SOMO: WAKIFUNGA MILANGO MUNGU ATAINGILIA KATI - ASKOFU GWAJIMA

Mfano wa mlango uliofungwa ©GavinAdams
SOMO: WAKIFUNGA MILANGO MUNGU ATAINGILIA KATI

Unapotaka kufanya jambo linalotaka kukuletea matukio makubwa halafu unashangaa nguvu kubwa inaingilia kati ili kukuzuia usilifanikishe fahamu kuwa huo ndio wakati ule Mungu huingilia kati ili jambo hilo litimie kama ilivyokusudiwa.


Panapofikia wakati wa Kusudi la Mungu, Mungu anaweza kukufuata popote pale ulipo bila kujali umesoma, una elimu au uko kwenye hali gani. Mungu alifunga safari akaenda jangwani kumtafuta mtu ili amtumie, alipofika jangwani akamkuta Musa kando ya mlima wa midiani ambao sasa unaitwa mlima wa Bwana. Musa aliona kijiti kinawaka moto. Cha ajabu Mungu aliamua kukaa kwenye kichaka kwaajili ya kumchukua mtu mwenye kusudi naye. “Bwana amefanya appointment na wewe na tabia yako ileile haijalishi jinsi ulivyo” Musa alikuwa na miaka themanini na bado alimchagua ili amtumie, Mungu anaweza kusema nawe lakini hatua ya kwanaza unatakiwa usogelee kichaka. Musa alimsogelea Mungu alipokuwa kwenye moto na Mungu akamwambia nimeshuka kukufuata nataka uende Misri ukawaokoe watu wangu sababu nimesikia kilio chao na unamfahamu farao na nitakuwa pamoja na wewe. Mungu anakwenda pamoja na wewe kwa walewale walio kuloga, walio kuonea, walio kuumiza, walewale waliokutesa Mungu anakutuma uende na anakwenda pamoja na wewe.

Musa alihitaji tukio ili aamini aende alipo tumwa na Mungu, Mungu hakumkatalia na akamwambia weka mkono wako kwenye ukwapa na Musa akaweka na alipoutoa mkono wote ukawa na ukoma, kwa wayahudi kipindi kile ukiwa na ukoma unatengwa na jamii mpaka unakufa kwahiyo Musa alipoona akaogopa na kumwomba Mungu aurudishe uliyokuwa na Mungu akamwambia weka tena mkono wako na alipoweka mkono ukawa mzima. Mungu alijua Musa anamwogopa kobra wa Misri ambaye ni kama Mungu wa wamisri na anauwezo wa kumpofusha mtu asione kwa mate yake ndipo akamwambia Musa tupa fimbo yako chini nayo ikageuka ikawa kobra Mungu alimaanisha Musa akienda kwa farao amtumie kobra huyo kuwashinda kobra wa farao na alifanya hivyo, Tunatakiwa tutumie silaha za maaduni kuwateketeza wenyewe na yeye ambomoaye boma nyoka atamuuma, achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe kwa jina la Yesu. Mungu akamwambia Musa ainyanyue fimbo ile aondoke nayo maana fimbo ile ndiyo iliyotumika kuwavusha wana wa Israeli.
Akili kubwa kuliko zote duniani ni akili ya kufahamu majira na jinsi ya kutenda kwa wakati huo maana kuna wakati wa kurusha mawe na wakati wa kukusanya mawe, kuna wakati wa kuuwa na wakati wa kuuhisha. Musa akaenda kwa farao kuongea naye akiwa amesha kuwa mtu tofauti ametengenezwa na Bwana kwenye jangwa la mateso na shida akawa mtu tofauti tayari kumkabili farao, Mungu akitaka kukutumia anakutengeneza ili uwe mtu tofauti, Mungu akitaka kukutumia anakutengeneza kwanza utukanywe kwanza, uzomewe kwanza, uhangaike kwanza na ukishakuwa tayari anakutuma ukatimize kusudi lako alilokupa.

“Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtu Hata milele. Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake. Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu. Wala kuwahuzunisha.” Maombolezo 3:31-32

Mlokole yuko juu sana kuliko elimu yeyote, kuliko jina lolote litajwalo, kuliko jambo lolote na ameinuliwa juu, Mungu ameifuata serikali ya Tanzania anainyanyua kutoka shimoni anaiweka juu, Mungu amekuja kwenye maisha yako anakunyanyua na kukuweka juu, Mungu kwetu ni Mungu mwenye nguvu na ni mwamba wa kale. Bwana ndiye mchungaji wa Tanzania na serikali yake, na Bunge lake, na Ikulu yake, na majeshi yake, na usalama wake, na amani yake, na watu wake haitapungukiwa na kitu. Ukienda porini kuwinda huwezi kuona ndege aina ya tai sababu wanakuwa wako juu sana lakini ukimaliza kuchuna utawaona wamekuja wengi, wana wa Ufalme wote ni kama ndege aina ya Tai wako juu ya wote hakuna jambo wanaloshindwa kuliona. Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni ambalo ni Yesu kristo. Tai anaangalia kutokea juu.
Musa alipita kwa farao na farao akamkumbuka, Musa akamwambia jambo la kwanza Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo amesema waache watumwa ulio wamiliki wasafiri mwendo wa siku tatu jangwani ili wakamwabudu Bwana wao, farao akajibu kwa kiburi akiuliza Mungu ni nani na kwanini nimskilize, cha pili akamwambia nyoka wa Misri atakuteketeza nipe ishara huku wale wazee na wachawi na wenye akili wakimwangalia, Musa akaichukua ile fimbo aliyokuwa nayo akaiangusha chini ikageuka ikawa kobra wa Misri ambaye sio pepo, wale wazee wa Misri wakadondosha fimbo zao na fimbo zao zikawa nyoka kama wa Musa na farao akafurahi kwasababu Musa alikuwa na nyoka mmoja dhidi ya wale wengi wa kichawi ambao ni pepo lakini aliwameza nyoka wote wa wale waganga na akageuka fimbo ambayo imemeza nyoka miamoja. Maana yake ukifunga milango ya kuwaruhusu watu watoke Mungu ataingilia kati na kuwakomboa.

“Basi palikuwa na mvua ya mawe, na moto uliochanganyikana na ile mvua ya mawe, nzito sana, ambayo mfano wake haukuwapo katika nchi yote ya Misri tangu ilipoanza kuwa taifa. Na ile mvua ya mawe ikapiga kila kilichokuwako mashambani, binadamu na mnyama, katika nchi yote ya Misri; hiyo mvua ya mawe ikapiga kila mmea wa mashambani, na kuuvunja kila mti wa mashamba. Katika nchi ya Gosheni peke yake, walikokaa wana wa Israeli, haikuwako mvua ya mawe. Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; Bwana ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu. Mwombeni Bwana; kwa kuwa zimekuwa za kutosha ngurumo hizo kuu na hii mvua ya mawe; nami nitawapa ninyi ruhusa mwende zenu, msikae zaidi. Musa akamwambia, Mara nitakapotoka mjini nitamwinulia Bwana mikono yangu; na hizo ngurumo zitakoma, wala haitanyesha mvua ya mawe tena; ili upate kujua ya kuwa dunia hii ni ya Bwana.” Kutoka 9:24

