SOMO: UNABARIKIWA KWANZA NDIPO KAZI BIASHARA NDOA ZINAZAA MATUNDANa King Sam

UNABARIKIWA KWANZA NDIPO KAZI BIASHARA NDOA ZINAZAA MATUNDA
Mwanzo Genesis 1:22
-Mungu akavibarikia, akisema, Zaeni, mkaongezeke, mkayajaze maji ya baharini, ndege na wazidi katika nchi.
Mungu alibariki kwanza ndipo (AKASEMA) zaeni,

Kitu unachotakiwa kutafuta ni kubarikiwa kwanza ndipo vile unavyotaka kufanya vitazaa matunda,Kama haujabarikiwa kile utakachofanya hakiwezi kuzaa matunda,ndiyo maana unaona watu wengi wanamatatizo katika kazi biashara au katika ndoa kwa sababu hawajabarikiwa,utaombeaje mtu kazi yake ifanikiwe wakati haujabarikiwa?

Chochote unachofanya Mtu ukibarikiwa kinazaa
Neno Baraka watu wanalitafuta nje ya Mungu,Mungu peke yake ndiyo anayebariki kwa Neno lake na ukishapokea baraka ndipo vile unavyovifanya vinakuwa na matokeo
Haijalishi ni nini unafanya Kama MUNGU amekubariki utakuwa na matoke makubwa hata Kama unauza mboga biblia inasema hivi....
Zaburi Psalms 1:3
Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa.

Angalia Yusufu Mungu alivyokuwa naye kwa sababu alikuwa Mtu alibarikiwa hata wangemfunga angefanikiwa tu,
Uwezi kuzaa na kuongezeka Kama haujabarikiwa, Mwanzo Genesis 39:2
BWANA akawa pamoja na Yusufu, naye akasitawi; naye alikuwa katika nyumba ya bwana wake, yule Mmisri.

Abraham alibarikiwa kwanza,alifanyika Baraka kwanza,ndiyo maana Leo Mimi na wewe tumeunganishwa kwenye Baraka kupitia yeye,na ndipo Abraham kila alichofanya kilizaa matunda alipobarikiwa ndipo tumboni la Sarah lililokuwa limekoma likafunguka,tena hata Kama walisema familia yenu haiwezi kufanikiwa au kusema au kujenga Nyumba au kuja na Biashara nk Kama Mungu amekubariki akaweka mkono wake juu yako basi walivyoona kila kitu kitabadilika,

Watu wanachagua kazi wanafikiri kazi ndiyo Baraka wewe ndiye baraka Kama haujabarikiwa chochote ufanyacho akitakuwa na matunda,utachagua sana,
Ndiyo maana unaweza kuwa unalipwa milioni kumi na hauna matoke ya hizo pesa lakini kuna Mtu analipwa laki tano ni Kama vile analipwa milioni ishirini,Kwa nini kwa sababu ukisha barikiwa kile kidogo ulichonacho kinakuwa kingi mikononi mwako

Angalia biblia inavyosema mdogo atakavyokuwa akishabarikiwa na Mungu ....
Isaya Isaiah 60:19
Jua halitakuwa nuru yako tena wakati wa mchana, Wala mwezi hautakupa nuru kwa mwangaza wake; Bali BWANA atakuwa nuru ya milele kwako, Na Mungu wako atakuwa utukufu wako.
20 Jua lako halitashuka tena, Wala mwezi wako hautajitenga; Kwa kuwa BWANA mwenyewe atakuwa nuru yako ya milele; Na siku za kuomboleza kwako zitakoma.
21 Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
22 Mdogo atakuwa elfu, Na mnyonge atakuwa taifa hodari; Mimi, BWANA, nitayahimiza hayo wakati wake.

Wewe unaitaji kutafuta Baraka za Mungu juu ya maisha yako na Baraka si kukimbilia kuombewa ndipo unabarikiwa hapana biblia inasema hivi..
Kumbukumbu la torati 11: Deuteronomy 11:26
Angalieni, nawawekea mbele yenu hivi leo BARAKA na LAANA;
27 BARAKA ni hapo mtakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, niwaagizayo leo;
28 na LAANA ni hapo msiposikiza maagizo ya BWANA, Mungu wenu, mkikengeuka katika njia niwaagizayo leo, kwa kuandama miungu mingine msiyoijua.

BARAKA chanzo chake ni wewe kulishika Neno la Mungu na kulifanyia kazi unataka kazi yako Biashara yako unataka Ndoa yako zifanikiwa wakati haulishiki Neno la Mungu uko kinyume unatafuta maombi wakati haulitii Neno la Mungu,usipo badilika katika jina la Yesu huwezi kufanikisha mambo yako badilika katika jina la Yesu,

Yesu ni Neno la Mungu shika Neno la Mungu ili ufanyike baraka katika jina la Yesu amen

King Sam
Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067
Namba ya whatsapp hii +447977225185
Ubarikiwe na Yesu
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.