WASTAHILI NDIO CHAGUO LA GK ALBUM MPYA YA WANA WA NG'ANG'ANIA SHINYANGAHakuna ubishi kwamba linapokuja suala la uimbaji mzuri uliopangiliwa vyema basi kwaya ya AIC Shinyanga ni moja ya kwaya nchini inayoendelea kutumika kwa viwango vya juu na kuendelea kushikilia usukani wa kufanya vyema kwenye tasnia ya muziki wa injili nchini. Kupitia chaguo la GK jumapili ya leo tumeamua kukuwekea moja ya nyimbo zinazopatikana katika album yao mpya kabisa iliyotoka karibuni iitwayo 'Pigo la Fainali' wimbo tuliokuchagulia unaitwa 'Wastahili' ni wimbo wa kumrudishia Mungu sifa na utukufu kwa matendo makuu anayotutendea kila iitwapo leo.

Licha ya kwamba wimbo huu una maneno mazuri lakini pia mpangilio wa sauti ukiongozwa na solo aliyeanzisha basi utakubaliana na GK kwamba wana wa Ng'ang'ania wamefanya kazi nzuri inayostahili pongezi. Basi tukutakie utazamaji na usikilizaji mwema wa wimbo huu. Jumapili njemaShare on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.