CHAGUO LA GK: NJOONI TUSEMEZANE

Uhali gani mpenzi msomaji wa GK, tunatumai kwamba Jumapili ya leo imeenda vema upande wako. Maana katika yote BWANA Mungu anasema Njooni tusemezane, hivyo haijalishi unahisi na kujistukia kwamba una lumbesa la dhambi - tena za rangi nyeusi tii.

Kwa Neno lake tu tumefanyika kuwa wana - wote walioamua kumpokea. Basi katika hili Chaguo la GK kwa wiki hii tuko na Douglas na Nelson (waite Dolaa na Nelly) kutoka Jijini Arusha, nao wanatukumbusha Maneno ya Mungu, kwamba njooni tusemezane. Haijalishi uko hatua gani, ya kujiua ama kurudishwa nyuma. Tamka Neno naye atakusikia, maana maombi hayawezi ku-expire.


Jumapili njema yenye baraka tele.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.