watu wakuvushe pale shetani anapokuvunja moyo ili usiendelee mbele.

Ukiri:
“Ninaamuru kwenye ulimwengu wa roho tukio litokee la kukutia moyo uende kwenye mafanikio yako kwa jina la Yesu.”

Wana wa Israeli walipovunjwa moyo mikono yao ilidhohofika wakashindwa kuendelea kumjengea Mungu nyumba, njia moja ya adui anaweza kuitumia ni kulegeza mikono yako ili usiendelee mbele.

Silaha tatu zimetumika ili kuzuia kusudi la Mungu lisifanywe na wana wa Israeli, ya kwanza imetumika kuomba kujiunga nao ikashindikana, ya pili ni ile ya kuvunjwa moyo mpaka mikono yao ikalegea, walivunjwa moyo miaka miwili na hawakulifanya kusudi la Mungu lakini baadaye wakatokea watu wawili hagai na zekaria ambao wao walikuwa si wajenzi waliwakuta watu wamekata tamaa wakaanza kuwachochea kwa kuwaambia inukeni mumjengee Bwana anasema adui zenu wamewekwa chini yenu, Bwana amesema adui zenu wamejikwaa na kuanguka ndipo walipoamka na kuendelea kujenga, silaha nyingine ni ile ya kwenda kuwashitakia kwa mfalme ili awaondolee kibali wasinjenge nayo haikufanikiwa bali mfalme aliwalinda mpaka wakamaliza ujenzi. Tunatakiwa tuamke tuijenge Tanzania liwe taifa jipya la kustawi, wabunge wake waamke waijenge nchi tena bado tunaweza kulijenga Taifa letu tena likastawi bila kujali maadui wanatumia mbinu gani kutuvunja mioyo kwa jina la Yesu. na ilo roho yako iamke sababu inawezekana unaweza kusimaa tena na kujenga.

“Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli. Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.” Ezra 5:1-

Unabii maana yake ni Mungu anazungumza kutumia kinywa cha mwanadamu, unabii ni Mungu anatoa maelekezo kupitia kinywa cha wanadamu. Maadui wa Israeli walipoona Israeli wameanza kujenga wakawa wanawashambulia na wana wa Israeli kwa kuwapiga ili wasijenge lakini waisraeli waliamua kujenga kwa mkono mmoja na mkono mwingine wakitumia silaha kupigana na adui, kumbe hata katikati ya matatizo unaweza kuendelea kujenga yako huku ukipigana ya adui. Kama mtu akiwa hana kazi akija kukusemesha na wewe ukaacha kazi ukamsikiliza ujue wewe ndiye unayepoteza maana yeye hana kazi hana cha kupoteza, Unatakiwa ubaki kwenye kazi yako huku mkono mmoja ukibeba silaha na mwingine endelea kufanya kazi kama askari wa Bwana Yesu kristo.

Kwenye mojawapo ya kanuni ya kivita inasema “Wakikushinda wanunue, na wakikushinda ungana nao”

Tunaona maadui hawa wa Israeli walipoona njia zote zimeshindikana wakaamua kumwita Joshua afanye maongezi juu ya ujenzi wao lakini Joshua alikataa kuacha ujenzi na kuwafuata na kuwasikiliza, walipoona amekataa waliamua kumwandikia mfalme barua kwamba kuna watu wameanza kujenga nyumba kwa bidii sana ambayo ilibomolewa miaka mingi iliyopita. Tunajifunza adui ukisha mshinda sikuzote hujaribu kukushawishi ili uache kazi yako na kumsikiliza anachokitaka lakini unatakiwa ubaki ndani ya kazi yako na akisogea fyeka na endelea na kazi yako kwa jina na Yesu.

Maadui walitumia kila njia kukwamisha ujenzi huu lakini walishindwa kwasababu Mungu akiamua kufanya jambo lazima litafanyika na kutimia.

Mtu ambaye anaongea sana na kutisha sana kwamba ataweza ataweza ujue mtu huyo hawezi anaogopa bali mtu akiwa amekaa kimya huyu ni wa kumwogopa sana, Imani ya kikristo imeanzia msalabani na leo imejaa duniani kote Ukristo duniani hautavunjwa na mtu yeyote tena kwa jina la Yesu na tunayaweza mambo yote katika yeye apaye nguvu. Mambo ya Mungu huwa yana upinzani sana lakini mwisho wake huwa yanaushindi wa kishindo kikuu, ni ushahidi tosha mtu kama yupo safi kila idara hana changamoto zozote zile yeye kile itu kwake kimefanikiwa basi yupo upande wa shetani. Kila tatizo unalolipata ni nafasi ya Mungu ili umtukuze baadaye.

