13 SEPTEMBA NI ZAMU YA TUPONILE KOMBA JIJINI ARUSHA

Baada ya kumaliza tamasha kubwa la kusifu na kuadubu ndani ya E.A.G.T Elerai Jijini Arusha, sasa ni zamu ya Tuponile Komba kuzindua DVD ya Kesho Yako Inakuja.

Kama hujui kilichojiri kwenye audio yake basi fika Jumapili ya tarehe 13 uone namna ambavyo Mungu anamtumia muimbaji huyu pamoja na mume wake, Mtumishi wa Mungu Michael Komba. Sanjari naye waimbaji kadha wa kadha watakuwepo kusindikiza tukio hilo, akiwemo Martha Baraka, Kwaya ya Matendo, Kwaya ya Ebenezer, Kwaya ya Ukombozi, pamoja na waimbaji wengine kutoka One Voice Family International. Familia anayotokea Tuponile.

Endelea kufuatilia ukurasa huu wa GK, nasi tutakulelera taarifa zaidi kwa kadri zinavyotufikia.Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.