AMKA USILALE MAFISADI WASIKUANGAMIZE NDIO CHAGUO LA GK LA LEO, TAZAMAJumapili ya leo katika chaguo la GK tumekuchagulia wimbo uliobeba ujumbe mahususi kwaajili yako mdau wetu wa GK kutoka kwa kwaya maarufu ya Uinjilisti Kijitonyama Lutheran jijini Dar es salaam, wimbo unaitwa "Amka Usilale" ambao ujumbe wake unaendana na hali iliyopo kwasasa katika kuelekea uchaguzi mkuu mwezi ujao.

Tunakutakia utazamaji na usikilizaji mzuri wa wimbo huu katika kusindikiza jumapili yako. Barikiwa sana, vinginevyo usikose tarehe 27 ya mwezi huu katika uwanja wa taifa wa zamani ama uwanja wa Uhuru ambako kwaya ya Efatha Uhuru Moravian Kariakoo, waliotamba na wimbo kama twaomba amani ama mafarakano, usalama uko wapi na nyinginezo watakuwa wakizindua album yao wakisindikizwa na waimbaji mbalimbali wakiwemo Uinjilisti Kijitonyama. Usikose


Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.