Musa aliamua kushusha mvua ya uharibifu kwenye nchi nzima ya Misri lakini haikupiga Gosheni mahali ambapo wana wa Iisraeli Wanakaa. farao akashangaa jinsi alivyokuwa anaongoza mvua na radi na Musa alipomwendea ili apate ruhusa yakuondoka farao akakataa tena. Musa alikwenda kupiga maji baharini na maji yakagawanyika ikawa damu lakini farao hakuwaruhusu sababu alidhania ataendelea kumfanya Musa atumie maajabu yake yote ili yaishe na aendelee kumkandamiza lakini hakujua kama Mungu ameingilia kati jambo lile na miujiza yake haiishi. Musa akatoa chawa lakini farao hakumsikiliza, Musa akafanya uchunguzi wa wanaompa kiburi farao ni kina nani na ndipo akafahau ni waganga wa kienyeji Musa akaamua majipu yawapate wote na farao baada ya kuyaona yote yale farao akamwambia akienda kumwona tena atamuuwa na Musa akaambiwa na Mungu yeye farao ndiye atakaye kufuata wewe, Mungu akamwambia atakwenda kuiachilia roho ya kifo ipite kwa kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, huko gosheni Wana wa Israeli walipewa maelekezo na Musa wachinje kondoo bila kukata mfupa na wale chakula usiku wajiandae tayari kuondoka Misri na kupaka damu juu ya nyumba zao na ile roho ya kifo ikipita ikiona damu itapita juu. Wana waIsraeli walikuwa wanakula ili waondoke na leo tunakula ili tuondoke kwenye umasikini tulioupata, tunaondoka na dhahabu zetu, familia zetu, kazi zetu. Wakati watu wanalalamika wewe utakuwa unajenga kwa jina la Yesu kristo, wakati watu wanalalamika upepo umegeuka wewe ndiye utakayekuwa unatengeneza upepo, wakati wengine wanalia wewe utakuwa unacheka na kusonga mbele unachukua kila chombo cha mmisri, unaondoka na kila chombo na mali nyingi.

Musa alikuwa amepitia shida za kumtosha, kwenye matatizo ya kumtosha alikuwa jangwani kwa muda wa miaka 40 na anaijua njia vizuri anazifahamu dhiki zote vizuri, alikuwa ameiva kwaajili ya kuwapeleka wana wa Israeli kwenye nchi yao ya ahadi. Farao aliwaendea wayahudi ili waondoke haraka lakini wayahudi hawakuwa na haraka bali waliuchukua ule utajiri wa farao na wamisri na Biblia inasema wayahudi waliondoka katika nchi ya Misri kwa jeuri na mali za wamisri walizokuwa wakizitaka hakupatikana wa kuwazuia kuzichukua. Biblia inasema wakaondoka na kila walichokuwa wanahitaji.

Wamisri walikuwa na msiba mkuu na hakuna aliyemsaidia mwenzake kuzika sababu kila mtu alipatwa na msiba. Farao akaona dalili kabisa wanakwenda na hakuna tatizo akapawa na wazo ili awafuate na Biblia inasema wakachaguliwa watu mia sita ili wawafuate wana wa Israeli warudi nao na wale askari mia sita waliochaguliwa walikuwa ni wamwisho. Kwao upo mkono wa mwanadamu lakini kwetu sisi upo mkono wa Mungu.

Mungu alipowaondoa watu wake katika nchi ya utumwa ya Misri akaamua kutowapitisha njia fupi yenye wafilisti na wakapita njia ndefu hadi baharini. Musa anaijua njia ya Mungu mfuate mpaka mwisho hata kama huelewi njia fuata mpaka mwisho atakuvusha baharini uende kwenye nchi ya ahadi, akili kubwa ya kuelewa Biblia ni kuikubali mpaka mwisho, ukiitii sauti ya Mungu utafanikiwa, akili mbovu kuliko zote duniani ni kuulizauliza kuhusu Bwana. Ukimtii Bwana Mungu na kutii Sheria zote alizokuelekeza Baraka hizi zitakufuata, ukiwa mahali popote utabarikiwa.

Musa asiye na fimbo usimfuate sababu bahari inaangalia Musa mwenye fimbo aliyotoka nayo jangwani ndipo imtii, siyo ya kichungaji. Kwenye Biblia fimbo ni ishara ya neno la Mungu. Mahali walipoingia wana wa Israeli palikuwa pana milima kila upande na wakashindwa kurudi nyuma sababu wamisri walikuwa wanakuja, na wana wa Israeli wakasahau ile nguvu iliyowaua wazaliwa wa Kwanza, Musa alikuwa anajua majeshi ya farao yanakuja na alikuwa tayari kuyakabili.

