ASOMAE NA AFAHAMU


Na King Sam

ASOMAE NA AFAHAMU 

Nachoweza kuwaambia ndugu zangu katika Kristo Yesu tafuteni Neno la Mungu maana tupo kwenye nyakati za hatari nyakati ambazo Mtu atakuja kuokolewa tu na Neno la Mungu alilonalo ndani yake,kwa mujibu wa biblia kunawakati unakuja nautatafuta kulisoma Neno na hautaweza kwa sababu utakuwa umezungukwa kila kona,biblia inasema hivi...
Amosi Amos 8:11
Angalia, siku zinakuja, asema Bwana MUNGU, ambazo nitaleta njaa katika nchi; si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya BWANA.
12 Nao watatanga-tanga toka bahari hata bahari; na toka upande wa kaskazi hata upande wa mashariki; watapiga mbio, wakienda huko na huko, kulitafuta neno la BWANA, wasilione.

Ndugu zangu Kama ilivyoandikwa katika biblia kimeshatimia kila kitu wakati utakapofika utendaji kazi yake utaweza kuokoka kama haukuwa na Neno la Mungu ndani yako maana utaweza kupasa sauti ukitaja Yesu bali lile Neno ndani yako ndilolitakuwa linakuokoa maana malaika wenyewe wanalisikiliza Neno ili walitendee kazi siyo sauti ya kelele ni sauti ya Neno, biblia inasema hivi....
Zaburi Psalms 103:20
Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.

Je unaweza kuokolewaje na Mungu?ni kupitia Neno lake tu ulilolibeba kunawatu wanafikiri kwa sababu eti wameumbwa na Mungu basi Mungu atawaokoa ndugu yangu nikuambie kweli Kama hautatafuta Neno la Mungu uwezi kuokoka na uharibifu ndiyo maana Mungu alimtua Yesu iliumtafute ukimpata uokolewe kupiti yeye Yesu in Neno la Mungu na Kama hauna Neno hauna Yesu na Kama hauna Yesu hakuna kuokolewa na uharibifu,biblia inasema hivi....
Ufunuo Revelation 3:10
Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

ASOMAYE NA AFAHAMU
Hizi ndiyo roho zimetkuja duniani tayari zipo zimeaza kazi ilia hazijalipuka ili kufikia mwisho balizipo tayari unaweza Ona Iraq na Syria na nchi zingine hizi Roho zitaenea ulimwengu mzima muda si mrefu kama uwezi sasa hivi kutafuta Neno utalipata wakati huo,Angalia kule Iraq Na Syria hawawezi kulitafuta Neno

KUNA FARASI WANNE ZISOME KWA MAKINI UPATE UFAHAMU,
Ufunuo Revelation 6:2
Nikaona, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda ana uta, akapewa taji, naye akatoka, ali akishinda tena apate kushinda.

3 Na alipoifungua muhuri ya pili, nikamsikia yule mwenye uhai wa pili akisema, Njoo!

MSTARI WA NNE NI SILAA ZA VITA NA VITA KUUA WATU
4 Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa AMANI katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa UPANGA mkubwa.

5 Na alipoifungua muhuri ya tatu, nikamsikia yule wa tatu mwenye uhai akisema, Njoo! Nikaona, na tazama, farasi mweusi, na yeye aliyempanda ana mizani mkononi mwake.

MSTARI WA SITA NI KUHUSU BEI KWENYE SUPERMARKET ITAKAVYOKUWA...
6 Nikasikia kama sauti katikati ya hao wenye uhai wanne, ikisema, KIBABA cha ngano kwa nusu rupia, na vibaba vitatu vya SHAYIRI kwa nusu rupia, wala usiyadhuru MAFUTA wala DIVAI.

7 Na alipoifungua muhuri ya nne, nikasikia sauti ya yule mwenye uhai wa nne akisema, Njoo!

MSTARI WA NANE NI KUHUSU VIFO KUPITIA NJAA,TAUNI NI MAGONJWA NA KUPITIA VITA
8 Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni MAUTI, na Kuzimu akafuatana naye. Nao wakapewa mamlaka juu ya robo ya nchi, waue kwa UPANGA na kwa NJAA na kwa TAUNI na kwa hayawani wa nchi.

Ndugu yangu hizi FARASI uwezi pona pasipokuwa na Neno la Mungu kila siku najaribu kufundisha Neno ili uje upone pasipo Neno hautapona kuna watu wanatafuta umaarufu badala ya kutafuta Neno nawaambia pesa hazisaidii mtu kwenye hizi FARASI wala umaarufu wako,
NENO NDILO LITAKUPONYA TU NENO LA MUNGU,
UBARIKIWE NA YESU UKITAFUTA NENO LAKE,AMEN.
Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.