SOMO: UPENDO WA YESU - KING SAMUPENDO WA YESU..
Ayubu 5:26
Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.
Si mpango wa Mungu ufe na ugonjwa wala ufe kwa ajali wala ufu kwa njia yeyote ile ya mate so,Kama baadhi ya watumishi Kila kifo wanasema ni mapenzi ya Mungu hakuna kitu Kama icho wewe mwenyewe utataka kunibishia lakini Leo nataka kuonyesha Upendo wa Mungu na Kama ukijuwa alikupangia mambo mazuri hata kurudi kwako kwake usife kienyeji kwa mateso,

Leo hii nataka ujuwe tu vifo vya magonjwa ajali sumu kuuliwa nk ni kazi ya shetani,vitu vitatu vinavyosababisha kufa kwa Mtu Kama hakuaga akafa labda kwa magonjwa au kauliwa au kajiua nk ni
-shetani
-dhambi
-kutokutii
Tuanze kuona shetani alivyofanya pale Eden shetani ndiye alikuja kwanza kusababisha pili Mwanadamu akakataa Kutii Neno la Mungu tatu dhambi ikachukua nafasi ndipo kifo kikapatika,
Yakobo 1:13
Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu.
14 Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.
15 Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti.

Angalia Upendo wa Mungu ndipo utajiwa kuwa alikuwa bado anaupendo na in mpaka Kesho aliondoa au alimuosha mwanadamu baada ya kutenda dhambi kitu cha kwanza ni hiki
Mwanzo 3:21
BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.

Hapa Mungu alichinja mnyama damu ikamwagika kwa maana ya kuosha dambi kikubwa siyo mavazi ni damu Kama ya Yesu ili Adamu apate kuishi,na shetani hasipate nafasi kusema basi atawatawala Mungu alikuwa bado anamwitaji huyo mwanadamu kwa hiyo ili dhambi isimtenge na Mungu ikabidi Mungu aiondoe kwa damu ya mnyama,

Zidi kuangalia Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu kaini anavyamiwa na Roho ya Uuaji kwa sababu Mungu anaupenda kwa aliyemuumba anamwambia kaini hivi
Mwanzo 4:6
BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

Leo hii kila kifo ni mpango wa Mungu hakuna kitu Kama icho watumishi tubadilike kwa kujua kusudi la Mungu na kujua mpango wa shetani
Angalia Upendo wa Mungu kwa sodoma na Gomorrah walikataa kutubu dhambi zao wangeokoka na moto
Yuda 1:7
Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele.
Vilevile wakati wa Nuhu Kama wangetubu wangeokoka lakini walikataa kwa Upendo wa Mungu alimtuma Nuhu lakini hawakumsikiliza walikataa Neno la Mungu ndiyo maana wakafa maji haukuwa mpango wa Mungu kuwauwa Kama wangetubu lakini in dhambi yao iliwauwa

Angalia Upendo wa Mungu kwa wana wa Israel alituma Musa kuwaokoa kutoka utumwani na kuwaongoza jangwani na huko aliwapa sheria ya kuwafanya kuishi na kwayo na kuifanya, akaweka Mtu ukitenda dhambi kuna damu ya mnyama ya kumuosha ili awe karibu na Mungu maana dhambi inamtenga Mtu na Mungu lakini hawa watu waliotoka Misri walikataa kuamini Mungu wakafia jangwani,haukuwa mpango wa Mungu kuwauwa Bali kutokutii kwao kuliwaua,Kama ni ingekuwa ni mpango wa Mungu wangefia Misri.

Angalia Upendo wa Mungu kwetu akamtoa mwana wake wa pekee
Yohane 3:16
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Leo hii kila kifo ni Mungu nakataa kwa herufi kubwa
Mpango wa watu kufa ni shetani na dhambi na kutokutii Mungu uwezi kuwa Mtumishi wa Mungu ukafa kwa mateso ya magonjwa hakuna kitu Kama hiyo,Wengine usemaga mbona Elisha alikufa kwa ugonjwa nakataa kwa herufi kubwa Yesu alikuwa hajaja,mbona Ezekia aliyekuwa na kansa na pamoja aliambiwa atakufa alikataa na akapona na hapo Yesu alikuwa hajaja,tena mbona Ayubu aliandamwa na kila ugonjwa na hakufa?na Yesu alikuwa hajaja?
Tusihubiri Injili Yesu ambayo hakuitoa au kutuma.....
Daudi mwenyewe anasema hivi
Zaburi 118:17
Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
Kifo cha watakatifu ni kulala siyo magonjwa maana Yesu aliyatwaa siyo ajali maana umeagiziwa malaika
Kama ukitenda dhambi na kutotii basi utakufa hivyo Ezekia alipotubu aliokokana kifo na kupona ugonjwa wake je wewe si zaidi Yesu alikufa kwa ajili yako badilika ili usipotwe na uovu wa shetani katika jina la Yesu

Zaburi 103:3
Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,
Ubaikiwe na Bwana Yesu amen.

King Sam
Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067
Namba ya whatsapp hii +447977225185
Ubarikiwe na Yesu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.