“Na Bwana akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa ujeuri. Wamisri wakafuata nyuma yao, farasi zote na magari yote ya Farao, na askari zake wenye kupanda farasi, na jeshi lake, nao wakawapata hali wamepanga pale karibu na bahari, karibu na Pi-hahirothi, kukabili Baal-sefoni. Hata Farao alipokaribia, wana wa Israeli wakainua macho yao, na tazama, Wamisri wanakuja nyuma yao; wakaogopa sana; wana wa Israeli wakamlilia Bwana. Wakamwambia Musa, Je! Kwa sababu hapakuwa na makaburi katika Misri umetutoa huko ili tufe jangwani? Mbona umetutendea haya, kututoa katika nchi ya Misri? Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani. Musa akawaambia watu, Msiogope, simameni tu, mkauone wokovu wa Bwana atakaowafanyia leo; kwa maana hao Wamisri mliowaona leo hamtawaona tena milele.” Kutoka 14:5-

Mungu aliongea neno la kiimani kabla hajatenda jambo, mambo yakifunga Mungu huingilia kati, mahali ambapo uwezo wa kibinadamu umefikia mwishi Mungu huingilia kati na kufanya jambo la ajabu. Musa aliwaambia wana wa Israeli tulieni Muuone utukufu wa Bwana, ‘Upepo wa Bwana unavuma Tanzania unaigawa bahari’. Musa alipoigawanya bahari wana waisraeli hawakuwa na maswali na vilio vyao vilisimama wakaanza kupita katikati ya bahari. Wana wa Misri waliingia baharini ili wawafuate waisraeli, watu wa Mungu walipotoka nje ya maji wamisri wakawa wako katikati ya maji, na Musa akaipiga ile fimbo mara nyingine na maji yakawafunika wamisri wakaelea.

Kwenye kitabu cha Ufunuo imeandikwa watatifu watakapoingia mbinguni zitachukuliwa nyimbo mbili za Musa na Mwanakondoo. Wamisri walitaka na wao wawahi kabla bahari jaijagawanyika, ile nuru ya moto ya wana waisraeli ilikuwa inawamulikia wamisri wakawa wanaona njia ya kuwafuata wana wa Israeli lakini lile wingu likarudi nyuma na kukaa nyuma ya waisraeli hivyo kufanya wamisri wasione njia ambapo ilipofika zamu ya alfajiri Mungu alichungulia jeshi la wamisri tairi za magari yao zikachomoka na wakaanguka. Usiogope wakikufuatitia kwenye ndoa yako, biashara yako, kazi yako ikifika zamu ya alfajiri Mungu ataingilia kati na wataanguka kwa jina la Yesu.

“ Wana wa Israeli wakaenda ndani kati ya bahari katika nchi kavu; nayo maji yalikuwa ukuta kwao mkono wa kuume, na mkono wa kushoto. Na wale Wamisri wakawafuatia, wakaingia ndani kati ya bahari, farasi zote za Farao, na magari yake, na wapanda farasi wake. Ikawa katika zamu ya alfajiri, Bwana akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri. Akayaondoa magurudumu ya magari yao, hata yakaenda kwa uzito; na Wamisri wakasema, Na tukimbie mbele ya Israeli; kwa kuwa Bwana anawapigania, kinyume cha Wamisri. Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako juu ya bahari, ili maji yarudi tena juu ya Wamisri, juu ya magari yao, na juu ya farasi zao. Musa akaunyosha mkono wake juu ya bahari, na kulipopambazuka, bahari ikarudi kwa nguvu zake; Wamisri wakakimbia mbele yake; na Bwana akawakukutia mbali hao Wamisri kati ya bahari. Yale maji yakarudi yakafunikiza magari na wapanda farasi, hata jeshi lote la Farao lililoingia katika bahari nyuma yao; hakusalia hata mtu mmoja. Lakini wana wa Israeli wakaenda katika nchi kavu katikati ya bahari; na hayo maji yalikuwa ni kuta upande wao wa kuume, na upande wao wa kushoto. Ndivyo Bwana alivyowaokoa Israeli siku ile mikononi mwa Wamisri; Waisraeli wakawaona Wamisri ufuoni kwa bahari, wamekufa. Israeli akaiona ile kazi kubwa aliyoifanya Bwana juu ya Wamisri, ndipo hao watu wakamcha Bwana, wakamwamini Bwana, na Musa mtumishi wake. Ndipo Musa na wana wa Israeli wakamwimbia Bwana wimbo huu wakanena, na kusema, Nitamwimbia Bwana, kwa maana ametukuka sana; Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini. Bwana ni nguvu zangu, na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Yeye ni Mungu wangu, nami nitamsifu; Ni Mungu wa baba yangu, nami nitamtukuza. Bwana ni mtu wa vita, Bwana ndilo jina lake.” Kutoka 14:22-

