HAKIKISHA UJUMBE HUU UNAMFIKIA UNAYEDHANI ATAKUWA RAIS WA TANZANIA

Baadhi ya wagombea kiti cha urais 2015 Tanzania Bara
Kabla ya kutangazwa kwa wagombea wa nafasi ya Urais kupitia vyama mbalimbali nchini kuliamsha hisia kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili ambao waliamua kuwapigida debe watiaji nia wanaodhani wanafaa kwa nafasi ya Urais wa Jamhuri.

Ujumbe uliomo katika wimbo huu ni watofauti kabisa, waimbaji wa kwaya ya Efatha Uhuru Moravian ya jijini Dar es salaam, wameweza kuwawakilisha vyema Watanzania sambamba na kusimama katika zamu yao kama waimbaji wa muziki wa injili, kwakutoegemea upande wowote zaidi ya kufikisha ujumbe huu mahususi kwa mgombea ambaye atashinda nafasi ya Urais kwamba kuchaguliwa kwake ni kwamba Watanzania wamemuamini kwamba atatumika vyema kutatua matatizo ya watanzania na zaidi wamemuombea.

Sitaki niharibu kwa maneno mengi ila sikiliza ujumbe huu maalumu kwako wewe Rais utarajiwaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nakuomba mdau hebu share ujumbe huu na ndugu, jamaa na marafiki ili kuhakikisha ujumbe unamfikia mlengwa. Hongereni sana Efatha Choir

Baadhi ya waimbaji wa Efatha Choir wakiimba nchini Ujerumani mapema mwezi June mwaka huu.

SIKILIZA WIMBO HUU

Efatha kwaya pia watakuwa wanazindua album yao mpya katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam tarehe 27 ya mwezi huu wa 9. Taarifa zaidi zitakujia.
Share on Google Plus

About Gospel Kitaa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.