UJUMBE: TUMAINI LIPO KWA YESU TU - KING SAMTUMAINI LIPO KWA YESU TU;
Mahali ambapo dunia imefikia ni pabaya na si sehemu flani tu ni kila mahali duniani,watu wamekuwa wamekuwa wanatumaini vitu,wameweka matumaini si KWA Yesu tena,
Ogopa kuona mpaka wachungaji waimbaji watu waliokuwa wanamtumikia Mungu wamegeuka na kuona Tumaini la maisha yao lipo kwenye Saisa,
Wanawake wameweka tumaini Lao kwa wanaume wanatumaini wakiolewa maisha yao yatabadilika,
Wanaume nao vile vile mpaka wengine wanafikiri wakienda ulaya ndipo watafanikiwa,ndiyo maana wengine wanaiba wengine wanauza madawa ya kulevya,
Lengo ni wanatafuta tumaini la maisha Yao,

Watu wamefika mahali wanafikiri viongozi kwenye nchi ndiyo watawaletea matumaini ya mafanikio katika hali walio nayo,juweni hata hao nao ni wanadamu wenyewe wanafikiri kuwa viongozi wa nchi watapona nao wameweka tumaini kwenye uongozi,watu wanawatumainia wanadamu,
Yeremia Jeremiah 17:5
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA.
6 Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema; Bali atakaa jangwani palipo ukame, Katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu.
7 Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.

Kwa nini umasikini utazidi katika jamii au katika nchi au kanisani kwa sababu watu wameacha kumtumaini Kristo Yesu wamegeukia vitu siasa wanadamu,
Mtu atakaiye barikiwa katika ulimwengu huu na kwenda mbinguni ni Mtu yule tu atakaye weka Tumaini lake kwa Yesu,

Wachungaji wengi hawafungui huduma kwa sababu ya kumtumikia Mungu Bali ni sehemu ya maisha yao yaani siyo lengo ni kumtumikia Kristo kwa moyo ni ili wafanikiwe kimaisha wawe na pesa na magari na majumba kwa sababu Tumaini kwa Kristo halipo,
Ndiyo maana wanataka pesa kwa kila njia maombezi ni pesa,wanauza mafuta mani nk

Yesu alisema neno ili
Yohane John 16:33 Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Ukweli badilikeni YESU tu ndiye tumaini la maisha yake na watoto wako na kazi yako na ndoa yako,
Hakuna njia nyingine.

King Sam
Kama unataka niwasiliane na wewe kwenye simu namba yangu hii hapa +447903180067
Namba ya whatsapp hii +447977225185
Ubarikiwe na Yesu

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.