Wana wa Israeli walipokwenda kila mahali walipozuiliwa Mungu aliingilia kati. Kama kuna watu wanamwabudu Mungu wa hakika ni sisi, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo ni Mungu wa maajabu na ishara, ni Mungu wa vita.

Musa alikuwa anauwezo wa kuongea na jangwa na kuwavusha wana wa Israeli baharini pekee hivyo akamkabidhi Joshua.Wana wa Israeli wakiongozwa na Joshua walifika mahali wakakuta ukuta mrefu wa ngome ya utawala, Ukuta wa Yeriko ndio ukuta wa mwisho wa kuingia kwenye nchi ya ahadi, watu wa yeriko walikuwa wamefunga milango kwa makufuli makubwa ili wana wa Israeli wasiingie ndani. Yoshua alikuwa hagawanji maji kwanza ndipo apite lakini yeye alikuwa anauwezo wa kwenda bila kungojea, “kizazi cha Musa ni cha kupita chini ya maji na kizazi cha Joshua ni cha kupita juu ya maji”. Jemedari wa jeshi la Bwana alimfuata Joshua kumsadia kuangusha ngome ya yeriko alipomfikia Yoshua alimwambia Yoshua avue viatu vyake na Yoshua akakumbuka ni Yule aliyemtokea Musa Jangwani na akamsujudia mpaka chini akaenda kuiangusha Yeriko pamoja na mtu anayeifahamu ngome ya Yeriko vizuri sana.

Wakati ukuta wa Yeriko umefungwa Mungu aliongea maneno haya

“Basi Yeriko ulikuwa umefungwa kabisa kwa sababu ya wana wa Israeli; hapana mtu aliyetoka wala hapana mtu aliyeingia. Bwana akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake. Nanyi mtauzunguka mji huu, watu wote wa vita, mkiuzunguka mji mara moja. Fanya hivi siku sita. Na makuhani saba watachukua tarumbeta saba za pembe za kondoo waume, mbele ya hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga tarumbeta zao.” Yoshua 6:1-2

Wana wa Israeli waliuvunja ukuta wa Yeriko kwa kuuzunguka mara sababa wakaingia kwenye nchi ya ahadi na kumiliki, usiuogope ukubwa wa Ukuta wa Yeriko wa maisha yako zunguka utaanguka na utaingia kumiliki kwa jina la Yesu

Namba ni mpango wa Mungu kwenye Biblia namba tatu ni namba ya kutapikwa ‘Yesu siku tatu’ na ‘Yona siku tatu’, namba Tano ni namba ya nguvu ya uweza, Mamlaka, Namba Saba ni namba ya ukamilifu, namba Ishirini na moja ni namba ya kutembelewa Danieli alitembelewa siku ya ishirini na moja. Wana wa Israeli walipozunguka siku ya saba siku ya saba walizunguka mara saba mbali ya ukuta.

Lipo tendo ambalo Mungu analiingilia kati kwenye maisha yako limefungwa na Mungu taingilia kati ili pafunguke uingie na kumiliki vyote vilivyomo ndani yake. Bwana anasema nendeni mtamkuta mwanapunda amefungwa mfungueni na mtu akiwauliza mwambie Bwana ana haja naye, kila kufuli la magonjwa, mikosi, kukataliwa funguka kwa jina la Yesu.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.