UPONYAJI KWA WANANDOA JUMAMOSI HII SINZA CHRISTIAN CENTER


Kipindi cha uchumba, watu wengi hukifurahia. Ni kipindi ambacho wapendanao huonyeshana kila aina ya upendo na kutabasamiana kiasi kwamba watu hutamani hilo jambo liendelee. Wengine hufanbikiwa kuendeleza, na wengine mara baada ya tu ya kuwa wanandoa, baada ya muda mambo hubadilika. Pengine kwa mawazo kwamba "sasa hakuna wa kuniibia, huyu ni wangu" na kwamba "hata nifanyeje yeye ni wangu, hawezi kuondoka". Tunajisahau kwamba ili mahusiano yoyote yaweze kudumu kwa amani na furaha, ni lazima upendo wepo mara dufu na kuwe na namna bora ya utatuzi wa migogoro inayojitokeza.

Kuna mengine mengi unayajua wewe mke ama mume wa mtu kwa kadri unavyoishi na mwenza wako. Hili linawezekana kwa wanandoa, iwe waliofunga ndoa mwezi mmoja uliopita, ama wana miaka kumi pamoja, na hata miaka 30. Kwa pamoja jambo lenye heri la mabadiliko linaweza kufanyika kupitia semina muhimu ya wanandoa itakayofanyika mwisho wa mwezi huu, yaani Jumamosi tarehe 29 Agosti 2015 katika ukumbi wa SINZA CHRISTIAN CENTER – SINZA KUMEKUCHA kuanzia saa 4:00 kamili asubuhi hadi saa 12:00 jioni, ambapo pia chakula cha mchana kimeandaliwa.

Mwalimu katika semina hiyo muhimu ni Mtumishi wa Mungu Mchungaji Mitimingi

Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na Branea Spiritual Family, ambao ni waandaaji wa semina hiyo kupitia

Bwana Marco Yambi - 0767 056109 ama 0767 555792

Osca Mwarabu - 0718193901

Ewe mwanandoa, tukutane huko kuhuisha na kuboresha zaidi ya kile kipindi cha uchumba.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.