SOMO: NGUVU YA KUSHUKURU KWENYE MAFANIKIO YA MWANADAMUFaraja Mndeme,
GK Contributor.

Kushukuru kwenye mambo mengi kwenye maisha yetu ya kila siku ni moja ya njia muhimu sana ya kuweza kutufikisha kule tunapotamani kufika. Huwezi kufanikiwa katika kiwango unachohitaji kwenye maisha yako binafsi bila kuwa na tabia ya kujifunza tabia ya kushukuru. Kushukuru ni tabia ambayo kila mmoja wetu anaweza kujifunza. Kuna faida nyingi sana zinazoambatana na kushukuru kwenye maisha yetu ya kila siku. Mafanikio hayo unaweza usiyaone moja kwa moja katika picha kubwa ya tafsiri yako ya kufanikiwa, lakini kwa sehemu moja au nyingine huwezi kutenganisha kufanikiwa kwako dhidi ya kiwango chako cha shukurani.

Mafaniko Machache Yanayoambatana na Kushukuru. 

I. KUSHUKURU HUVUTA KILE UNACHOHITAJI KWA HARAKA ZAIDI. 

Fikiria kwenye maisha yako unahitaji kupata kitu kutoka kwa mtu mwingine halafu baada ya mtu yule kukusaidia unaondoka tu bila kumshukuru. Je unafikiri kwa wakati mwingine yule mtu uliyeondoka kwake atafanyaje? Kuwa na shukrani kwenye maisha yetu ya kila siku hujenga tabia ya kubata kibali kwenye maeneo mbali mbali tunakutana na watu. Unaposhukuru unapata nafasi na kufungua mlango mwingine kwa mtu husika na unaweza ukapata nafasi zaidi kwa watu wengine. Shukurani ni zaidi ya kusema ahsante. Maisha yako kwa ujumla na namna unavyofanya vitu inaweza kutujilisha iwapo kwamba una shukrani au unaigiza kuwa na shukurani. Ujenzi wa tabia ya kushukuru kutakufungulia milango isiyokuwa na Mipaka. Shukurani inaweza kukupa kibali hata mahali ambapo ungefikiri usingeingia. Ni Muhimu sana kujifunza tabia ya kushukuru kwenye maisha yetu ya kila siku. 

II. KUSHUKURU HUDUMISHA MAHUSIANO

Moja ya tatizo kubwa la mahusiano mengi kufa ni kukosekana kwa tabia ya kushukuru. Kuwa na tabia ya kushukuru ni ishara ya kwamba unathamini kile ulichotendewa na upande wa pili. Unapopuuzia kushukuru maana yake haukufurahishwa na kile ulichotendewa na upande mwingine. Ni muhimu sana kujenga tabia ya kushukuru na kuifanya iwe sehemu ya maisha yetu. Fikiria iwapo umempatia mtu zawadi nzuri halafu mtu yule anaichukua halafu aanze kulalamika kwa kuisema vibaya zawadi uliyompatia, je unafikiri ni kitu gani kinaweza kutokea? Shukurani hutunza mahusiano yoyote yale na kuyafanya yastawi zaidi kutoka hatua moja kwenda nyingine. Huwezi kutofautisha namna ya kufanikiwa kwa mtu kwenye mahusiano mbalimbali na kiwango cha shukurani alicho nacho kwenye maisha yake kwa ujumla. 

III. SHUKURANI HUFUKUZA MBALI TABIA HASI. 

Mara nyingi tumekutana na watu wanaopenda kulalamika na kunung’unika mara kwa mara. Ukifuatilia maisha ya watu hawa mara nyingi hawana furaha maana maisha yao yanakuwa yamefunikwa na nguvu hasi wa sababu ya malalamiko ya mara kwa mara. Nguvu hasi hupelekea kufunga fahamu zao na kutokuona faida zinazopatikana mbele zaidi kwenye neno Shukurani. Shukurani katika kila jambo huweza kukufungulia milango zaidi na zaidi kutoka hatua moja kwenda nyingine. Unapotaka kufukuza tabia kandamizi zinazokufanya usiwe na furaha mara kwa mara, jifunze tu kushukuru katika kila jambo unaloliona kwenye maisha yako ya kila siku. Usipojifunza kushukuru kwako kila jambo litakuwa baya na litakuwa halina thamani kwa sababu maisha yako yamejengwa kwenye msingi wa malalamiko na manung’uniko na sio shukurani katika kie ulicho nacho. Huwezi kutenganisha maisha ya furaha ya mtu aliyonayo na kiwango cha shukurani alicho nacho kwenye maeneo mbali mbali yanayomzunguka. 

IV. SHUKURANI HUKUTUSAIDIA KUJIFUNZA ZAIDI. 

Kuna namna mbalimbali za kujifunza kwenye maisha. Hakuna mtu anayezaliwa huku anafahamu yote, bali wote tunahitaji kujifunza kutoka kwa wengine. Unapojenga tabia ya kushukuru inakufungulia mwanya wa kuweza kupata na nafasi ya kujifunza kutoka kwa wengine kutoka katika yale wanayoyafamu maishani mwao. Huwezi kuingia kwenye moyo wa mtu kirahisi na kupata kibali cha kujifunza kutoka kwake iwapo haukujenga tabia ya kushukuru. Shukurani hukusaidia kuweza kupata nafasi ya kujifunza kutoka kwa mwingine. Usipokuwa mtu wa shukurani unaweza kutumia gharama kubwa sana kuweza kujifunza kutoka kwa wengine kwa sababu tu hauna tabia ya kupenda kushukuru. Ni muhimu sana kujifunza kushukuru kwenye kila jambo muhimu kwenye maisha yako ya kila siku. Unapotaka kujifunza kwa kiwango kikubwa na uende mbali zaidi, njia moja wapo ni tabia ya kushukuru.

Email : naki1419@gmail.com 
+255788454585 
God Bless You All

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.