FAIDA CHACHE ZITOKANAZO NA KUJISOMEA VITABU MARA KWA MARA

FAIDA CHACHE ZITOKANAZO NA KUJISOMEA VITABU MARA KWA MARA 


Na Faraja Naftal Mndeme, 
GK Contributor.

I. KUJISOMEA VITABU HUONGEZA UWEZO WA AKILI KUFANYA KAZI KWA UFANISI ZAIDI. 
Mara nyingi unapotumia muda mwingi binafsi kwa kujisomea vitabu hukusaidia kuiwezesha akili yako kufanya kasi kwa ufanisi zaidi.Watu wengi wanaonekana wana akili zaidi kwenye ulimwengu wa sasa hutumia muda mwingi kujisomea vitabu mbalimbali kuongeza na kuboresha uwezo wa akili zao.Unapojiona una akili za kawaida jiulize unatumia muda gani kuweza kujisome na kujifunza mambo mbali mbali yanayopatikana kwenye vitabu.Watu wa Jamii ya Kiafrika ni wachache sana ambao hupenda kujisomea na kujifunza zaidi kwenye muda wao binafsi kwa kujisomea vitabu mbali mbali.Iwapo unahitaji kuboresha akili zako na uwe na uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua changamoto mbali mbali kwenye maisha yako binafsi,jenga tabia na uwezo wa wewe binafsi kujisomea vitabu mbali mbali. 

II. KUJISOMEA VITABU HUSAIDIA KUONGEZA NA KUBORESHA KUMBUKUMBU KATIKA UBONGO WAKO. Watu wengi wamekuwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu ukiacha mbali na wale waliopatwa na ajili au aina fulani ya athari kwenye ubongo wao .Namna moja wapo ya kuweza kuboresha na kuongeza uwezo wako wa kumbukumbu ni kuhakikisha unajenga uwezo binafsi wa kujisomea vitabu mbalimbali wewe binafsi.Hakikisha unakuwa na ratiba binafsi yaw ewe kila siku kuweza kujisomea na kujifunza mambo mbali mbali kwa kujisomea vitabu.Huwezi kuwa na kumbukumbu za kutosha na zilizo katika ubora unapaswa iwapo uwezo wako wa kujisomea wewe binafsi ni mdogo na hauweki jihudi binafsi na za makusudi za kuweza kujisomea. 

III. KUJISOMEA VITABU HUONGEZA UWEZO WA KITAALUMA. 
Wanataaluma wengi ambao wameonekana kufanya vizuri kwenye eneo fulani la kitaaluma mara nyingi watu wa namna hii wamejiwekea utaratibu wa kuweza kujisomea vitabu wao binafsi.Huwezi kufanya vizuri kwenye kiwango cha juu cha taaluma fulani iwapo wewe ni mvivu wa kujisomea na kujifunza mambo mbali mbali katika muda wako binafsi wa kujisomea vitabu.Iwapo unatamani kufanya vizuri zaidi kwenye eneo fulani la kitaaluma hakikisha unawekeza muda mwingi binafsi wa kujisomea vitabu . Uvivu wa kujisomea vitabu hupumbaza akili na kuifanya taaluma uliyokuwa nayo kufa kabisa/kutofanya vizuri katika kiwango cha juu kilichokusudiwa.Ukiona kwenye taaluma fulani haufanyi vyema jiulize muda binafsi unaotumia kujisomea vitabu mbalimbali. 

IV. KUJISOMEA VITABU HUKUSAIDIA KUJUA MAMBO MENGI ZAIDI. 
Muda mwingi nimekutana na watu wakijiuliza mtu fulani mbona anafahamu mambo mengi lakini bila wao kufwatilia kwamba inawezekanaje watu wengine wawe wanafahamu mambo mengi kuliko wao.Ukiona mtu anafahamu mambo mengi kuliko wewe tambua mtu huyo hutumia muda mwingi kujifunza na kujisomea vitabu yeye binafsi.Iwapo unatamani kufahamu na kujua mambo mengi kuliko watu wa kawaida hakikisha unajenga uwezo wake wa kujisoma vitabu bila kuwa mvivu.Tabia ya kujisomea binafsi ni tabia ambayo inajengwa taratibu na baada ya muda fulani kupita utajikuta umezoa na kujisomea itakuwa sehemu ya maisha yako maana utaona faida zake kwa undani zaidi. 

V. KUJISOMEA VITABU HUSAIDIA KUBORESHA MAISHA BINAFSI YA MSOMAJI. Maisha unayoishi yanatoa kiwango cha akili ulichonacho,hauwezi kuishi zaidi ya kiwango cha akili ulichonacho.Hauwezi kuishi maisha bora zaidi ya akili uliyonayo,iwapo unafikirIa kuishi maisha bora zaidi ya akili uliyo nayo imekupasa kupata akili mpya,moja ya njia muhimu ya kuweza kupata akili mpya ni kuweza kujisomea vitabu maana vitabu vitakupa taarifa mpya ambazo haukuwahi kuwa nazo na pindi utakapozipata na kuziweka kwenye vitendo maisha yako yataboresheka zaidi na kuwa vizuri zaidi ya pale ulipo leo.Hakikisha unaongeza akili zako kwa kuwekeza muda wa kujisomea vitabu wewe binafsi mara kwa mara na ukiwa na ratiba endelevu isiyo ya kubahatisha. 

E-mail: naki1419@gmail.com 
+255788454585 
God Bless You All.

Share on Google Plus

About Ambwene Mwamwaja

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.