Ukiri
“Dhiki yangu ni nyepesi na ya muda mfupi lakini inanitengenezea utukufu baadaye”

“Ndipo mfalme Dario akatoa amri, na watu wakatafuta katika nyumba ya vyuo vya tarehe, hapo akiba zilipowekwa katika Babeli. Na chuo kimoja kilipatikana huko Akmetha, katika nyumba ya mfalme iliyo katika wilaya ya Umedi, na ndani yake maneno haya yameandikwa ili yakumbukwe. Katika mwaka wa kwanza wa mfalme Koreshi, mfalme Koreshi alitoa amri, Kwa habari ya nyumba ya Mungu huko Yerusalemu, nyumba hiyo na ijengwe, mahali watoapo dhabihu, na misingi yake ipigwe na kufanywa imara sana; kuinuka kwake kuwe mikono sitini, na upana wake mikono sitini; ziwepo safu tatu za mawe makubwa, na safu moja ya miti mipya; gharama zake zitolewe katika nyumba ya mfalme. Na vyombo vya dhahabu na fedha, vya nyumba ya Mungu, ambavyo mfalme Nebukadreza alivitoa katika nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu, akavileta mpaka Babeli, na virudishwe, vikaingizwe tena katika hekalu lililoko Yerusalemu, kila kimoja mahali pake, na wewe uvitie katika nyumba ya Mungu. Basi sasa ninyi, Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na hao wenzi wenu wa Kiajemi, mlio ng'ambo ya Mto, jitengeni na mahali pale; iacheni kazi hii ya nyumba ya Mungu, msiizuie; waacheni liwali wa Wayahudi, na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi, kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng'ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Na kila kitu wanachokihitaji, katika ng'ombe wachanga, na kondoo waume, na wana-kondoo, kwa sadaka za kuteketezwa watakazomtolea Mungu wa mbinguni, na ngano, na chumvi, na divai, na mafuta, kama makuhani walioko Yerusalemu watakavyosema, na wapewe vitu hivyo vyote siku kwa siku, msikose kuwapa; wapate kumtolea Mungu wa mbinguni sadaka zenye harufu nzuri, na kumwombea mfalme, na wanawe, wapate uzima. Pia nimetoa amri kwamba, mtu awaye yote atakayelibadili neno hili, boriti na itolewe katika nyumba yake, akainuliwe na kutungikwa juu yake; tena nyumba yake ikafanywe jaa kwa ajili ya neno hili. Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakaonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. Ndipo Tatenai, liwali wa ng'ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakafanya hayo kwa bidii, kwa sababu mfalme Dario alikuwa ametuma watu kwao. Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa msaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido. Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi. Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario. Na wana wa Israeli, na makuhani na Walawi, na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu kwa furaha.” Ezra 6: 1 - 16

Amri ikitolewa na Mungu hata kama shetani atoke shimoni kuipinga lazima jambo lililokusudiwa litimie. Majira hayawafuati watu bali watu wanayafuata majira, usishindane na majira ukishindana nayo majira yatakuuwa. Kwenye ulimwengu wa rohoni kuna sauti inasema hii ni saa ya Ufufuo na Uzima Duniani hii ni saa ya Bwana.

Ufunuo12:7
Shetani jina lingine anaitwa nyoka wa zamani,
Yohana 11,
Shetani ni Mungu wa ulimwengu huu na hana uwezo wa kukunyanganya kile ulicho nacho bali anauwezo wa kukucheleweshea muda tu kisitimie amka upigane ulitimize kusudi lilowekwa ndani yako kwa jina la Yesu.

Mahubiri yeyote kama hayajagusa kwenye maisha ya mtu basi hayana maana lakiniYesu alipokuja duniani hakuja kuleta dini, ndio maana alikuwa anaongea na watu, anaponya watu na kuongea lugha za watu. Kila tatizo lina chanzo chake na ukitaka kuleta ufumbuzi unateketeza chanzo cha tatizo hilo kwanza ndipo tatizo linaondoka. Lazima ujue chanzo ili uondoe matatizo uliyoyano kwa jina la Yesu.

Amen
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.