CHRISTIAN FASHION DAY 2015 NI LEO HII NDANI YA NEW SAFARI HOTEL ARUSHA


Yakiwa yamebaki masaa kuelekea tamsha la ulimbwende wa mavazi hapo kesho 26th Septemba, New Safari Hotel,Kuanzia saa nane mchana
CHRISTIAN FASHION DAY ni siku maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya wakristo wote wa ulimwengeni kusherekea imani yao katika mtazamo wa uvaaji unaokidhi utanashati, ustaarabu na nidhamu.

Ni siku ambayo wabunifu wa mavazi wa kikristo bila kujali dhehebu au tofauti za mfumo wao wa ibada wanakutana kujadili na kuzungumzia maswala muhimu yanayohusu mavazi stahiki na muonekano sahihi unaomfaa mkristo.

Tukio hili kuitwa CHRISTIAN FASHION DAY haikuwa na lengo la kutenga Imani zingine, hapana bali lengo kuu ilikuwa kuonesha msimamo wa kiimani na kujenga mtazamo halisi wa vitu na mavazi yatakayooneshwa katika siku hiyo kujali utanashati, ustaarabu na nidhamu.CHRISTIAN FASHION DAY ni wazo lililotokana na kijana mbunifu wa mawazi mkristo anayeitwa Isack Jonas mwenye label yake ya mavazi inayoitwa BENIS. Kwa kukulia kwake kanisani tangu utotoni ukizingatia ni mtoto wa mchungaji amekua akiona na kusikia mijadala mingi sana ikiibuka makanisani juu ya mavazi na muonekano unaomfaa mtu anayesema ameokoka na ni mkristo, hivyo baada ya kuanza kutumia kipawa alichopewa na Mungu cha kubuni mavazi akaamua atumie ujuzi huo kuandaa tukio hili ambalo lengo kuu ni kurejesha utanashati wenye maadili na kukuza utamaduni wa muafrika katika viwango vikubwa Zaidi kujulikana, kufahamika na kuheshimika.

Tukio hili pia linalenga kuwajengea vijana wa kikristo uwanja wa kutumia vipaji na vipawa vyao vya ubunifu wa mavazi au uoneshaji wa mavazi stejini (modeling) bila kuwa na hofu ya kufanya kazi na watu au makampuni yatakayoweza kuingilia Imani zao na kuwakosesha uhuru wa kutumia vipawa hivyo.

Pia tumekusudia kuuonesha umma wa watanzania na ulimwengu kwa pamoja kuwa mbali na hayo ambayo ulimwengu unaweza kukuonesha pia kuna uchaguzi mwingine ulio bora Zaidi katika uvaaji na kupendeza.
Tukio hili limeandaliwa na vijana wakristo Arusha baada ya kushirikishwa wazo hilo na Isack.
Mbali na BENIS pia CHURCHBOY CHURCHGIRL INITIATIVE umoja ambao unawahimiza vijana kumtumikia Mungu kwa kutumia vipawana karama walizopewa wamehusika saan katika kuandaa tukio hili hivyo kuleta picha kubwa na nzuri ya ushirikiano mkubwa uliopo ndani ya vijana waliochagua kumfuata Kristo bila kusita au kubabaishwa na ulimwengu.


usipange kukosa 
GK nayo itakuwepo kukuletea tukio zima.


Share on Google Plus

About Bony Kazi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.